Zoezi la Vitambulisho kugomewa?...

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
-Kwa kuwa zoezi la vitambulisho vya Taifa linawahusu Watanzania wa dini zote,

-Na kwa kuwa kupata kitambulisho kutamfanya mtu apatikane kila akitafutwa,

-Na kwa kuwa kitambulisho cha mtu hakionyeshi dini yake,

-Na kwa kuwa zoezi la vitambulisho linafanana-fanana na Sensa,

Ndugu zangu Waislamu(wenye mpango wa kugomea sensa) wanaonaje wazo la kugomea

Vitambulisho vya kitaifa,
ambavyo ni vya kudumu, kuliko kugomea Sensa ya Watu na Makazi,

ambayo inadumu kwa muda wa miaka 10 tu?

Naomba mwongozo wa hoja hii!
 
haaahaa watu mna visa nyinyi....wengine wanaanzisha haya mazogo ili wapate kula si unajua tena
 
Waache wagomee vitambulisho. Siku itafika watakapotozwa faini mahakamani kwa kutokuwa na kitambulisho. Na vile vile kutokutambulika kama raia wa Tz. Huduma zote za umma watakosa. Wanaoleta hii fikra wafikirie zaidi sio kusema na kudanganya watu.
 
-Kwa kuwa zoezi la vitambulisho vya Taifa linawahusu Watanzania wa dini zote,

-Na kwa kuwa kupata kitambulisho kutamfanya mtu apatikane kila akitafutwa,

-Na kwa kuwa kitambulisho cha mtu hakionyeshi dini yake,

-Na kwa kuwa zoezi la vitambulisho linafanana-fanana na Sensa,

Ndugu zangu Waislamu(wenye mpango wa kugomea sensa) wanaonaje wazo la kugomea

Vitambulisho vya kitaifa,
ambavyo ni vya kudumu, kuliko kugomea Sensa ya Watu na Makazi,

ambayo inadumu kwa muda wa miaka 10 tu?

Naomba mwongozo wa hoja hii!

kama website ya TTB, Diary za ofisi ya wzr mkuu watatumia data za NIDA watagomea pia
 
Australia waligomea Vitambulisho serikali ikasema asietaka
kuchukua kitambulisho hataweza kununua shamba, kufungua account,
kutibiwa, kupewa leseni au kupewa huduma yoyote bila kitambulisho, walifyata mkia
kwa Tanzania wakigomea serikali itatumia mabavu kama hayo lazima kuwa nacho
waislamu najua ni upepo tu utapita kuhesabiwa watahesabiwa sana.
 
Sisi waislamu wote tuandaane haiwezekani serikali hii itunyanyase hivi nilikuwa sijasoma vizuri zile nyaraka zao ambazo ni nyingi mno na zinachosha ....kumbe hicho kipengele hakipo?...lazima waweke kipengele cha dini ili kila tukiomba kitambulisho cha mtu tuwe tunajua dini yake.....
Sisi waislamu ktk hili hatutakubali mpaka kieleweke yaani ni jino kwa jino na ngangari kinoma nadhani wote mnatujua sisi waislamu tukisema hatutanii na mmeona tulivyo gomea sensa na mnakumbuka mambo ya uamsho huko zenji kwa hiyo serikali lazima iheshimu matakwa yetu
 
hakuna mtu atagoma katika hawa watu(islamic)sema kunawajanja wachache tu wanataka wajulikane tz hii na kwakuwa wanapata washabiki actually wameshajulikana.
ninauhakika hakuna atayegoma kuandikishwa sensa.mark my words
 
Nilimsikia Mbunge mmoja katika maongezi ya kawaida akieleza kuwa zoezi la Sensa, Vitambulisho vya taifa na Katiba vingefanyika kwa ufanisi, kwa gharama nafuu, kwa kuokoa muda na rasilimali na kuwafikia watanzania wote kwa wakati endapo yangefanyika pamoja.
Naunga mkono kabisa.
Isingekuwa ngumu kwa karani wa sensa pamoja na fomu za dodoso, kuwa na fomu za vitambulisho vya taifa na fomu ya tume ya katiba kwa ajili kujaza maoni.
Nimetafakari nikabaini kuwa hili lingewezekana tena kwa ufanisi mkubwa.
Tuchangie !

NB:
Naomba MoDs wai stick hii topic kwa faida ya siku zijazo.
 
Back
Top Bottom