Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Hapo kuna kiini macho, hata nisingejua kusoma picha ningeitambua. Zile pilika zake zote za mabilion ya uswis na alisema data anazo, leo hii ghafla eti kasain had afidavt kua hana jina hata moja! Hembu hilo fumbo wawafumbie wengne, welevu tushaling'amua. Sasa kumbe alikua anataka umaarufu gani mpya kupitia mabilion ya uswis, wakati hata jina moja hana. Lol!
 
"zitto is a great man" haiwezekani mtu mdogo atawale habari za mitandao ya kijamii kila kukicha kama mtu huyo siyo tishio.
 
Watanzania ni nani alikuwa anajua kuwa Kunafedha zimefichwa nje ya nchi kabla ya Zitto kuibua swala hili?
Mnataka kusema leo hii Watanzania mnataka kusema hakuna fedha zilizofichwa uswisi?HAPANA HAPANA HAPANA kabla haujamhukumu zitto soma hapa>>"According to data from the Swiss central bank, the amount of money that the Tanzanians held in savings and

deposit accounts in Swiss banks grew to $5.41 billion in 2012, up from $3.6 billion the prior year, although the annual amounts have varied considerably over the past decade" Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters.Kwa maana hiyo ni kweli kunafedha zimefichwa nje ya nchi,Fedha za watanzania,fedha za walipa kodi,fedha za walala hoi,fedha za miradi ya maendeleo ndani ya nchi yetu zimefichwa na mafisadi nje ya nchi.
Nimeshitushwa sana na namna Jaji werema alivyoongoza serikali kumgeukia zitto kibao eti hana majina ya watu walioficha fedha nje ya nchi,Kwa maana hiyo anataka kusema hakuna fedha zilizofichwa nje ya nchi?Mbona hajakili kuwa ni kweli kunafedha zimefichwa nje ya nchi lakini walioficha fedha hizo hatujapata majina yao.
Kimsingi itakuwa ni aibu sana serikali kukosa Plan B ya kupata majina ya watu walioficha fedha nje ya nchi,Kama zitto hana majina,Je serikali majina yako wapi?KAMA SERIKALI HAINA maana yake siku zote hizi serikali na Tume iliyoundwa ilikuwa inakula sitting allowance bila kuwa na plan B yao ya kupata majina ya walioficha fedha nje ya nchi?
Zitto ameonesha njia,ZItto ni Musa aliyeamua kuwatoa wana wa israel Misri(kutoa watanzania kwenye lindi la ufisadi na kuanika mafisadi)sasa kosa lake liko wapi?
Naiona fedheha kwa viongozi wa serikali yetu kuamua kupambana na zitto na kaucha kupambana na watu walioficha fedha nje ya nchi.Kwangu mimi zitto ni Mfalme na mshindi katika hili,Serikali play ur role kwenye hili tuachane na kumchafua yule aliyefichua ukweli huu kuwa fedha zimefichwa nje.
Kwa mwenendo huu nachelea kusema Walioficha fedha uswis wameshawateka ama kuwazidi kete waliochaguliwa kufuatilia fedha hizo,Hivyo basi fedha haramu hizo za uswisi zimetumia kuwakaba,kuwateka na kuwashibisha wanatume na sasa wameamua kugeuza kibao kusema ZItto hana majina hivyo wanatengeneza mazingira ya kutupoteza watanzania katika hili.
Haya Zitto hana majina,Serikali majina yapo wapi>?

Alafu unaonekana una Akili fupi sana kama wewe huwa usomi basi ni wewe, Mimi nimejua hata Kabla hata zitto ajamwaka porojo zake kwenu. Nilipost kwenye Fb wall yangu kabla hata zitto ajapost kwenye tweeter by the way wa kwanza kuleta haya bungeni ni Zitto au wakina Kangi lugora?

Wacha kupotosha.
 
upuuzi mwingine....nitaje nisitaje?
Kama majina anayo kwa nini asiweke hadharani?Dr Slaa alitoa list of shame pale mwembe yanga bila hizi mbwembwe za tisha toto!
 
Hivi kuna mdudu gani kaingia JF? Inashangaza, inasikitisha na inaudhi...watu wanaamka tu wanaposti yale waliyokuwa wakiyaota usingizini. Something is amiss somewhere!
 
Watanzania ni nani alikuwa anajua kuwa Kunafedha zimefichwa nje ya nchi kabla ya Zitto kuibua swala hili?
Mnataka kusema leo hii Watanzania mnataka kusema hakuna fedha zilizofichwa uswisi?HAPANA HAPANA HAPANA kabla haujamhukumu zitto soma hapa>>"According to data from the Swiss central bank, the amount of money that the Tanzanians held in savings and

deposit accounts in Swiss banks grew to $5.41 billion in 2012, up from $3.6 billion the prior year, although the annual amounts have varied considerably over the past decade" Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters.Kwa maana hiyo ni kweli kunafedha zimefichwa nje ya nchi,Fedha za watanzania,fedha za walipa kodi,fedha za walala hoi,fedha za miradi ya maendeleo ndani ya nchi yetu zimefichwa na mafisadi nje ya nchi.
Nimeshitushwa sana na namna Jaji werema alivyoongoza serikali kumgeukia zitto kibao eti hana majina ya watu walioficha fedha nje ya nchi,Kwa maana hiyo anataka kusema hakuna fedha zilizofichwa nje ya nchi?Mbona hajakili kuwa ni kweli kunafedha zimefichwa nje ya nchi lakini walioficha fedha hizo hatujapata majina yao.
Kimsingi itakuwa ni aibu sana serikali kukosa Plan B ya kupata majina ya watu walioficha fedha nje ya nchi,Kama zitto hana majina,Je serikali majina yako wapi?KAMA SERIKALI HAINA maana yake siku zote hizi serikali na Tume iliyoundwa ilikuwa inakula sitting allowance bila kuwa na plan B yao ya kupata majina ya walioficha fedha nje ya nchi?
Zitto ameonesha njia,ZItto ni Musa aliyeamua kuwatoa wana wa israel Misri(kutoa watanzania kwenye lindi la ufisadi na kuanika mafisadi)sasa kosa lake liko wapi?
Naiona fedheha kwa viongozi wa serikali yetu kuamua kupambana na zitto na kaucha kupambana na watu walioficha fedha nje ya nchi.Kwangu mimi zitto ni Mfalme na mshindi katika hili,Serikali play ur role kwenye hili tuachane na kumchafua yule aliyefichua ukweli huu kuwa fedha zimefichwa nje.
Kwa mwenendo huu nachelea kusema Walioficha fedha uswis wameshawateka ama kuwazidi kete waliochaguliwa kufuatilia fedha hizo,Hivyo basi fedha haramu hizo za uswisi zimetumia kuwakaba,kuwateka na kuwashibisha wanatume na sasa wameamua kugeuza kibao kusema ZItto hana majina hivyo wanatengeneza mazingira ya kutupoteza watanzania katika hili.
Haya Zitto hana majina,Serikali majina yapo wapi>?

“Foolishness is more than being stupid, that deadly combination of arrogance and ignorance.” (Paul David Tripp)
 
Huyu dogo njaa zinampeleka pabaya sana. Zito ni mnafiki sana na ni msaliti bora ya YUDA. Ccm wanamtumia sana.
 
Kumbe kila kitu hasemi ukweli.Hatendi ukweli. Kazi ni kujichora tu kuwa yu sahihi muda wote;mpambanaji;mfuata Kanuni;anayefuatwafuatwa;anayesemwa vibaya;anayenyanyaswa na kadhalika. Kumbe, wapi! Leo Tanzania imeambiwa 'ukweli'. Ukweli kuwa Zitto anafanya maigizo tu kuhusu mabilioni ya Uswisi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mnadhimu wa Serikali Bungeni, Jaji Fredrick Mwita Werema na William Lukuvi,kama nilivyowataja, 'wamemuanika' Zitto.

Wakichangia kwa kufuatana, Werema na Lukuvi wamesema kuwa Zitto hana hata jina moja la walioficha mabilioni Uswisi-hoja anayoishupalia Zitto kila uchao. Wakasema kuwa Zitto, kwa kiapo (Affidavit) ametamka na kuthibitisha kuwa hana hata jina moja la mficha-mabilioni Uswisi. Mimi siamini!

Kumbe Zitto ni mtu wa utani hivi kwa watanzania!?? Hoja amewasilisha Bungeni;amekutana na viongozi mbalimbali wa kidunia kuhusu suala hili;amesafiri kwenda Ujerumani mara kadhaa kwa suala hili na kadhalika. Kweli atubabaishe wakati wote huo? Siamini.

Kama Zitto amechokozwa leo (na tena amedhalilishwa), umefika muda wake kujibu mapigo. Kutaja majina ya waficha-mabilioni Uswisi. Hana haja ya kumpa Godbless Lema. Ataje mwenyewe. Muda ni huu.Akishindwa, tutamuona muongo sana. Atakuwa hafai (na kutamka kimatendo kuwa hautaki) Urais wa nchi hii wala Uenyekiti wa chama chake cha CHADEMA.

CCM 'tumembeep', kama anaweza atupigie!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Chezea Zito wewe... Kumbuka zito alianzisha huo Mchongo ili apate Ganji cha juu toka kwa Waficha pesa sasa ameshavuna chake mapema huku na yeye wamemfundisha pa kuzificha hizo Ganji walizompatia . Sasa ananijidai Hana Majina ! Haingii akilini jaribuni kutafakari vizuri
 
Yani Huyu zzk ni msanii mzuri wa comed kwa nn asianzishe kikundi chake akashindana na kina masanja yani sikuamini masikio yangu kumbe aliisha apa kwamba hawajui walioficha pesa nje inamaana alikuwa anatugombanisha na serikali yetu huyu mtu hatufai hata kidogo watu kama hawa ni wakuogopa Kama ukoma
 
Zitto akitaka asalimike, ataje,ayaweke majina hadharani. Na kama chadema itaendelea kumfuga basi tutathibitisha kuwa ni chama cha kilaghai.

Mhhhh kwanini usiseme Bunge likiendelea kumfuga? we si ndiyo ulikuwa unasema CDM wanamuonea leo imekuaje?
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili.

Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015.

Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA).

"Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka nazo, nitatafuta chuo nikafundishe na kama nitakosa ni bora nikalime michikichi... sihitaji urais," alisema.

Katika mkutano wa wanafunzi hao, walisema Bw. Makamba ana sifa zote za kuwa rais wa nchi kamaatagombea nafasi hiyo mwaka 2015 ili aweze kulikomboa Taifa ambalo hivi sasa linakabiliwa na matukio mengi ya uvunjifu wa amani.

Wanafunzi hao walikwenda mbali zaidi na kuyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni pamoja na vurugu, kutekwa kwa watu wasio na hatia, kufanyiwa vitendo vya ukatili, kumwagiwa tindikali na kupungua kwa mtangamano wa kijamii.

Mwenyekiti wa mkutano huo ambao ulifanyika mkoani Morogoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Mbeya, Bw. Theonest Theophil, alisema Bw. Makamba alipata kura 72 ambapo Bw. Kabwe alipata kura 20.

Bw. Theophil alisema sifa za kiongozi wanayemtaka kwanza awe kijana mwenye fikra mpya, atakayeleta matumaini mapya, kuwaunganisha Watanzania, asiyeendekeza siasa za kikanda, mdini na mkabila.

Sifa nyingine ni kiongozi mwadilifu asiye na rekodi ya kutuhumiwa mahali popote kwa vitendo viovu, mtulivu, mwenye busara na anayepima kauli zake.

Source: Majira

ACT watamuweka nani agombee udiwani kule MWANDIGA, Ubunge kule Kigoma kaskazini na Urais? Yona? Mwigamba? Mkumbo? Mchange? Njano?
 
Back
Top Bottom