Habari ndugu zangu,
Asante kwa wote mliolia nami katika kifo cha binti yangu mpendwa aliefariki kwa uzembe wa watu wa afya, faraja yenu ilikuwa tiba sana sijaamini JamiiForums kuna watu wana roho nzuri hivi na wanaumia kwa matatizo ya watu.
Maisha baada ya maziko yamekuwa magumu sana muda wote...
Inauma ...inauma nikama moyo unavuja damu natafuta angalau mtu aushike usivuje aniambe pole tu iniponye maumivu haya ya milele, mtoto mdogo alieonja maisha alifariki kwa mateso makali mbele yangu ni kitu ambacho kili wakati kinajirudia napoteza hamu ya aya maisha kabisa...nimemzika mwanangu kwa...
HOSPITAL IPO DAR ES SALAAM , WILAYA YA ILALA NI YA SERIKALI....IPO BARABARANI KAMA UNAENDA KARUME....MTOTO ALIKUWA NA JOTO TU NA ALIFIKA MZIMA KABISA LAKINI YALIYOTOKE NIMESHTAKI KWA MUNGU ATAAMUA YEYE NDIO ANAJUA NAPITIA YAPI MANESI NA DOKTA SIWAJUI KWA JINA ILA SURA ZAO SITAZISAHAU NA OFISI...
Naomba niulize nikitaja hospital itamrudisha mwanangu? Namba sihitaji mchango nahitaji msaada wa kiroho au mwana saikolojia nahisi roho yangu inatoka sijatumiwa na mtu hata 100 wala sijaomba pesa ya mtu punguza ujuaji kwenye masuala ya watu
Naomba mwandishi mmoja mzuri aneweza kuandika anaitafute nimuelezee mwanzo mwisho yeye ndio aandike mimi sijaja kuomba au kumwambia mtu nimelia uchungu huishe lakini hauishi naitaji faraja hata ya maneno wana jf naumia sana jamani nafarijika nikisoma pole
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.