IOGT sio branch ya scout ya Tanzania, faida ziko nyingi lakini yaelekea umeamua kujikita kwenye mbili na lugha za kiskauti Si za JF, zinafundishwa kambini tu. Kama wewe ni skauti unapaswa kujua hilo.
IOGT ni taasisi moja na TSA ni nyingine, sina hakika na utofauti gani unaouulizia. Kama umeamini kuwa hakuna faida zaidi ya kuingia bure 77 kwa nini unauliza? Kama unazijua lugha za kiskauti kwa nini unauliza. Kwa nini unahutaji kujua cheo changu? Imebidi nikutwange maswali kwa sababu umeuliza...
Hata marais wengi duniani wamepitia skauti! Tunapoendelea kutafiti juu ya uhusiano wa uskauti na urais wa nchi; na wewe endelea kutafiti uhusiano wa uskauti na ugaidi.
Shallow kwa dimension gani? Kila ulicho uliza nimekujibu isipokuwa suala la bajeti. Ukija na swali vague ukategemea kupata jibu detailed wewe utakuwa 'mzuzu' kwa lugha ya kiskauti
Syllabus ya skauti inaundwa au kubuniwa na skauti wenyewe, kupitia timu ya kiufundi ya kimataifa au kitaifa. Kuhusu tija gani, nikupe mfano mmoja tu rahisi, kwa sasa skauti wako mstari wa mbele jijini Dar wakisaidia na kuokoa watu waliokumbwa na mafuriko. Mengine ni mengi kwani lengo la kwanza...
Skauti haruhusiwi kumpiga mtu yeyote; kwa sababu yoyote ile. Hao waliompiga mwenzao; ilikuwa ni ugomvi? Iliwapasa walimu katika shule husika kushughulikia suala hilo kwa taratibu za kinidhamu.
Ndugu SPANISH CP
Skauti sio chama cha kisiasa kwa hiyo siwezi kujibu swali la uhusiano kati ya skauti na CCM, na wala sijui mtoto wa Kikwete ana cheo gani kwenye Scout Tanzania. Mbunge wa Mafia Mh. Abdulkarim Shah ni Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania.
Chama kina miradi ya kujiingizia kipato, so hakitegemei misaada tu kama inavyodhaniwa na wengi. Jengo lilinusurika kutokana na madeni ya siku zilizopita, halitaporwa tena kulingana na mikakati iliyopo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.