Alhamisi ya pili ya Mwezi Machi kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Figo Duniani ili kutoa ufahamu na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa afya ya figo na magonjwa yanayohusiana na figo. Kupitia maadhimisho haya, watu hupata fursa ya kujifunza kuhusu njia za kuzuia magonjwa ya figo, kudhibiti magonjwa ya figo, na umuhimu wa kuwa na maisha yenye afya ya figo.
Aidha, maadhimisho haya huchangia katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu haja ya kuchangia katika juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa ya figo, pamoja na kusaidia watu wenye matatizo ya figo kupata msaada unaohitajika.
Hata hivyo, ugonjwa huu huambatana na dhana nyingi potofu zinazofifisha kasi ya kupambana nao hivyo JamiiCheck imekuandalia ufafanuzi wa Dhana hizo kama sehemu ya...