Kama hujui uliza ueleweshwe. Zitto hakupokea hizo pesa na ndio maana zimekatiwa risiti ili zirudishwe benki.
Viongozi wa juu wa chama wamkemee huyo lema na zitto. Huo ndio mpasuko halisi.Hii Nchi inakabiliwa na intellectual deficit ya hali ya juu sana yaani badala ya Wapinzani kutumia muda wao kui-attack CCM wanashambuliana wenyewe kwa wenyewe,Wasichokijua hawa wapuuzi ni kwamba wanaipa CCM opening bure ya kuwa-attack na hata kupoteza uhakika wa kufanya vizuri katika chaguzi mbalimbali zijazo.Chadema acheni huu upuuzi wenu mnakiumiza Chama!!!
Nilimwambia Godbless J Lema JF siyo Sakina au Stendi ya Vifodi, angalia sasa unavyomdhalilisha Lema.
Mhhh sijaona sehemu ambayo Zitto kasign kuonyesha kwamba kapokea hiyo pesa cz listi inaweza kuandikwa bt pesa mtu usichukue ww leta ushahidi hapa unaonyesha sign ya zito kupokea hiyo pesa
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mkuu umemifurahisha sana, haya majibu nilikuwa sijayaona. Vijana wanatoana roho JF kumbwe mwenyewe kashafunga mjadala wa posho tangu 2011, si kwa maneno matupu bali kwa vitendo. Na hapo kwenye kukataa msamaha wa kodi ndipo aliponikosha zaidi.Mkuu, kuna haja ya kujikumbusha majibu ya ZITTO katika hili
ZITTO KABWE NAYE AJIBU BAADA YA LEMA KUANDIKA WARAKA KUWA ZITTO NI MNAFIKI
Zitto katika Facebook wall yake leo.
Kuchukua au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi (principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho.
Sio posho tu, hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu, kwamba siwezi kuwa Waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao.
Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu Serikali haiwalipi walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu za afya huko vijijini nk.
Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.
Duh sipendi kama kuna unafiki wowote zitto anafanya,
ila hapa mkuu umeonesha ifinyu wa fikra kabisa ndugu yangu.
Hapo serikali ime acknowledge kupokea kiasi cha fedha kutoka kwa zito, bahati mbaya sioni vema kwa imelipwa kama nn maana hzo ni general receipt so is multi-purpose.
Mkuu umemifurahisha sana, haya majibu nilikuwa sijayaona. Vijana wanatoana roho JF kumbwe mwenyewe kashafunga mjadala wa posho tangu 2011, si kwa maneno matupu bali kwa vitendo. Na hapo kwenye kukataa msamaha wa kodi ndipo aliponikosha zaidi.