Zitto: Watanidharau, watanicheka, watapambana lakini nitashinda!

ZZK for sure you need a Break. Kwa sasa we know un abifu na Prof. Upo impaired u cany judge well. Hii vita upo peke yako huku wanafiki wanaojua wataibika wakikusupport. Angalia Kaka dunia haina Siri.

He needs a break into explaining what people been thinking kuwa ndo alichomaanisha au? why don't you discuss the substance of what amekileta kwetu? Stop attacking him, u are the 1 to be given a break. Bifu na Waziri linakuja kwa sababu gani haswa? Umesoma vizuri alichoelezea Zitto au una attack tu? Na hautaki watu wamsapoti ili wasije kuonekana wanafiki, shame on you...Demokrasia unaijua????
 


Ni MANTIKI GANI Ilimfanya huyo ZITTO KABWE kukingia kifua na kumtetea MWIZI yuke MKURUGENZI wa TANESCO bila Hata ya kumfanyia UCHUNGUZI kama MMOJA wa COMMITTEE ya NISHATI BUNGENI ?
ALIKUWA anataka kuficha nini ? HIVI ANAPASWA KUWAOMBA RADHI Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar au
Atainyamazia kimya kama Viongozi wa Chama tawala cha CCM Wanavyofanya --- KUNYAMAZA KIMYA ILI YAPITE ? Hajui Hatua yake iliwadhuru Wananchi ? Ambao angependa KURA ZAO ? Sasa kama kawaida yake AKATUTANGAZIA kuwa Wataizima GENERATOR iliyoko NYUMBANI kwa Mr. MHANDO ili ajue Uchungu wa kutokuwa na Umeme, lakini hiyo ilikua vunga wananchi... alimbakiza pale pale kuendelea KULA pesa za NCHI... ZITTO KABWE atatueleza ya kuwa huo sio U-MIMI MIMI MENTALITY ? NI KIJANA NDIO; NI MSOMI NDIO; Lakini faida yake ni kwa nani ? MAFISADI Wachache ? au Wananchi ? Kama ni Wananchi, aende kwenye VYOMBO vya HABARI na kulizungumzia SUALA la kumpigia kifua Mr. MHANDO...



View attachment 67912

Unakumbuka issue ya Dowans Zitto Kabwe aliongea nini na mkamuita fisadi na mla rushwa? Kama haukumbuki katafute majibu, ulinganishe na what is transpiring now, halafu uje tuongee.
 
Unakumbuka issue ya Dowans Zitto Kabwe aliongea nini na mkamuita fisadi na mla rushwa? Kama haukumbuki katafute majibu, ulinganishe na what is transpiring now, halafu uje tuongee.

Ni mimi nimeandika SIO KUNDI LA WATU tafadhali sana rekebisha hilo... aliishia WAPI na DOWANS ? Iliishia kama VILE Signature za kutaka Waziri Mkuu ajiuzulu ?
 
Ni mimi nimeandika SIO KUNDI LA WATU tafadhali sana rekebisha hilo... aliishia WAPI na DOWANS ? Iliishia kama VILE Signature za kutaka Waziri Mkuu ajiuzulu ?

cheki unavyojibu kwa jazba, shushia na maji ya kunywa kwanza halafu rudi mkuu. Ni hoja tu sio vita.
 
mkuu pole sana,naona kamjamaa kamekubana maswali,unaishia kujikanyaga kanyaga tu.JIBU SWALI BWANA USIKWEPE.

Na nikijibu Zitto Kabwe atawaomba msamaha wananchi kwa kumlinda Mhando au atapanda ndege na Rais Kikwete Kuonyeshwa JINSI ya KUKAA akiwa RAIS na kupungia kwa MARINGO ?
 
Zitto ni mwanasiasa wa level nyingine kabisa,hata hata kama hatumpendi..truth be told! Majibu yake huwa ni facts to facts. Kama sivyo,inakuwaje vigumu kujibu au kukanusha kuwa haya anayosema especialy juu ya rasilimali nza madini,mafuta na gesi? Badala yake mnakimbilia kuleta personnal attacks na kuhama kwenye hoja. Wanasema anafanya mambo kibinafsi,ni ujinga tu kwa sababu kila mtu ana fikra na mawazo yake katika kuchanganua,na uwezo unatofautiana kati ya mtu na mtu. Ni upumbavu wa hali ya juu kulazimisha binadamu awe na styles of thinking! Unless kama CDM kuna njia rasmi ya chama kufikiri mpaka iwe kosa kwa mwanachama kufikiri na kutoa maoni yake katika mambo mbalimbali katika mustakabali wa taifa.
Yaani kila nikisoma michango ya pro-Chadema na anti-Zitto huku jamvini huwa napata taswira nyingi sana za watanzania. Natamani siku moja watanzania waanze kufikiri kiuhalisia tofauti na kufikiri kimazoea. Watu wamejikita ku-block ideas za watu makini badala ya kupambana kwa hoja.
 
sikujua jf ina vilaza wengi namna hii, yaani badala ya kujadili hoja wanamjadili aliyeitoa tena kwa maneno yasio na ushaidi.
Kwa namna hii tanzania hatufiki popote.
 
Ukweli siku zote haujifichi, at long last kila kitu kitakuwa wazi
 
mkuu huu mjadala ulikuepo hapa nadhani mwezi mmoja uliopita,unachosema siyo kweli. unajua wakati mwingine baadhi yetu tunaishiwa busara,tunaongozwa na chuki na hasira matokeo ni kuandika hoja dhaifu kama ulivyofanya.

Acha kuleta longo longo jibu hoja ; kipi nilichosema sio kweli kitaje na ni vipi naongozwa na chiki, kwa kuonesha undumila kuwili wa Zitto? Mimi najua nina busara na ndio maana I am focused kwenye issues bali wewe ndio unaleta mambo ya Zitto the person!! Common grow up!! Kama unadhani nimeandika hoja dhaifu mbona hujaijibu umebakia kulalama tu.
 
Naamini zito anajua mambo mengi kwenye sekta ya madini kuliko waziri Mhongo,ndio maana anathubutu kumwita mwongo.. Zitto anajua madudu mengi kwenye hiyo sekta yaliyofanywa na serikali hii,hivyo haamini kama serikali hii inaweza kujisahihisha.
 
Sijawahi kuwa karibu na ZZK zaidi ya kusoma vinavyoandikwa juu yake, kusoma makala zake, kutembelea mitandao, kuongea na watu na pia utafiti binafsi. Zitto kwa jinsi ninavyomuona mimi ni msomi, au anaonyesha usomi katika vitu anavyoviongea - sijui kuhusu anavyovifanya. Kwa sisi tunaopiga kura kutokana na kusikiliza watu nadhubutu kusema kwamba Zitto ni mwanasiasa, mwanaharakati, mtafiti na nimuelemishaji. Hebu kwa mda flani tuache kumjadili na badala yake tuyatafakari aliyowahi kuyasema na anayoendelea kuyasema pamoja na matokeo yake.

Je, bila yeye kutembeza daftari la kutafuta sahihi 70 ili kumuondoa Waziri mkuu JK angevunja baraza la mawaziri? Je bila yeye na wenzake kupiga kelele kuhusu mgao hadi sisi kuijua Richmond, kuundwa kwa kamati ya Mwakyembe Lowassa si angekua bado ni Waziri Mkuu? Kama si Zitto na upinzani kueleza ubovu kwenye mikataba ya madini sheria mpya za madini pamoja na kamati ya Bomani vingekuwepo kweli?

Ni muhimu kujua kwamba kila Mtanzania ana haki ya kuwa raisi. Obama alitangaza kuutaka uraisi 2005 mara tu baada ya uchakuzi alioshinda Bush 2004. Tokea hapo Obama alikua katika campaign za urais hadi 2008 alipopambana ma Mama Clinton akamuangusha kwenye uchaguzi wa ndani na kuingia kwenye kinyang'anyiro kikuu cha uraisi na akashinda 2008. Hapa kwetu majirani zetu Kenya kuna kijana anaitwa William Ruto. Yeye Ruto hajawahi kugombea urais. Lakini mwaka 2007-2008 mara tu baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya Ruto alitangaza nia yake ya kugombea uraisi wa Kenya 2012 (uchaguzi umesogezwa hadi 2013). Wakati akiyasema haya Ruto alikua bado ni mwanachama wa ODM, inayoongozwa na Raila Odinga.

Tumuacheni Zitto Kabwe afanye kila anachokiona ni bora kwake. Cha kujiuliza labda ni usahihi wa anayosema na kuyataka na kwa maoni yangu mimi yuko sahihi. Katiba (ya chama chake - CDM pamoja na ya nchi) inamruhusu kutoa maoni na kugombea Uraisi.
 
ZZK siku za ujinga zilishapita. Wewe ni msaliti mkubwa sana. Unachokitafuta kila mmoja wetu anakijua. Tulia kabisa tutamchagua rais tunaemjua na ambaye atatuletea mabadiliko ya kweli. Wewe komaa kwanza na ujifunze jinsi uongozi wa kweli ulivyo tofautiana na ubinafsi! Watanzania wengi tumeshaelimika!
 
Makala safi tatizo tu wanasayansi wetu mnatuangusha. je popo ni mnyama au ni ndege au si mnyama na wala si ndege?
 
Kwa hapa naona ZZK yuko sawa kabisa sisi tunachezewa akili zetu hauwezekani mtu aseme hakuna mgao tena halafu unakuja tena kwa kasi

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Nimependa Article hii chini
Unafsi wa Zitto na wapinzani wake

Kitila Mkumbo

Toleo la 262
10 Oct 2012
















KATIKA siku za hivi karibuni kumetokea malumbano kutokana na uamuzi wa Zitto Kabwe kutangaza kwamba atagombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao. Katika kutekeleza azima yake hiyo ametangaza pia kwamba hatogombea tena nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini. Ikumbukwe kwamba hii si mara ya kwanza kwa Zitto Kabwe kutangaza kutogombea ubunge huko Kigoma Kaskazini.
Mwaka 2007 akiwa ziarani nje ya nchi alitangaza kwamba asingegombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2010. Hata hivyo aligombea na akashinda na ni mbunge hadi leo hii. Nitaeleza baadaye katika makala haya nini maana yake kisiasa na yeye mwenyewe Zitto ni mwanasiasa wa namna gani.
Watu kadhaa ndani na nje ya CHADEMA wamehamaki baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombea urais. Wengi wa wanaopinga kauli ya Zitto wanaipinga kwa minajili kwamba ametangaza mapema na kutangaza huko kutasababisha mgogoro, mgawanyiko na fujo katika chama.
Hamaki hii imekolezwa zaidi na mwasisi wa CHADEMA na mwanasiasa mkongwe hapa nchini, Mzee Edwin Mtei, ambaye amesema kwamba hatua ya Zitto kutangaza mapema kugombea urais ‘itasababisha mzozo na mpasuko’ kwa kuwa wapo wanachama wengine pia wanaoutaka urais. Kuna wengine ambao wamemuona Zitto Kabwe kwamba ni mbinafsi anayejijali zaidi yeye bila kujadili mustakabali wa chama chake.
Wengine wameenda mbali zaidi na kusema kwamba Zitto Kabwe amenunuliwa na anakitumikia Chama cha Mapinduzi na kutangaza urais ni moja ya mikakati katika kufikia azima ya kuidhoofisha CHADEMA. Katika makala haya ninajadili mantiki ya hoja hizi na kuanisha kama uamuzi wa Zitto kutangaza kugombea urais ni jambo la afya kwa CHADEMA na demokrasia yetu au la.
Pamoja na kwamba nami pia siungi mkono tabia ya wanasiasa, hasa katika CHADEMA kutangaza katika muda huu kugombea urais, siwaoni wanasiasa hao kama wanakikosea chama chao kufanya hivyo. Aidha, siwaungi mkono kabisa wale wote wanaompinga Zitto Kabwe kutangaza kuutaka urais katika kipindi hiki.
Siyaungi mkono makundi haya kwa sababu nadhani kwamba yanaenda kinyume cha utamaduni wa kisiasa tunaojaribu kuujenga ndani ya CHADEMA. Kimsingi, makundi yote mawili, Zitto na wapinzani wa tabia zake, wanaendekeza unafsi, jambo ambalo CHADEMA wanajaribu kulikomesha katika siasa za Tanzania. Nitaeleza baadaye maana ya dhana hii.
Wanasiasa wa aina ya Zitto Kabwe ni waathirika wa mfumo uchwara wa uliberali ambao tumeamua kuufuata kimya kimya bila hata kuuelewa vizuri.
Aidha, hamaki na upinzani dhidi ya kutangaza kugombea urais inadhihirisha jinsi ambavyo wengi wetu hatujaielewa vizuri dhana ya uongozi katika mfumo tulio nao wa uliberali uchwara. Tunataka tutende kijamaa wakati tunaishi kiliberali. Katika mfumo wa ujamaa tuliojaribu kuujenga baada ya uhuru, suala la uongozi lilikuwa si suala la mtu binafsi.
Uongozi ulikuwa ni jukumu la wanataasisi kuamua nani anafaa katika nafasi gani. Hivi ndivyo Rashidi Kawawa alivyoweza kuacha cheo cha uwaziri mkuu kwa kumpisha Edward Moringe Sokoine na yeye kuchukua nafasi ya Waziri wa Ulinzi.
Hii ni kwa sababu enzi hizo waliokuwa wanaamua nani ashike nafasi gani ni chama na si mtu kujichagulia nafasi ya uongozi. Katika enzi za ujamaa wetu wa kitanzania, kiongozi mwenye cheo kikubwa na kidogo wote walikuwa ni viongozi wanaoheshimika na kuheshimiana; na ndio maana wote waliitwa ‘ndugu’, sawa na wananchi wenzao ambao hawakuwa viongozi.
Utaratibu huu tumeuua baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi na kuamua kuufuata mfumo wa kiliberali bila kuuelewa sawa sawa misingi yake. Katika mfumo wa kiliberali uchwara inaelekea haikubaliki kwa mtu aliyewahi kuwa waziri mkuu arudi kuwa waziri wa kawaida. Katika mfumo wa kiliberali, ngazi moja ya uongozi huzalisha ngazi nyingine ya juu zaidi, na ukishaenda huko hurudi chini bali unahakikisha unaendelea kwenda juu zaidi. Kwa hiyo, ukizingatia mantinki hii ya uliberali uchwara, huwezi kumshangaa Zitto kwa kuutaka urais na kusema kwamba yeye sasa ubunge basi; anataka kwenda juu zaidi na pengine ubunge sio saizi yake!
Kwa hiyo, Zitto Kabwe ameonyesha unafsi ambao ni tabia ya kawaida katika uliberali, hususani huu uliberali uchwara tunaofuata sisi. Mfumo huu una tabia ya kuzalisha viongozi wenye matamanio na utashi binafsi. Katika mfumo huu uongozi ni biashara. Ili uwe kiongozi katika mfumo wa kiliberali lazima uonyesha matamanio na utashi, na ujiuze vya kutosha kabisa. Kwa hiyo kutangaza nia na kujimwagia sifa juu ya uwezo ulio nao katika nafasi fulani ni sehemu kabisa ya mfumo wa kutafuta uongozi katika mfumo wa kiliberali.
Uongozi katika mfumo wa kiliberali ni juu ya mtu na wala sio juu ya taasisi. Anayepata uongozi katika mfumo huu ni yule mwenye uwezo wa kutengeneza mtandao wa wafuasi ambao atahakikisha anakuwa nao kwa kipindi chote hadi uchaguzi utakapofanyika.
Mkakati mwafaka wa kutafuta uongozi katika mfumo wa kiliberali unaambiwa ni kufanya maandalizi mapema. Huu ndio utamaduni ambao CCM imeuasisi kuanzia mwaka 1995 na ambao mtu alitarajia CHADEMA wangeukwepa.
Hata hivyo, sioni kwamba kitendo cha Zitto Kabwe kutangaza kuutaka urais kama ni kosa kwa sababu CHADEMA haijaweka rasmi utaratibu wa kuukataa utamaduni huu. Kwa kuwa utamaduni huu haujakataliwa rasmi kimfumo, haiwezi ikawa kosa mtu moja moja kuchagua kuutumia. Ndio maana Mzee Mtei kawataja watu wengine kadhaa, akiwamo yeye, kwamba nao wanaoutaka urais lakini hawajatangaza nia bado kwa hoja eti muda wa kufanya hivyo bado, kama vile ndani ya CHADEMA kuna muda rasmi uliowekwa wa kutangaza nia ya kugombea.
Ni wazi basi kwamba hata wale wanaompinga na kumzomea Zitto Kabwe kuutaka urais wanaonyesha unafsi. Hawafanyi vile kwa sababu wana misingi fulani wanayoiamini juu ya namna ya kupata uongozi, la hasha. Hawa wanafanya hivyo kwa sababu ya aina ya pili ya unafsi, ambayo ni fitina.
Hawa wanajaribu kuonyesha kwamba Zitto Kabwe kafanya kosa kubwa kutangaza kugombea urais, lakini hawasemi ni kosa gani na amevunja kanuni gani ndani ya chama. Wengine wameenda mbali zaidi na kumuona Zitto kama ni msaliti ambaye amenunuliwa ili kukidhoofisha CHADEMA.
Hii ni fitina na ni aina mbaya kabisa ya unafsi na tabia inayojitokeza vile vile katika uliberali uchwara. Nina wasiwasi kwamba watu wanaompinga Zitto kwamba nao labda wana watu wanaodhani wanafaa kuwa marais na wanajaribu kumchonganisha Zitto na jamii, ili hatimaye njia yao ya kuusaka urais iwe nyeupe huko mbele.
Katika mfumo wa kidemokrasia za kiliberali kutangaza kugombea urais hakupaswi kuleta mzozo wala vurugu katika chama. Wakati mwingine kitendo cha Zitto ni jibu kwa wapinzani wa CHADEMA aina ya Samuel Sitta wanaojaribu kujenga taswira ya hovyo kwamba ndani ya CHADEMA hakuna wenye uwezo wa urais zaidi ya Dk. Slaa aliyegombea kwa mafanikio mwaka 2010.
Kwa hiyo, wakati huu ambapo CHADEMA haina mwongozo elekezi juu ya namna ya ‘kuutaka’ urais, kutangaza kuutaka urais mapema ndio demokrasia yenyewe . Kwa hiyo tunapaswa kuwatia moyo wanachama wengine wenye matamanio ya urais watangaze wakati wowote na mahala popote wanapojisikia, wakati tukiweka misingi murua ya namna ya kupata mgombea mwafaka kwa wakati husika kutoka kwenye kundi la hao wanaojitangaza au wengine.
Kwa hiyo, wosia wangu wa leo ni kwamba kutangaza kugombea urais mapema hakupaswi kuleta mzozo au vurugu katika chama cha kidemokrasia kama CHADEMA. Ndiyo kusema hakuna sababu ya kupachika watu majina ya kifitina wanaotangaza kuutaka urais sasa na baadaye.
Muhimu ni kuweka mfumo utakaohakikisha kwamba CHADEMA hakizidiwi na nguvu za mfumo wa uliberali uchwara ambao umetamalaki nchini, ili hatimaye chama ndicho kiamue nani anakuwa mgombea.
 
Back
Top Bottom