Habari wadau,
Kwanza nianze kwa kutafakari kwanini shule za serikali haziongozi kwenye matokeo, kubali kataa sababu ni hizi.
1. Miundombinu na vifaa vya kufundishia.
2. Ufuatiliaji wa wanafunzi na mienendo ya walimu.
3. Mchakato wa kuwapata walimu na kuwafuatilia kwa ukaribu.
4. Mishahara...
Nakubaliana na wewe, serikali kama inatafuta walimu Bora ianzie kwenye matokeo ,wabadilishe vigezo vya kuwa mwalimu iwe kama unasomea rocket science, baada ya hapo hakuta kuwa na usaili kwa sababu walimu wanaomwagwa vyuo mtaani watakuwa wachache
Ajira kwa Sasa ni sawa na tatumzuka, ni uzalilishaji mtupu, kusoma kwa kutegemea kuajiriwa kunaongeza ufukara kwa wasomi, shahada saivi ni sawa na Bure.
Ni Bora mwanangu asomee kipaji chake na elimu ya pesa ambayo haifundishwi mashuleni.
Kazi ya ualimu ni ngumu kuliko unavyofikiria, kusoma kila wakati na huna ajira huu ni uchizi ni Bora nimalize chuo nisailiwe Kisha niende mtaani nikijua nimefaulu usaili kuliko Niko mtaani majukumu ni mengi eti nianze kusoma kwaajili ya usaili Tena bila mshahara inauma sana. Mtaani Kuna fursa...
Usaili sio kitu kibaya ila wanasaili watatajirika sana mkubali mkatae, usaili ni kama mpira wa penati , kukosa goli haimaanishi wewe sio Bora.
USHAURI WANGU
Kupata mwalimu Bora ni kumpima darasani Na matokeo ya wanafunzi akishindwa kwa mda Fulani uliopangwa anaondolewa hii Bora zaidi kuliko...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.