Zitto kuwa m/kiti wa CHADEMA taifa?

Siku zitto akipewa uenyekiti wa Chadema, wa kwanza mie naihama CCM na nnahamia Chadema.

Lakini, nnavyojuwa Chadema wanarithishana kutoka Baba Mkwe mpaka Mkaziamwana.

umehama lini KAFU.... au ulikua una maana utahama CCM-B ..... haa haaaaaa
 
CRAP! kama vatar yako.............kweli peoples power

avatar39777_1.gif
kweli sikuichunguza. akili yake inalala kama anavolala kifikra.
 
Umefanikiwa utunzi ila tumekugundua umetumwa wewe,CDM si NCCR, TLP au CUF hainunuliki na ZITTO anajiko kwa JK na kwa MAFISADI kuganga njaa na hana uwezo wa kuiongoza CDM sanasana anatumiwa na wanaotaka urais 2015 lakini atashindwa vibaya.

mmaroroi,
Mjumbe hauawi, mimi nimetoa taarifa kama mwandishi wa habari. Jadili hoja si mleta hoja. Mimi hakuna mahali nimeonesha interesti yangu. Kwangu mimi hadi zitto atakapojibu yale yote yaliyoandikwa na mwanahalisi kuhusu ukaribu wake na usalama wa taifa ndipo nitakapomuunga mkono. Huu ndo msimamo wangu.
Si lazima habari niliyoilta mimi niwe nakubaliana nayo. Hapana. Hicho ndicho nilichoona ama kusikia na ndicho nilicholeta.
 
thread ya Uchonganishi, HAINA MASHIKO

Gagurito,
Siyo thread ya uchonganishi, ila ni thread ya usichotaka kusikia wewe. Hata mimi sicho ninachotaka kusika pia. Mficho ugonjwa kifo kitamfichua. Wewe na mimi tuko pamoja ila unanishambulia kwa kuwa tu nimeweka ukweli hadharani.
 
icon1.png
Re: Zitto kuwa mkiti wa chadema taifa?


Rafiki yako hakukueleza ukweli nilichosikia mimi ni kwamba Zitto anaandaliwa kuwa mufti wa waislamu Tanzania kutokana na kuwa na elimu ya kuridhisha, kwani huyu mufti wa sasa hivi akikaa kikao meza moja na maaskofu hawezi kuwa napointi ya kuongea kwa sababu ni darasa la saba, huo ndio mkakati uliopo kwa sasa kwani licha ya swala la umri wake kuwa mdogo, imethibitishwa kwamba hakuna umri maalum wa kuwa mufti, na kuhusu kitakuwaje awe mufti wakati zitto haswali sala tano, hoja hiyo ilipanguliwa kwamba kuna viongozi wengi tu wa Bakwata ambao ni wakristo na wengine ni masheikh lakini wanamiliki bar za kuuza pombe, na wengine wameoa wanawake wakristo lakini hawajafunga ndoa za kiislamu. nitaendelea kuwapa update hizi kwa kadili ninavyozipokea.​

uuwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, mkuu huku tusielekee maana tutaleta hadithi za Pwagu na Pwaguzi
 
:ballchain:

This guy is so controversial.....kumwamini unataka lakini upande mwingine wa kutokumwamini unakuzidia nguvu zaidi

Mikakati hii nina uhakika haitakisafisha CHADEMA bali kukichafua zaidi

Just to be honesty, sidhani kwa namna yoyote ile kama Zitto anaweza kuwa suluhu ya mageuzi ya kisiasa kwa kupitia CHADEMA...Amekwisha kuonje mvinyo na umeshamlewesha

Kama ni hoja ya vijana or whatever the case it might be , ni BORA MARA 300 kumpa yule jamaa Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya (jina limenitoka kidogo) kuliko huyu mtafuta sifa kwa gharama yoyote

 
Siku zitto akipewa uenyekiti wa Chadema, wa kwanza mie naihama CCM na nnahamia Chadema.

Lakini, nnavyojuwa Chadema wanarithishana kutoka Baba Mkwe mpaka Mkaziamwana.


Najua utahamia kwa sababu ana attributes ambazo CCM mnazitaka kwa mtu ili awe kiongozi wenu....kugawa watu, kusimamia maslahi ambayo unayabandika jina la umma hata kama umma hauoni maslahi kwenye unayosimimia na vijitabia vingine vya ajabu ajabu

Ila kama ukweli Zitto atavuta wanachama wa aina yako ndani ya CHADEMA, basi Zitto kuwa M/kiti ni sawa na mwisho wa uhai wa CHADEMA...........
 
Watu wengi hawajaelewa iledhana ya "Posho Mbili" ilikuwa na maana gani na inaweza kutumika vipi kumregulate mwanasiaisa aliyewahi kuchukua posho mbili. Wabunge wengi wa bunge liliopita hasa wale waliokuwa katika Kamati za Bunge hususan Kamati ya Nishati na Madini na Kamati ya Mashirika ya Umma aliyokuwa akitumikia Mhe Zitto walihusika katika kuchukua posho mbili.

Kama wajumbe wa Kamati za Bunge walikuwa wakilipwa posho na Ofisi ya Bunge kwa ajili ya kazi, malazi na kujikimu wawapo katika vikao vya kamati ya Bunge. Lakini pia walikuwa wakipokea posho kutoka katika mashirika mbali mbali kama vile Shirika la TANESCO ambalo walikuwa wakiyafanyia shughuli mbali mbali. Hivi karibuni ilitajwa kuwa posho kwa ajili ya Lunch inayotolewa na TANESCO ni Shilingi Milioni Moja kwa siku.

Dhana hii ya posho mbili nio ilifanya watu kama akina Mwakyembe na Kamati nzima ya Nishati na Madini kunywea mbele ya Serikali katika hoja ya Richmond na kuacha hoja hiyo ipite kimya kimya. Kwani kama wangeendelea kuipinga TAKUKURU ingetumika kuwafikisha mahakamani hivyo wasingepata fursa ya kugombea ubunge tena. Hata Mhe Zuberi Zitt inasemekana alihusika katika kupokea posho mbili. Hivyo ili asifikishwe mahakamani na kuharibiwa kwa political career yake mara kwa mara hupatiwa maelekezo ya nini anatakiwa kufanya ina a certain situation. Hivyo tusimtarajiw Mhe Zitto kuweza kutoka nje kususia hotuba ya Rais wa CCM, kushiriki maandamano yanayoendelea na kuendeshwa na CHADEMA n.k


hivyo Mhe Zitto sio candidate mzuri wa nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA kwa sababu ya kuwa na sifa za kifisadi ikiwemo kupokea posho mbili, kosa ambalo linaweza kumfikisha mahakamani siku yoyote. Na kama atakamata uenyekiti wa CHADEMA kutokea hapo CDM itakuwa ni mja ya institutions za RA.
 
Sasa hivi katika JF unatakiwa kuwa mwepesi kung'amua na kukwepa mawe. Bila hivyo utajikwaa, kuanguka na kuwa kibogoyo
 
Wakuu,
C) Tatu, Chama chetu kinonekana au kinatuhumiwa kuwa chama cha Wachagga . Hivyo mimi nitamaliza hoja hiyo ili tushinde 2015. Ndani ya mkakati huu anategemewa kuchota kura toka mikoa yote isipokuwa wachaga. Wanategema kutumia fitina ikibidi hasa kama mbowe atagombea tena. Ikionekana Mbowe ana nguvu watamlazimisha kwa kashfa iwe iwavyo.
D) Mbowe na Slaa wote wawmetoka kaskazini, SASA ni muda muafaka na kanda zingine nazo ziongoze CHADEMA kama tumekomaa na tunataka kuingia ikulu.Hoja hii nayo inategewa kuwapa nguvu mikoa mingine. Tayari wapambe wako kazini isipokuwa kanda ya kaskazini.

E) Kete kubwa kuliko zote ni kuwa, kwa kuwa Chadema inatuhumiwa kwa udini na waislamu, mimi ndiye suluhisho pekee. Hapa tayari kuna watu wamesambazwa kwa wajumbe ambao ni waislamu ndani CDM ili wamwuunge hasa wale wanaoonekana kuwa wataweza kumaintain nafasi zao na kuwashawishi potetial leaders to be. Kumbuka uchaguzi wa taifa utafanyika baada ya chaguzi za ngazi ya chin kuisha kote nchini.

Humbly I submit.
Hizi hoja za ubaguzi wa namna hii mnazitoa wapi wapi? Hii sasa inakera sana, hv tumekosa hoja za kuzungumza mpaka tuanze kueelezea mambo ya kibaguzi kama haya? Huu sasa utoto, yaleyale ya UVCCM na Vigogo wa CCM.
 
Kigoma is firmluy behind me and I dedicately serve them. Don't ever under estimate watu wa Kigoma.

Ni vizuri kuwa zitto ameibuka na kusema sisi wengine tunaumwa zitophobiasis,
Maswali matatu, kwa zitto kabla hujatoka humu ndani
Ulikuwa na uhusiano gani na Jack zoka Naibu mkurugunzi mkuu wa usalama wa Taifa hadi mkawa mna mawasiliano naye mara zaidi ya moja hasa kipindi cha uchaguzi mkuu? Mna undugu, biashara au nini? Je hukuona ni vizuri uwaambie viongozi wako ili wajue kuwa una masiliana yenye nia njema ya mambo mengine na mtu ambaye anatuhumiwa cha CHADEMA kwa kuchakachua kura zao?
Una uhusiano gani na Fisadi Rostam Aziz hadi ukawa na mawasiliano naye mara nyingi kama mlivyonukuliwa na Gazeti la mwanahalisi. Hukuona umuhimu wa kuwashirikisha viongozi wako?
Je unaweza kutuambia humu ndani kwamba sina mpango wa kubomoa chadema na kuhamia NCCR kama ilivyoandikwa na Gurti na wajumbe wengine humu JF?
 
Uwongo na propaganda. Kuna watu hawana raha bila kuandika kuhusu Zitto. Wanaugua ugonjwa wa zittophobiasis!
I challenge huyu rafiki yangu atajwe humu ndani.
Yote haya ni habari za kusadikika kwa malengo maalumu.
Hapakuwa na makubaliano yeyote kwamba uchaguzi wa chama ujao nitagombea. Kila mwana chadema ana haki ya kugombea na sio Zitto peke yake kama inavyorajibu kujengwa.
Acheni hila la kutuvuruga. Acheni tujenge chama chetu. Thread kama hizi zina lengo moja tu, kutugawa viongozi wa chama.
I have full trust to the current leadership and I am totally loyal to the Leadership of the Party under Rt.Hon. Freeman Mbowe!



Kwa mara ya kwanza nimekugongea THANKS

The Following 5 Users Say Thank You to Zitto For This Useful Post:

Goldman (Today), King of Kings (Today), Mwita Maranya (Today), Sn2139 (Today), SUWI (Today)​
 
Heee, hiyo mikakati inatishia uhai wa CHADEMA manake kusema ukweli tuhuma hizo za ukasikazini na udini zipo masikioni mwa watu. Nadhani kuna watu wanzisambaza kwa makusudi. Kwa kutumia hiyo mikakati naona kuna hatari ya Zitto kushinda, amejipanga. Hivi unakumbuka JK alipochukua form ya kuomba ridhaa ndani ya CCM ili achaguliwe kuwa mgombea wao mwaka 2005 pale Kibaha, aliulizwa je ukishindwa, akasema hapa hakuna kushindwa na kweli alishinda. Tusubiri tuone ya Zitto.

INA MAANA TAYARI UMESHAAMINI??? KWELI TUNA KAZI.
HIVI MNAMWONA ZITTO KAMA JINGA FULANI VILEEEEE?? AU UKIMYA WAKE NDO MMEFANYA MRADI WA MAJUNGU??
Anyway, KAma kuna mtu wa CDM tunaomba updates za maana kwenye website yenu, haya majungu huwa yanastress
Tunachotegemea ni nguvu ya watu, sio ya Slaa, Mbowe au Zitto.
 
hii thread sasa ifungwe ..... zitto ni mstaarabu na uzuri huwa yupo humu JF ......ameshakanusha haya yote .... sioni authenticity ya hii habari na hakuna mantiki yeyote ya kudiscuss kitu ambacho kiko proved

mvua zimeanza kunyeesha sehemu nyingi na sasa nasikia ngurumo kila mahali ...... tujadili kuongeza uzalishaji kwa kilimo chetu cha mvua za masika .....

nahisi kilimo kwanza ni mpaka 2020
 
Katika zengwe zilizopikwa dhidi ya Zito, hii inaongoza. Nilitegemea atumie hekima zaidi kunyamazia thread kama hizi lakini anapojaribu kuzijibu ndio anauchochea moto wenyewe.
Jamani mwacheni Zitto hatagombea 2015 katiba ya sasa inamzuia, umri utakuwa bado!
 
Thanks Zitto but this of WATU WA KIGOMA goes both way.

Here i mean "They are watching your steps and now they know Mbivu na Mbichi............" Do you know about this?

Yes, Yes.... We should'nt ever under estimate watu wa Kigoma.
Kigoma is firmluy behind me and I dedicately serve them. Don't ever under estimate watu wa Kigoma.
 
Back
Top Bottom