Ziwa Nyasa ni milki halali ya Malawi

Nimesikia kuna mafuta wa Waingereza ndiyo shinikizo usiniulize source.
Mh! Hapa kuna kaukweli nn!? Maana wakati flani nikiishi Njombe kuna jamaa mmoja fundi wa magari alikuwa akitengeneza gari za bos wangu Muingereza ambaye kwa mujibu wa dreva huyo Bosi wangu pamoja na wenzie walikuwa wakipiga tripu za siri ziwa nyasa kupitia Ludewa wakiwa ma diving equipments...anadai walikuwa wakitumia diving equipments katika ziwa hilo.

Bosi wangu huyo wa zamani ni Muingereza ambaye baadaye pia aliwahi kuondoka nchini kwa sababu zisizofahamika wazi ila fununu ni kwamba wakuu wa nchi walimwondoa kwa sababu Maalumu kabisa.

So ulipozungumzia hili nikaunganisha na story za fundi yule na namna bosi wangu yule walivyoondoshwa nchini ndani ya masaa 48 napata hisia flan Amazing hivi.
 
Town centre ya wilaya ya kyela haikuwa hapo ilipo sasa bali ilikuwa kwenye kijiji fulani kinaitwa lugombo(umbali wa km kama 40 kutoka kyela mjini ), kilichofanya town centre ihame kutoka lugombo mpaka ilipo sasa ni baada ya ziwa kusogea na kuharibu miundo mbinu na makazi ya watu. Kwa hiyo mpaka wa ziwa hauwezi kuwa maji maana maji yanahama.
 
Nchi hii ilivyoya ajabu utashangaa ziwa tunanyanganywa kizembe na kuwaachia wenzetu wakaneemeke tz ni nchi ya maajabu sana hatuvijali vilivyo vyetu.
Kama hapo zenj mafuta chukua, umeme pata kwa bei ya kutupa, kazi zetu kwa mambo cio ya muungano, kogamboni wamefanya kipande kisiwa hicho. Zenj yao, tz yetu. Ati tumechanganya damu bc wawe mkoa au kanda. Kwa utaratibu huu nakubaliana na wewe mkuu tunaweza kuwachia. Membe yuko wapi jamani alikuwa na msimamo dhahiri.
 
Pia tuwe makini tunapojenga hoja huko katika vyombo vya kimataifa tunapodai sehemu yetu ya Ziwa!

Kimsingi sisi hatudai 50% ya ziwa, ni makosa kusema kuwa eti tunadai nusu ya ziwa! kwa sababu kimsingi 30% ya hilo ziwa tayari ipo msumbiji tunachokigombania sisi na Malawi ni takriban asilimia 70 au 75 hivi iliyobaki
. SISI TUNACHOKIDAI NI MPAKA ULIOPITA KATIKATI YA ZIWA!
 
Sina haja ya kusoma chochote, hiyo ni International law kwamba chochote kilichoko mpakani kinamilikiwa na nchi zote, hilo halina mjadala!
mkuu
ziwa haliko mpakani..malawi wanasema kuwa ziwa lote ni lao na kama ndivo ilivo hivo..maana ake hiyo international law haiwezi kuwa applicable hapo
 
mkuu
ziwa haliko mpakani..malawi wanasema kuwa ziwa lote ni lao na kama ndivo ilivo hivo..maana ake hiyo international law haiwezi kuwa applicable hapo


Una maanisha nini unaposema halipo mpakani? Hiyo ramani yao (Malawi) inaonyesha mpaka uko ndani ya ardhi ya TZ yetu au lilipoishia Ziwa?
 
Pia tuwe makini tunapojenga hoja huko katika vyombo vya kimataifa tunapodai sehemu yetu ya Ziwa!

Kimsingi sisi hatudai 50% ya ziwa, ni makosa kusema kuwa eti tunadai nusu ya ziwa! kwa sababu kimsingi 30% ya hilo ziwa tayari ipo msumbiji tunachokigombania sisi na Malawi ni takriban asilimia 70 au 75 hivi iliyobaki
. SISI TUNACHOKIDAI NI MPAKA ULIOPITA KATIKATI YA ZIWA!
Wamalawi walipewa sehemu ya nchi kavu ya Msumbiji wao wakatoa ziwa Malawi, maji. Hawana shida nayo. Ninachosema mie, tusiende mahakamani, ICJ, watatupiga. Tutumie equitable principle tu....half letu, half lao.!!
 
Jaribuni.
ustadhad faizza salaam..
umekuwa na jazba sana juu ya hili suala nakusihi punguza munkari ...
kwanza nikuulize unajua kwa nini malawi wanasema ziwa ni lao...??
kuna mambo mengi sana hayaja andikwa kama ambavo wazee wetu waliopigania uhuru hawajatajwa..
tanganyika ilipora sehemu nying tu..mfano mwengne ni juu ya zanzbar..hivi unajua zanzbar ilikuwa ina nautical miles nying baharini kuliko tanganyika??
sasa ukiona watu wanakomaa na vitu wanasababu nyingi tu
 
Malawi wakibeba ziwa letu naomba naramani ya dunia ibadirishwe.....walikuwa wapi miaka yote iyo wanatuona sisi ni makoro siyo?
 
Ukifanya fujo,
umeambiwa usifanye hiki,
ukaamua kukaidi, utapigwa tu...
hamna namna nyingine, maana
wote tukubaliane kwamba nchi hii
tunaiendesha kwa misingi ya
kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki
unaona kwamba ni imara zaidi...
wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga
tu.... Mimi nasema muwapige tu,
kwa sababu hakuna namna
nyingine... maana tumechoka.”
 
Duuuuh angekuwepo mtangulizi madarakan ingekuwa raisi kidogo huyu mheshimiwa dokta anaweza akatuma jeshi tu maan internatonal diplomacy hana kabisaaaa
 
Wamalawi walipewa sehemu ya nchi kavu ya Msumbiji wao wakatoa ziwa Malawi, maji. Hawana shida nayo. Ninachosema mie, tusiende mahakamani, ICJ, watatupiga. Tutumie equitable principle tu....half letu, half lao.!!

Hawawezi kutupiga kwa sababu

(1) Tanganyika halikuwa koloni la Mjerumani kuanzia 1919- 1961, Laiti Mkataba wa Heligoland ungekuwa applicable basi mkoloni wetu angekuwa ni mjerumani throughout!. Lakini kitendo cha sisi baadae kutawaliwa na Muingereza kinyume cha mkataba wa Heligoland uliotuweka sisi Kwa Mjerumani basi ni ushahidi kuwa Heligoland Treaty ilivunjika baada ya vita ya kwanza ya dunia.

2. Muingereza Mwaka 1922 wakati akiitawala Tanganyika baada ya vita kuu ya kwanza alihamisha mpaka wa Tanganyika na kuuweka katikati ya Ziwa, huu ni ushahidi kuwa Heligoland treaty ilikuwa abbrogated na mshindi, Hata hivyo muingereza aliurudisha mpaka ufukweni miaka michache kabla ya Uhuru, hii ya pili ni haina effect kisheria kwa sababu baada ya vita ya pili ya dunia sisi Tulikuwa Proctorate territory , Haikuwa halali kwa Taifa angalizi kubadiri mpaka wa Proctorate territory!

3. Tukienda katika International law, Maji ya Mpakani baina ya mataifa mawili mpaka unapita katikati!

4. Tayari tulishatuma diplomatic note toka enzi hizo kuwa sisi hatuna claim zaidi ktk ziwa Nyasa isipokuwa mpaka unaopita katikati.
 
Una maanisha nini unaposema halipo mpakani? Hiyo ramani yao (Malawi) inaonyesha mpaka uko ndani ya ardhi ya TZ yetu au lilipoishia Ziwa?
Hii ni sawa na tanganyika kuitawala zanzibar kupitia muungano lakini sifikirii wamalawi watakubali kutawaliwa kupitia ziwa nyasa.
 
Back
Top Bottom