Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Hao wanzanzibar acheni waende tu kelele zimezidi

Mnawachukia Wazanzibar kwakuwa hawaipi kura CDM! Safari hii mkienda kwenye kampeni mtakutana na tindikari, mmeshaona wakifungungwa wahusika? Mvae mask.

Body without head
 
Kumbe kila kitu hasemi ukweli.Hatendi ukweli. Kazi ni kujichora tu kuwa yu sahihi muda wote;mpambanaji;mfuata Kanuni;anayefuatwafuatwa;anayesemwa vibaya;anayenyanyaswa na kadhalika. Kumbe, wapi! Leo Tanzania imeambiwa 'ukweli'. Ukweli kuwa Zitto anafanya maigizo tu kuhusu mabilioni ya Uswisi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mnadhimu wa Serikali Bungeni, Jaji Fredrick Mwita Werema na William Lukuvi,kama nilivyowataja, 'wamemuanika' Zitto.

Wakichangia kwa kufuatana, Werema na Lukuvi wamesema kuwa Zitto hana hata jina moja la walioficha mabilioni Uswisi-hoja anayoishupalia Zitto kila uchao. Wakasema kuwa Zitto, kwa kiapo (Affidavit) ametamka na kuthibitisha kuwa hana hata jina moja la mficha-mabilioni Uswisi. Mimi siamini!

Kumbe Zitto ni mtu wa utani hivi kwa watanzania!?? Hoja amewasilisha Bungeni;amekutana na viongozi mbalimbali wa kidunia kuhusu suala hili;amesafiri kwenda Ujerumani mara kadhaa kwa suala hili na kadhalika. Kweli atubabaishe wakati wote huo? Siamini.

Kama Zitto amechokozwa leo (na tena amedhalilishwa), umefika muda wake kujibu mapigo. Kutaja majina ya waficha-mabilioni Uswisi. Hana haja ya kumpa Godbless Lema. Ataje mwenyewe. Muda ni huu.Akishindwa, tutamuona muongo sana. Atakuwa hafai (na kutamka kimatendo kuwa hautaki) Urais wa nchi hii wala Uenyekiti wa chama chake cha CHADEMA.

CCM 'tumembeep', kama anaweza atupigie!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

 
Aaaah....
mzee Tupatupa kumbe bado mlikuwa hamjastuka siyo? wenzenu CHADEMA loooooong time wamestuka kwama jamaa hana lolote, ni mpenda sifa tu...

yuko tayari kudanganya watanzania, kudanganya bunge, kutumia pesa za umma kwenda sijui uswizi kumbe anachezea watanzania shere.

sasa mme-mbipu subirini atawapigia; bila shaka taratibu ziko njiani anakwenda kuandaa press conference pale serena. Sijui na ktk hili atahitaji msaada wa mwanasheria, sina uhakika. Nadhani atawapigia...
 
duuuh wanasiasa uchwara sijui njaa ni shida sana. Huyu anastahili kabisa kabisa kushitakiwa kwa kudhalilisha bunge na kuongoea watanzania.

tunahitaji kuona hicho kiapo alichosaini zitto according to werema na pia tunahitaji kuona 'majina na akaunti' kutoka kwa zitto. Tofauti ya hapa ni majanga tu
 
c alisema serikal ikichelewa kuyataja ye atafanya hivyo? sasa majina yako wapi!..ngoja 2subiri kauli yake.
 
Zitto ni mtu wa hovyo sana....CHADEMA fukuzeni huyu mtu...anahadaa Watanzania na anatuaminisha uwongo...
 
Zitto akitaka asalimike, ataje,ayaweke majina hadharani. Na kama chadema itaendelea kumfuga basi tutathibitisha kuwa ni chama cha kilaghai.
 
VUTA-NKUVUTE Zitto alishtukiwa siku nyingi na watanzania.hata kwenye daladala wanamsema vibaya sana huyu mtu.nawashangaa wahariri wanavyomwandika kwenye kurasa za mbele za magazeti yao kila uchao.hii inaonyesha ni kwa kiasi gani uandishi wa habari ulivyo chini hapa tanzania.uandishi kabila hii ni janga kwa hakika.
 
Last edited by a moderator:
Zitto akitaka asalimike, ataje,ayaweke majina hadharani. Na kama chadema itaendelea kumfuga basi tutathibitisha kuwa ni chama cha kilaghai.

Mbona akili yako wewe gamba imedumaa? chama chakavu na watu chakavu kweli! unataka ataje wakati Werema amesema mpaka aliwekwa chini ya kiapo akasema hana hayo majina. Sasa wewe huelewi nini! Huyu bwana yenu magamba mchukueni huku kwetu hatuhitaji scraper. Chukueni hilo zigo lenu maana mnalipenda na ndio sera yenu kudanganya
 
Zitto akitaka asalimike, ataje,ayaweke majina hadharani. Na kama chadema itaendelea kumfuga basi tutathibitisha kuwa ni chama cha kilaghai.

Uwiiiiii Zito kabaki mwenyewe. Nimeamini Watanzania hawampendi mtu wanapenda mtu mkweli na mudilifu. Nawapongeza sana
 
Back
Top Bottom