Hii inategemea sanasana na wewe unatokea wapi. Mara nyingi kama unatokea Mwanza gharama zinakuja kidogo Kwa kulinganisha na ukitokea Arusha. Hii ni Kwa sababu kutokea Arusha kwenda Serengeti ni lazima upitie HIFADHI ya Ngorongoro ambapo utalazimika kuilipia tozo kadhaa. Vile Ile utatumia muda...
Hii pia ni chaguo zuri Kwa wale wenye budget ndogo ambapo itakugharimu angalau shilingi elfu 45 ya nauli kutoka Arusha Hadi Mugumu, Musoma au Tarime kupitia Ngorongoro na Serengeti. Tatizo la kutumia njia hii ni kwamba utawaona wanyama wale tu walioko pembeni ya barabara. Kwa vivutio vingine...
Mkuu 90km Kwa Serengeti ni chache sana. Kumbuka Ina ukubwa wa zaidi kilomita za mraba elfu 14. Eneo kubwa ni tambarare tu yenye nyasi ndefu na wanyama wachache. Hivyo basi Ili uifaidi vizuri inakubidi utembee eneo kubwa zaidi.
Karibu sana tukuhudumie msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya.
Samahani Kwa kuchelewa kukujibu mkuu.
Kwa ufupi safari hii itakuwa ya 7 days na 6 nights. Kwa mtazamo wangu naona itakuwa vizuri kama ukilala lodges za bei nafuu. Kwa siku hizo sita ndani ya Serengeti pekee itapendeza kama ukilala kwenye lodges/hotel angalau tatu tofauti katika maeneo tofauti...
Tanapa hawana guides, ikitokea ukaenda bila gari hautaruhusiwa kuzunguka hifadhini. Sanasana watakuunganisha na kampuni binafsi Ili upate gari. Gharama zinaweza kuwa kubwa zaidi kulinganisha na endapo utapanga safari mapema na kupat gari.
Karibu.
M nawapokea watu upande wa Ikoma gate iliyoko jirani na mji wa mgm ila kutokea mwanza nikarb maana ukitokea Arusha itakuradhimu kufk mpaka mjin mgm ndipo uludi Tena hifadhini mkuu maelezo zaid 0625818341
Hiyo 50k inaweza kuwa tozo ya gari tu mkuu, mtu wa kukuzungusha itabidi uongeze angalau 50k nyingine. Na Chakula uzingatie pia.
Wafanyakazi wa serikali hawausiki kukuzungusha, ni watu binafsi kama sisi yaani tour guides.
Karibu tukuhudumie. 0625818341
Kwa mtanzania kuingia hifadhini gharama ni elfu kumi na Moja na mia nane (11,800/=). Hiyo ni tozo ya kiingilio tu. Tatizo ni kwenye usafiri ndugu. Hapo ndipo zinapojitokeza gharama ambazo wengi hawazimudu.
Serikali Haina magari kiivo kusema ndo yatumike kukuzungusha kutalii. Endapo yangekuwepo...
Unachosema ni ukweli kabisa lakini kutokana na mazingira ya kuwafikia hao nyani ndipo tofauti zinapojitokeza. Pengine inakua bure, pengine unalipia. Kwa mfano, Mimi nilieko Serengeti haiwezi kuwa bure kuja HUKO udsm kuwaona hao nyani. Lazima nigharamike, nilipe nauli, chakula na hata kulala...
Inaweza pungua kama nilivyofafanua ila huduma inakua siyo nzuri kiivo. Tatizo ni gharama ya kukodi gari, kuweka mafuta na kuilipia tozo ya kuingilia hifadhini.
Karibu mkuu!
Kiuhalisia gharama unazolipa ni kwaajili na kuwafanya waendelee kuwepo, yaani gharama za uhifadhi. Hizo gharama nyingine ni kwaajili tu ya kuweka mazingira rafiki ya kufikapo. Karibu sana.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.