mwambieni kwanza atueleze amepataje utajiri wote huo alionao? pengine ndiyo maana hataki posho maana ameishashiba
Nasikia kulengwalengwa na machozi....... watoto wetu mtarithi nini kwa spidi hii ya mama-MyarukoloNeema Kishebuka, Dsm
Kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) iumewataka wabunge wa chama hicho kurudisha pesa zilizowekwa katika account za wabunge kwa ajili ya kuhamasisha zoezi la kuhesabu watu linalotarajiwa kufanyika nchini kote Agost 25 mwaka huu.
Kamati hiyo iliyokutana jijini hapa imetoa maagizo hayo na kuwataka wabunge wake kuzirudisha fedha hizo kwa katibu wabunge wake baada ya kuzipitia akount zao na kubaini kuwepo kwa pesa hizo kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila mbunge zilizowekwa katika akaunti zao.
Kamati hiyo imesema kuwa si halali wabunge hao kupokea pesa hizo kwa kuwa ni wajibu wao kuhamasisha zooezi la sensa katika maeneo hayo.
Imeelezwa kuwa ni wajibu wa wabunge kushughulikia masuala ya kiserikali kama ya sensa ya watu na makazi hivyo kupokea pesa Hizo ni sawa na rushwa kwani ni wajibu wao.
Hata hivyo wabunge hao wamekanusha kupata taarifa ya kuingiziwa pesa Hizo na ofisi ya Bunge na kuahidi kuzinagalia akaunti hizo na endapo watakuta pesa zimeingizwa watazirudisha kama kamati kuu ilivyoagiza.
Kwa upande wake naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, aliwaasa wabunge wa CHADEMA kuwa makini na pesa zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa masuala ambayo tayari ni wajibu wa wabunge wa Bunge hilo lililo chini ya Ana Makinda.
"Hii ni rushwa ya wazi ndugu zangu, mimi nimeambuwa na katibu wa Bunge kuwa amewaingizia milioni moja kila mbunge sasa ni wajibu wetu kurudisha pesa hizo kwakuwa ni wajibu wetu kufanya kazi za kijamii'' alisema Zitto.
Nadhani ni 350+ (nimechukua %20 ya kura 70x5 zilizotakiwa kumuondosha WM), hii ni kusema zaidi ya Shs. 350, 000,000. Tunaelekea wapi. Hawa wamekaa kama watoto wadogo, wakikatazwa mavi wanachezea mkojo.kazi ipo!
wabunge sijui miatatu na ngapi mara milioni moja!! vijichenji ambavyo vingeliweza alau kutosha kujenga kijizahanati na kijishule cha chekechea watoto wetu wakapata chanjo za polio na kuchangamsha akili zinatapanywa!
ama kweli kufa kwa mdomo mate kutawanyika!
nchi imeoza imebakiza kunuka tu