Kwa kweli hata mimi naungana nawe ndugu yangu. Nimejisikia aibu sana alipokuwa anadhihirisha upumbavu wake lakini pia na kushangaa anawezaje mtu kama huyu kuwa mbumbumbu kiasi hicho. Hata kauli zake dhidi ya Mtikila ni za kijinga. Yeye anafikiri baraka ni amani tu, hafikirii mahali nchi ilipo...
Huu ni ushahidi mmoja kati ya mwingi uliopo kwamba wanaotetea serikali 2 ni wafuasi vipofu wa dhana hiyo kwa kweli. Hata muasisi wake Mwl Nyerere katika mazingira haya ya sasa ya SMZ na katiba yake iliyofanyiwa marekebisho 2010 yaliyoitoa Zanzibar kwenye Muungano asingeweza kuitetea serikali 2...
Msingi wa Muungano ni hati yake ya makubaliano. Kutokuwepo kwa hati hiyo kunaondoa kabisa uhalali wa serikali mbili kwa sababu mfumo huu unainyima nchi ya Tanganyika uwepo na utambulisho wake ambao kwa kuwa hakukuwa na makubaliano halali ya kuiua haina budi kurudi. Walioiua Tanganyika walifanya...
Kwa kweli ipo haja wananchi tukemee hii tabia ya tbc kufanya upuzi huu. Masuala mazito kama haya wanathubutu kukatisha matangazo eti kisa wameshikwa pabaya! Any way wandugu mlio na link ya Dodoma tujulilsheni alivyomalizia Lisu Please.
Hiyo iko wazi kuwa ndugu hawa walijitungia tuhuma kukwepa ukweli. Hili kwa mwenye kufikiri linatosha kuonesha kuwa ama kwa hakika walipatikana pabaya ndiyo maana wakatafuta diversion kuficha uso kwa ajili ya haya. Kama wasingekuwa na hatia wasingeomba kujiuzulu. Hongera sana Cdm kwa ukomavu...
Nakubaliana sana na wewe ndugu. Ila kinachonishangaza ni jinsi wengi wasiovyoweza kuona hili, na hasa la kutokuwa na busara ya kutosha kuwa mwenyekiti. Wanadhani mtu kuweza kujenga hoja pekee kunatosha. Lakini pia hata huku kutaka sana madaraka ni dalili mbaya. Wengine tuliona tangu mwanza kuwa...
Ndugu mleta hoja, hii ni moja ya hoja zinazonipa kushangaa jinsi baadhi ya wenzetu mnavyo-react kwa mambo ya msingi na kusema haraka-haraka maneno makubwa bila kufikiri vya kutosha na kufanya uchambuzi wa jambo husika kwa makini. Hivi alichosema Mtei ni kipi cha kutosha kumlinganisha na...
Ulianza vizuri sana lakini mwisho wa hoja yako umejidhihirisha kuwa una fikra potofu juu ya Mh Mbowe. Pengine nia yako ni njema lakini umekosea kudhani kuwa mabadiliko ya uongozi yanatokea ili mradi tu ionekane kuwa watu wanapokezana madaraka. Uongozi ni vyema ubadilike kwa misingi ya...
Mzee Mtei anajua anachosema. Kujenga chama imara ni pamoja na kuwakomalia wanaokisaliti hata kama watu hao ni maarufu kiasi gani. Kilichoua ccm ni kuoneana haya inapofika kwa vigogo wenye majina. Mtu anayekaa kwenye chama kama kirusi ni hatari. Ni lazima "antivirus" ya chama ifanye kazi yake...
Ushauri ulioutoa kwa Nape ni wa muhimu kusikilizwa na wenzake wote walio na mawazo kama yeye. Kwa kweli mimi nilitarajia Nape awape pole wafiwa na majeruhi bila kuwasahau CHADEMA waliopigwa bomu kwenye mkutano wao, na sio kuwatupia lawama zisizo na msingi katika kipindi hiki cha majonzi. Huu sio...
Mimi nadhani kuwatwisha zigo kubwa USA kwa kuhisi tu ni kuwaonea sana. Pia ni kushoofisha juhudi za kupata ukweli wa mambo. Linapotukia jambo kama hili ni vyema kuwa objective katika kutafuta tatizo badala ya kukisia tu. Hivi kweli wanaosema tatizo ni USA hawazisikii DVD CDza uchochezi wa...
Kama cdm kikipuuza swala la kuwa na TV na Radio kitafanya kosa litakalokigharimu sana baadaye. Kujiweka kwenye mercy ya vyombo vingine vya habari badala ya kuwa na byako katika mazingira haya ya ushindani mkubwa namna hii ni hatari sana.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.