Zitto Kabwe: Say NO to Posho

KATI YA WATU AMBAO WANA WAKATI MGUMU HAPA DUNIANI NI MTOA MADA. SIJUI ANAJISIKIAJE HUKO ALIKO! KAMA LEMA NDO KAITUMA HII DIV5 BASI POLE YAKE!!
CHADEMA INA WABUUNGE VILAZA WAWILI AMBAO NI LEMA NA SHIBUDA.
#www.teamzitto.com.
 
Mungu anacheka - By Rose Mhando

WAKUU HABARI ZA SASA!,

Tazama hii kitu, alisema hapa achukui posho yoyote hile mpaka kwake kigoma RCC NA BARAZA LA MADIWANI, na mheshimu sana zitto ninacho muona kama atambui akuna siri ya watu wa wawili duniani isijekujilikana , siri ni yako tu ndio aitajulikana, Zitto GODBLESS J Lema
Ushahidi-+Zito.jpg
 
Sasa hapo ndo namshangaa ZZK. Kwa nini asipeleke kwenye account ya M4C ikaelimishe wananchi ili 2015 wabunge wa CDM waongezeke hoja ya kufuta posho ipite?
 
Sasa hapo ndo namshangaa ZZK. Kwa nini asipeleke kwenye account ya M4C ikaelimishe wananchi ili 2015 wabunge wa CDM waongezeke hoja ya kufuta posho ipite?
Kwa sababu m4c inakusanya pesa za wizi
 
Kurudisha posho wakati CDM inahitaji pesa kutoa elimu ya uraia itakayowakomboa wananchi zidi ya ujangili, ufisadi na mihadarati ya CCM, ni mkakati duni labda kama ana malengo binafsi. hausaidii hoja na msimamo wa CDM kufuta posho zote na kuboresha mishahara ya watumishi wa umma kupita, bali kumpa hoja ZZK kuwa yeye "binafsi" ni mtu wa action na sio maneno. Huo ndio unafiki anaopaswa kuuepuka.
 
Uhhh! Ndio walipotufikisha haya majamaa ya ccm. We no longer believe people can do things for good intentions. Everything good you do watu wanafikiri ni uchaguzi. Can we get out of the cage for a moment?
Mkuu Kitila Mkumbo, kitendo cha Zito kujijenga kwa mtindo wa kujitenga na wenzake kunatia shaka. Kumbuka wakati wa uchaguzi wa 2010, wagombea kadhaa wa ubunge waliopigiwa debe na Zito, baada ya uchaguzi kulikuwa na tetesi kuwa waliuza ushindi wao kwa maccm, mfano ni jimbo la Mbozi Mashariki, jimbo la Mbeya vijijini, jimbo la Kibaha na Jimbo la Musoma vijijini kunatia shaka pia. Mkuu Mkumbo, kulikuwa na tetesi pia kuwa wewe ni mtu wa karibu sana na Mhe. Zitto penginge unaweza kutuondolea wasiwasi juu ya mwenendo wa Zitto unaotia shaka?
 
Mkuu mimi sipo upande wa ZITTO lakini tambua unapoanzisha thread kama hii unaianika akili yako na kuiweka katika watu wasio na ufahamu wa kutosha juu ya masuala ya Fedha, hii Risiti upewa mtu pale yeye anapolipa fedha na ndio maana kinachoonekana hapo ni kuwa Zitto ndio aliyetoa pesa na sio aliyepokea.Jitahidi kuchunguza kitu kabla ya kupost kwani hii iliisha wasilishwa hapa jana na ilijadiliwa na makosa mengi yalionekana nashangaa leo unaibuka nayo tena. Kwa hiki unachokifanya naona unaondelea kumpaisha Zitto badala ya kumshusha.

Mie nafikiri huyu jamaa aliyepost sio kwamba anania mbaya na Zitto, ila anachojaribu kufanya ni kumsafisha Zitto; lakini kwa watu ambao akili yao ni nyepesi hawawezi kuliona hilo. Pamoja na hayo hata kama Naibu katibu Mkuu wetu anamapungufu ni wazi kuwa anjua kujenga hoja ukilinganisha na Lema. Tunachotakiwa ni kukaa pamoja na kuangalia wapi turekebishe ili haya magamba yasifanikiwe kuendelea kuongoza nchi 2015. Ila tukiendekeza majungu haya hatutafika mbali maana hayo aliyosema Mh. Lema kuhusu posho za mashirika ya umma, hakuna uthibitisho wa wazi ambao anaweza kutupakutuonesha na tukamwelewa sanasana ni propanganda tu.
 
:A S 11:Nawashangaa watanzania,tuna kasumba moja, wale wakweli uwa tunawapiga vita na mifano ninayo lkn wale wanafiki tunawashangilia,ila watanzania wachache tunaolitakia mema Taifa letu tuko pamoja nawe,hachana na vichaa kama Lema na ambatana na weredi
 
Ningekuwa Zitto, ningepokea Posho

Zuberi Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi amekataa kupokea poso ya vikao (Sitting Allowance). Anasema si halari kulipwa fedha hiyo kwa kuwa kukaa kwenye vikao vya bunge na vingine anavyoshiriki kama mbunge ni sehemu ya kazi zake kama mbunge.


Mbunge wa Arusha Mjini (chadema) Godbless Lema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema anamwona Zitto mnafiki kwa kile anachodai kukataa kwake posho ni hadaa kwa wananchi yenye lengo la kujipatia manufaa ya kisiasa, na kamwe (Zitto) hana chembe ya uzalendo kwa kuwa umasikini sio kipimo cha uzalendo. Hii ndio ajenda iliyotawala katika mitandao ya kijamii na magazeti.


Ukifuatilia msingi wa hoja hii tangu uibuke miaka miwili iliyopita, na ukisoma kwa makini maandiko ya Zitto na Lema katika mitandao ya kijamii waweza kugundua kuwa hawa wanasiasa wawili wana ajenda inayofanana, tofauti yao ni uwasilishaji, bila shaka na nia zilizojificha nyuma yao.


Kwa mujibu wa Lema mbunge hupokea kiasi cha Tsh 70,000 kwa kila siku anayoshiri vikao vya bunge na kamati zake. Kwa mantiki hii mbunge anapokea zaidi Tsh 12,000,000 kwa vikao vyote vya Bunge kwa Mwaka.


Pia Lema anadai kuwa Zitto kama Mwenyekiti wa PAC anapokea posho ya kikao kati Tsh 700,000 hadi 1,000,000 kwa kikao kimoja katika vikao vinvyofanywa na mashirika mbali mbali hususani Mashirika ya hifadhi za Jamii. Mashirika haya kwa ujumla kama yatafanya vikao vikao ishirini kwa mwaka Zitto atakuwa amepokea kiasi cha Tsh 14,000,000. Kiasi hiki kinaweza kuongezeka kama mpaka 20,000,000 kwa kuwa Zitto kama mwenyekiti wa PAC hupata mialiko wa kuhudhuria vikao mbali mbali.


Tarehe 7 Juni, 2011 Zitto alimwandikia Katibu wa Bunge barua ya kumuelekeza kuwa posho zake za vikao zielekezwe katika taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI) kupitia akaunti Na. 0IJ1087940900 ya benki ya CRDB tawi la Kigoma. Tarehe 10 Juni, 2011 Katibu wa Bunge alimwandikia Zitto barua ya kumtaarifu kuwa, ameelekezwa na Spika amueleze kuwa utaratibu wa Bunge ni kumlipa mbunge stahiki zake moja kwa moja, na kuwa mbunge mwenyewe anaweza kutoa pesa na kuzipeleka anakotaka. Siku hiyo hiyo ya tarehe 10 Juni, 20111 Zitto alimwandikia Katibu wa Bunge akimwelekeza asimlipe posho za vikao.


Kwetu Ukerewe tunazo changamoto nyingi za maendeleo. Jitihada zozote zile, ziwe kubwa au ndogo za kupunguza changamoto hizi zinakaribishwa. Umasikini wa kipato umekuwa ukiongezeka. Elimu ya watoto wetu na ndugu zetu imekuwa ikishuka kadri miaka inavyokwenda. Shule hazina walimu, kuna upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada, nyumba za walimu na vyumba vya madarasa. Huduma za afya bado hazirizishi. Vituo vya afya havitoshi, na katika vijiji ambavyo kuna vituo vya afya watoa hudumu hawatoshi. Katika zahanati ambako dawa zinapatikana, wananchi hawa uwezo wa kuzigharimia huduma za afya. Upatikanaji wa maji bado ni kitendawili, na wakati wa kiangazi hali huwa mbaya zaidi.


Kama ningekuwa mbunge nisingekataa posho kama anavyofanya Mbunge wa Kigona Kaskazini Zuberi Zitto Kabwe. Wapiga kuwa wangu wangeniuliza yego usarile? Wengine wangeniita mbula bhwenge. Ingekuwa vigumu kwao kunielewa. Ningekosa ujasiri wa kusimama mbele yao. Nitaupata wapi ujasili wakati nimekataa Tsh 60,000,000 za posho za vikao vya bunge kwa kipindi cha miaka mitano niliyo wawakilisa ?


Wangeniambia ulipaswa kuchukua posho utuletee tuitumie. Nusu ya kiasi hicho kingesaidia kujenga shule ya msingi Chibasi kule Malelema ili kupunguza mateso kwa watoto wanaotembea kilometa nyingi kwenda kusaka elimu katika shule ya msingi Mubule. Kiasi kilichobaki kingesaidia kumalizia ujenzi wa shule ya Sekondari Nyakuna, ambayo wananchi wa kata ya Nyamanga wamekuwa wakijitahidi kumaliza kwa kipindi cha miaka minne.


Ningekuwa mbunge wa ajabu kama Zitto kwa kukataa 70,000,000 ambazo ni posho za vikao vya mashirika ya umma kwa mwaka. Wananchi wa Chibasi wangeniuliza kwa nini nisingepokea pesa hizo niwapelekee wamalizie ujenzi wa zahanati yao ili kupunguza mateso kwa akina mama wanaosafiri mpaka Nyamanaga kutafuta tiba?


Ningekwepa kupita Bukonyo ili nisisikie kilio chao cha uchakavu wa zahanati na kukosekana kwa nyumba ya mganga, hali inayiomlazimu (mganga) kusafiri umbali mrefu kufika kazini.

Watoto wa kike wamekuwa waathirika wakubwa wa ukosefu wa mabweni katika shule nyingi za Ukerewe. Wanakaa geto. Wengi wao wamepata ujauzito na kukatisha masomo yao. Hitaji la mabweni ni kubwa sana. Dhamira yangu ingenisuta kama ninge kataa posho ya vikao vya baraza za madiwani na RCC.
Kwangu mimi ni uendawzimu kukataa posho ya wananchi. Wao ndio walipa kodi wakuu. Kuchukua posho yao na kuwarudishia ndio uwajibikaji. Tatizo ninaloliona kwa wanasiasa wetu ni ubinafsi. Tunakataa posho kwa manufaa binafsi, na wanaozipokea, na hata kudai ziongewe ni kwa masilahi binafsi.


Awali Zitto alipendekeza posho yake ipelekwe kwenye taasisi ya maendeleo ya Kigoma (KDI). Hii ilikuwa hoja ya msingi kwa kuwa lengo la taasisi hii ni kupeleka maendeleo kwa wananchi. Ningemuona Zitto mzalendo zaidi kama angepokea posho na kuzipeleka kwa wananchi kupitia taasisi hii kuliko kuzikataa wakati watu wa jimboni kwake hawana uhakika na elimu bora, afya na maji safi.


Naunga mkono hoja ya kupitia mfumo wa kutoa posho, hasa kwa wabunge. Kama mantiki ni kuwa hizi pesa ni za wananchii na kuwa si jambo jema kwa wabunge kujinufaisha kwa pesa za wananchi, wakati wenye nazo wanataabika, basi serikali iweke utaratibu wa posho kuelekezwa katika mfuko ya jimbo ambako zitatumika kwa maelekezo ya wananchi wenyewe.




Martin M. Malima

 
swala la posho ni swala binafsi zaidi siyo la kumsemea mtu kwa vyovyote vile kwahiyo zito anahesabu zake.
 
swala la posho ni swala binafsi zaidi siyo la kumsemea mtu kwa vyovyote vile kwahiyo zito anahesabu zake.

Chama kipya, sula la posho ni zaidi ya unavyolichukulia. Ukifiatilia msingi wa hoja ya posho na maelengo yake utagundua kuwa lengo lilikuwa ni kumsaidia mwananchi. Bila shaka ndiO maana Zitto aliomba posho yake ipelekwe KDI
 
Swala la posho ni swala ambalo kwa mtu makini ambaye anajua anachokifanya as Zitto huwezi kushabikia kwamaana unatambua kuwa uko kwaajili ya uwakilishi wa wananchi na sio wa taifa lingine bali taifa lako nawe ni mzawa wa taifa hilo !, na si jambo jema la kupokea posho kwa kazi unayofanya wakati wananchi hawapati hata pesa ya kutosha mlo wa siku moja! big up zitto kwa uamuzi na uzalendo wako kwa watanzania!
 
Mkuu Kitila Mkumbo, kitendo cha Zito kujijenga kwa mtindo wa kujitenga na wenzake kunatia shaka. Kumbuka wakati wa uchaguzi wa 2010, wagombea kadhaa wa ubunge waliopigiwa debe na Zito, baada ya uchaguzi kulikuwa na tetesi kuwa waliuza ushindi wao kwa maccm, mfano ni jimbo la Mbozi Mashariki, jimbo la Mbeya vijijini, jimbo la Kibaha na Jimbo la Musoma vijijini kunatia shaka pia. Mkuu Mkumbo, kulikuwa na tetesi pia kuwa wewe ni mtu wa karibu sana na Mhe. Zitto penginge unaweza kutuondolea wasiwasi juu ya mwenendo wa Zitto unaotia shaka?

Shida yetu ndiyo hiyo kuishi kwa tetesi. Nyerere aliwahi kuwauliza waandishi wa habari wa Kenya kuwa 'je wewe ukisikia kuwa mimi babako utakubali?' Hii ilikuwa ni baada ya kumuuliza kwamba yeye wana ugomvi na mzee Kenyatta. Watu wanazusha mambo bila ushahidi wowote na sisi tunashadadia na kuyabeba mzobemzobe kana kwamba ndiyo kweli. Na tunatumia muda mwingi kujadili mambo ya kuzushwa na muda mfupi kabisa kujadili ukweli. Bahati mbaya kazi ninayoifanya inanitaka kila mara nifanye argument on the basis of evidence. Kama hakuna ukweli uliyo bayana sishughuliki na jambo hilo.

Inategemeana unamaanisha nini unaposema mtu wa karibu na Zitto. Kama unamaanisha urafiki, yes, ni rafiki yangu kwa miaka mingi kabla hata sijaijua CHADEMA na wala hakuna mtu anayeweza kunichagulia marafiki.
 
Back
Top Bottom