Zitto kweli ni wakati muafaka kutangaza hili?

Status
Not open for further replies.
Habari wana Jf!
Kwa habari za kutoka kwa chanzo cha habar ndani ya CHADEMA huko arumeru ni kwamba mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Joshua Nassary amesema kwamba amesikitishwa sana na kauli ya zitto kutangaza nia ya kugombea urais kwan kauli hiyo haijaja muda muafaka na inachochea makundi ndani ya chama pia na kuvunja nguvu ya wapiganaji huko arumeru. Pia ijapokuwa ni haki yake kikatiba lakini haikuwa ni muda muafaka kwa sasa.
My take
zitto pamojaa na vijana wako wakina benard sanane acheni hila na chuki zenu kwani mnazidi kujiondolea imani kwenye chama, pia jueni kwamba 'this time tommorow' msilete upinzani ndani ya upinzani. kwani david kafulila aliwahi kusema kwamba" UONGOZI BILA DEMOKRASIA NI UDIKTETA LAKINI DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO"

Hata hivyo Zitto mwenyewe
amekanusha kuhusika na
waraka huo na amesema
mchezo huo ni mchezo wa
siasa chafu kupitia makaratasi. Alisema chama hicho kiko
imara na viongozi wote wako
bega kwa bega kuhakikisha
kuwa Nasari anashinda
ubunge wa jimbo hilo. Alisema kinachojaribu
kuenezwa ni uongo wa
kipuuzi unaopaswa
kudharauliwa na kila mwenye
akili timamu, na hakuna
kiongozi makini wa CHADEMA anayeweza kuwaza na
kuandika upuuzi huo. “Huo ni upuuzi, wapiganaji
wako mstari wa mbele;
hatuwezi kuanza kuwavuruga
hata kidogo, wala
kuwakatisha tamaa…hapa ni
kuungana tu, tena tunapenda CCM ijue kuwa tumeungana
kwa dhati na tuko pamoja
kuhakikisha mgombea wetu
anashinda jimboni. Hatuwezi
kusumbuliwa na mchezo
mchafu, tunatumaini wananchi watatuchagua kwa
hoja zetu na sera. “Hizo ni dalili za mfa maji…
CCM sasa wanatapatapa sana,
tunajua mpaka sasa hali yao ni
mbaya sana, hawatafanikiwa
kwa siasa chafu hizo,
tumeungana kikwelikweli; kwanza hizo wanazosambaza
si hoja ambazo watu wa
Arumeru Mashariki wanataka
kujua au kusikia. Kwa watu
wa Arumeru Mashariki hoja za
msingi ni juu ya maji yao, afya yao, elimu yao, ajira kwa
vijana na hizo ndizo CHADEMA
tunazungumzia si kufanya
propaganda,” alisema Zitto.

Chanzo:TANZANIA DAIMA LA JANA.
 
Zitto, kama kweli Umepima, umetafakari, au umeshauriana na wadau wako wa karibu au umejishauri mwenyewe kuwa unaweza kuwa Rais. Naomba urudi hapa kwenye JF Utangaze kuwa una nia ya kugombea urais, ili sisi tunaokujua kwa niaba ya watanzania wasiokujua, tuseme unafaa au haufai. Tafakari tena, pengine ulitoa uamuzi wa haraka. Ukishaamua, naomba urudi humu jamvini, uwaambie watanzania kuwa "NATAKA KUGOMBEA URAIS 2015". Pengine umri sio kigezo cha muhimu sana, kuna vingine vya maana zaidi.
 
Je, karani wa benki kuu kutaka kuwa Gavana wa benki kuu ni makosa?
Kwanini ulazimishe watu wawe na shallow ambitions?
Nyerere huyo huyo alisema kama unataka urais, wajulishe watu mapema ili wakuchambue vizuri, usijifiche.

Soma post uielewe, it is not a matter of shallow ambition, only the timing. Sisemi awe na ambitions za kuwa mkuu wa wilaya, Mkuu wa mkoa etc, only the timing!!! Muda bado!!!
 
Umetumwa wewe gamba mkubwa wa CCM usiyekuwa na mbele wala nyuma,unatumia makamasi kufikiri badala ya ubongo,akili umefungia kabatini.Hamuwezi hata siku moja kuivuruga Chadema mana inawanyima usingizi.

my frend pelege, mimi sio gamba kama unavyodhani wewe but mi ni mpiganaji na mwanchadema halisi, hii habari ni ya ukeli kabisa na kama huamini ngoja wakina molemo walete uthibitisho wa hii habari.
 
Habari wana Jf! Kwa habari za kutoka kwa chanzo cha habar ndani ya CHADEMA huko arumeru ni kwamba mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Joshua Nassary amesema kwamba amesikitishwa sana na kauli ya zitto kutangaza nia ya kugombea urais kwan kauli hiyo haijaja muda muafaka na inachochea makundi ndani ya chama pia na kuvunja nguvu ya wapiganaji huko arumeru. Pia ijapokuwa ni haki yake kikatiba lakini haikuwa ni muda muafaka kwa sasa.My take zitto pamojaa na vijana wako wakina benard sanane acheni hila na chuki zenu kwani mnazidi kujiondolea imani kwenye chama, pia jueni kwamba 'this time tommorow' msilete upinzani ndani ya upinzani. kwani david kafulila aliwahi kusema kwamba" UONGOZI BILA DEMOKRASIA NI UDIKTETA LAKINI DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO"
Unaweza kuthibitisha hila na chuki zangu? Wewe taarifa za ndani za CHADEMA umezipataje? Usilete majungu hapa,kama ni taarifa za ndani unazileta za nini huku hadharani? unajificha nyuma ya Fake ID halafu unataka kupotosha watu hapa
 
Kwani Dr akimpisha Zito na akampa suport si inawezekana? Ni mipango tu, nia ya kwanza ni magamba waondoke magogoni.

Pamoja na kwamba ametangaza kuweka nia ya kugombea uraisi 2015, nadhani kwa sasa hii sio big issue kwetu wanachadema.

Kwanza katiba ya sasa ya JMT haimpi uwezo wa kugombea nafasi hiyo.

Pili, kwakuwa nia yake ni kuingia ikulu kwa tiketi ya chadema, atalazimika kufuata utaratibu na katiba ya chadema ili kupata ridhaa hiyo, kitu ambacho hata yeye amekitambua katika waraka wake.

Tatu, kwakuwa bado tuna miaka mitatu hadi kufikia uchaguzi ujao, kujikita kumzungumzia sasahivi, kama ana nia mbaya na chama ni sawa na wavuvi kuanza kugombea samaki ambaye hawajamvua!
 
Nimesikitishwa saana na habari zilizo enea na kutangazwa na vyombo vya habari siku ya leo kuwa naibu katibu mkuu ana mpango wa kugombe urais, siyo kwamba nimesikitishwa na nia yake! Bali timing yake, hivi ni kweli mheshimiwa ameona huu ndio wakati muafaka kutangaza nia au kuna ajenda nyingine? Kwa kweli I was so furious with the breaking news, kama ni kweli mheshimiwa Zitto umeona ni muda muafaka nitakuwa na wasiwasi na weredi wako! Kila jambo lina majira yake mheshimiwa Zitto!

Sio kuwa hustahiri ila muda huu concentration nadhani imekuwa ni uchaguzi wa Arumeru, imekuwaje wewe ukaona tena ndio muda wako muafaka kwa ajiri ya kutangaza nia yako ya kugombea urais! Au kuna ajenda nyingine? Manaake the attention will definitely be drifted from Arumeru mpaka hoja yako, what is that?huelewi kuwa results zake zitakuwa mbaya?

Kwa kweli nimeanza kuwa na wasiwasi na baadhi ya viongozi kwenye vyama vya upinzani, nilifikiri lengo la vyama ni kuwa na sera mbadara za kumkomboa mtanzania, kumbe naanza kuwa na mashaka, lakini hata kama umewekwa pandikizi, I think you need to be a very introspective pandikizi and muono wako usiwe wa kiafrica I mean thinking of only tomorrow, but uwe unaenda mbali zaidi think of atleast 20 yrs ahead, I can assure you the day will come the rotten System will have to go! Don’t be among the leaders who will have to go with the rotten system.

Sory kwa kuandika ujumbe mzito namna hii , ila kwa kweli nimesikitika na kwa kuwa mimi ni mpenzi wa mageuzi without a party,but, you have made me doubt your party if you really have good intentions with our mourning nation.

Nawasilisha

Huyu ni traitor, you wait and see. One day we will retrieve this thread and refresh our memories on Kabwe's traitor-hood
 
CDM CDM, Hayo maneno angesema Baba Junior tusingesikia habari za timing...Af mbona sijaona athari yeyote toka atamke zaidi ya haters wake kumpigia kelele humu JF. Ina maana hata 2015 huyo mgombea atahitaji msaada wa akina Slaa kumpigia kampeni?
 
Timing sio nzuri, ila ni wazi zitto anataka kuwa rais kama mtz mwingine yoyote kwny siasa, haiwezi kuvunja chama
 
Huyu kasoma thread yangu arafu anaichakachua! Hebu kuwa msataarabu weee!

Wewe ulikuwa umesemaje kuhusu hili? Mimi nawashangaa hata wanaopiga kelele na kutokwa na mapovu ktk hii habari ya Zitto. Kutangaza nia ni haki yake bwana, lakini hawezi kwenda 1 kwa 1 lazima apite kwenye chujio sasa shida iko wapi? Mtu mwenyewe hajafika umri wa kuwa Rais kwa mujibu wa katiba na CDM tutakqwa wajinga namba moja au wa mwisho kama tutapeleka mtu wa miaka 30 na kadhaa. Pingamizi litatuh
 
Hiz bio za akina zitto si nzuri wa wapenda chama chetu. Watu wachape kazi kwanz rais atajitokeza baade kutegemeana na yule anayefaa kukabidiwa dhamana ya chama kuiongoza nchi. Si kwa style ya kila moja kusema mm nautaka urais.
 
Zitto, kama kweli Umepima, umetafakari, au umeshauriana na wadau wako wa karibu au umejishauri mwenyewe kuwa unaweza kuwa Rais. Naomba urudi hapa kwenye JF Utangaze kuwa una nia ya kugombea urais, ili sisi tunaokujua kwa niaba ya watanzania wasiokujua, tuseme unafaa au haufai. Tafakari tena, pengine ulitoa uamuzi wa haraka. Ukishaamua, naomba urudi humu jamvini, uwaambie watanzania kuwa "NATAKA KUGOMBEA URAIS 2015". Pengine umri sio kigezo cha muhimu sana, kuna vingine vya maana zaidi.

Zito ni mtoto anapotezwa na ushabiki wa wahuni wenzake mitaani. Anasikia makelele ya wahuni wenzake mitaani ndio kipimo chake kuwa anaweza kukabidhiwa nchi hii, Anaona anaweza kuwa Rais kwa ushabiki wa mitaani. Vijana wangapi wanajiandikisha kupiga kura na hata kama wamejiandikisha ni wangapi. Anataka kivuruga CDM. Masaliti, tutakuja kumbushana humu JF haya tunayoyasema leo, ataiua CDM. Migogoro mingi ya chama inaanzia na watu wa hivi!!! Simwamini tena,
 
my frend pelege, mimi sio gamba kama unavyodhani wewe but mi ni mpiganaji na mwanchadema halisi, hii habari ni ya ukeli kabisa na kama huamini ngoja wakina molemo walete uthibitisho wa hii habari.

Nimekupata sana Sharcole, magamba wao uwongo ni ukweli na ukweli ni uongo! Kama kweli wewe ni CHADEMA tafadhali tuonyeshe kadi yako ya uanachama wa CHADEMA PLEASE!
 
Neither Nassary nor Zitto are that stu**pid, hebu jiangalie wewe mtoa maada!
 
mwisho wa zito sio mzuri hata kidogo'hivi kama angekaa na kusubiri wakati muhafaka kungekuwa na tatizo??mbona hawa jamaa kutoka kigoma wana haraka sana au ndio ile damu kuchanganyika na warundi na wakongo'hii nchi mnaona kama haina mwenyewe'kwa taarifa yenu wenye nchi hii tupo na tumetuliia mtajionea mwisho wenu utakuwaje
 
Moyo wangu unaniuma kwa cdm ninavyo iamini na nimejitosa ila mbona tunazinguana? Ila akili nyingine inaniambia kwamba cdm kimekua chama kikubwa, hivyo kikawa 'complex'. Hii ni kawaida!
 
Zitto ni kigeugeu! Tukimpa nchi hii ataiuza, kwanza zitto ni mgonjwa wa kichwa na kila siku anaenda india, tukimpa nchi atatumia badget nzima kutibu kichwa chake.
 
Ni haki yake kutangaza nia! Nami nautaka Ubunge wa Kisesa! Nafikri Tumbo atanielewa! Hivi mjinga gani atakubali kupeleka mtu ambaye tunajua atawekewa pingamizi na kuondolewa kwenye mchuano? Hebu tusishushe hadhi ya Jf kiasi hicho! Shardcole anavyotulazimisha hadi anatia hasira! Gamba mkubwa huyu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom