Sijui mzee lowassa yuko wapi. Hizi reply za hawa watu wanaotetea hilo agizo la RC zimenifanya nikumbuke vile vipaumbele vyake vitatu wakati wa uchaguzi wa 2015. Aliona mbali sana yule mzee
Kwanini tanroads wakimbilie kubomoa wakati jambo liko mahakamani?
Kama kweli wamejenga kimakosa si wangesubiri mahakama itamke hivyo kabla ya kubomoa?
Halafu tabia gani hii ya kubomoa bila taarifa na kuwanyima watu nafasi hata ya kutoa vitu vyao?
Nakumbuka plan ilikuwa kwamba ziwepo stand 3.
1. Boko- kwa mabasi ya route ya kaskazini.
2. Mbezi- kwa mabasi ya route ya magharabi, nyanda za juu kusini, ukanda wa kati hadi kanda ya ziwa
3. Mbagala- kwa mabasi ya route ya kusini
Ofcourse...maana maeneo ya tmk hadi mbagala ndio watu wa kutoka lindi na mtwara wanapoishi kwa wingi. Sasa fikiria eti unatoka lindi..basi lije likushushe mbezi halafu uanze kupanda daladala kurudi mbagala[emoji1787]
Mkuu nimegundua kuna watu hawalifahamu jiji la dar..ukubwa wake..population..na challenge kwenye public transport. Wanafikiri ni rahisi tu mtu kushushwa magufuli na kupanda daladala na mizigo yake..wakati basi inaenda huko huko kupark.
Kumbuka huu utaratibu wa kulazimisha abiria wote wapande na kushukia magufuli umeanza juzi tu...na ndio maana imezua mjadala. Mapema mwezi huu wakwe zangu walinitembelea kutoka arusha na walishukia gomz na kuondokea gomz na ester luxury..ilitoondolea usumbufu wa kwenda hadi magufuli stand...
Issue siyo stand iwe wapi (wengine tulipinga kuhamishiwa mbezi lakini tushakubali imejengwa huko)....issue ni kwanini abiria wote walimishwe kupanda na kushukia hapo. Kama basi liko tayari kupakia na kushusha abiria wanaoishi karibu na yadi ilipo kuna ubaya gani? Basi lazma litapita mbezi na...
Hiyo stand kuwekwa huko mbezi hadi CAG alipofanya audit akasema haikua decision nzuri. Lakini basi ishajengwa...mabasi yote iwe lazma kupita kabla ya kuanza au kumaliza safari..lakini wasipigwe marufuku kusaidia abiria wanaotaka kwenda kushushwa karibu na basi inapolazwa.
Lakini pia...lengo...
Kumbe kweli wewe hulifahamu jiji..unatetea jambo ambalo hufahamu madhara yake kwa abiria.
Naomba siku upande basi uje dar likufikishe magufuli stand saa 1 usiku halafu ufanye mpango wa daladala hadi chanika. Halafu kurudi utoke chanika na daladala uwahi basi magufuli linaloondoka saa 12...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.