Mimi nimesema mara nyingi kama CCM inaendelea kuitawala Tanzania hakutakaa kuwe na mabadiliko ya kweli. Mwisho wa siku ni ulaghai tu. Unamchukua mtu huko hajafanya kitu ameshapewa uwaziri nchi ya kugawana tu hii. Viongozi wa kweli na raia wananyimwa haki zao mchana kweupe. Mungu hatatulia...
Mzee wa watu kakurupuka akidhani anayaendea majipu! La! kumbe cancer tupu. Magufuli hafiki popote ni mjinga tu anayeweza shabikia haya mambo. Wenye na akili zao wameshahamia kando wanaangalia tu cenema za bure Tanzania.
Mi ni mzaliwa wa Songea lakini nimefurahishwa sana na usemi wako wa watu wa kaskazini. Embu fafanua kidogo mleta mada je huku jamvini tunakuja na alama za namna gani zinazotutofautisha kikanda?
Kama huyu Muhongo hakuhusika na alikuwa innocent kiasi hicho ni kwa nini alijiuzulu? Yeye kama waziri...
Ulishamsikia Lowassa akija hapa kumsema yeyote? Hivi wewe mama yako hakukufundisha apandaye juu mngoje chini? Lowassa anajua hakuna pale Magufuli anaenda na CCM yake. Tena watamhujumu gizani ile mbaya kwa kujificha. Ni afadhali walipoiba kwenye mwanga wakigawana na marambo mchana kweupe. Sasa...
Unajuaje kama umtukanae ni BAVICHA? Kwani ana alama hapa? Huyu Magufuli wako atahangaika na vijipu kadhaa, lakini cancer ya CCM imemshinda tayari. We ngojea uone upinzani utakavyoshamiri mara hii kwani watanzania wanaamka kila kukicha.
Watanzania tumezoea kusifia moto wa mabua. Tutulie dawa ituingie sawasawa. Huko aliko Lowassa anachekaa tuuuu maana kuna wengi wameshakuja hapa kumdhihaki kama kwamba Tanzania inaongozwa na malaika kutoka CCM. Wapendwa, Chama Cha Majipu hiki! Tulitegemea lipya kweli?
Leteni akili zenu zote hapa...
Chama Cha Majipu? Chama Cha Makomeo? Chama Cha Mapombe? Chama Cha Mawaziri. Hii Tanzania inaendeleaa kugeuzwa shamba la BIBI Mzee? Ni lini tutaamka tuwatimue hawa wezi wanaotumalizia nchi eti mabadiliko! Ni nini kimebadilika hapa? Tutadanganywa mpaka lini?
Hakuna watu wajinga na wanafiki kama watanzania. Hivi hizi barabara za Magufuli alizojenga chini ya viwango kiasi hiki hazitoshelezi tu kuelewa kuwa hana lolote kwa nchi hii? Mnashabiakia vitu vya kijinga tu kama watoto wa Kindakenda. Magufuli kama ataenda na hii CCM anavyoenda ataishia pabaya...
Huyu ni kiongozi wa Chama Cha Majipu aliyefikiri watanzania watalala daima. Kipaa kimeruka maradufu maana mwenye na nchi kashaamka saa tisa usiku ni kutumbua majipu kwa kwenda mbele. Siku atafikiwa atakufa kwa heart attack.
Tanzania watu wanakimbilia vyeo ili mradi wanapata kula ya bure. Nawakumbusha comment yangu ya huko nyuma. Spika, Naibu Spika na wengine wengi tu waliokimbilia vyeo bila kujichunguza na kujijua wataishia kuumbuka kwa kujivua wadhifa zao hivi karibuni. Kama hii haitatokea nitajua hapa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.