Zitto Kabwe: Ndoto yangu ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mwamsheni bwana Mwandiga jamani aache kuota asije akakojoa kitandani!!
 
Ule mkoa ulisahaulika sana! JPM kama alitaka kuukumbuka, lakini mtu kama Zitto anamponda?
 
Huyu atakuwa rais kama Mungu anao mpango wa kuliadhibu taifa hili la Tanzania. Wala hatapakwa mafuta atakuwa kama walivyokuwa wakina nebukaridezar au dario.

Baba Paskali,
Salaam, Mkuu kwa kweli sikatai hoja zako na mtizamo wako kwa Kiongozi wa ACT Wazalendo ZZK, Kwa kweli moja ya sifa ya mwanasiasa ni maono na maono chanya, hakuna kiongozi asiye na maono.
Lakini linafika suala la nani kuwa nani ni Mipango ya Mungu, Rais ni cheo cha mwisho kabisa katika uongozi wa nchi, Lakini lazima ukumbuke kuwa MUNGU ndiye anayewaweka Wafalme, Rais ni Mfalme hata kama ni kwa muda maalum lakini ni Mfalme.
Rejea Biblia:
A:Mungu alipomtuma Samwel kumpaka mafuta Saul kuwa mfalme wa Israel

B.Mungu alipomtuma Samwel kumpaka mafuta Daud,
Kwa hiyo wafalme wote ni chaguo la MUNGU.
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa ndoto yake siku moja ni kuiongoza Tanzania akiwa katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Mimi urais nautaka, sababu naamini nina uwezo, nina maarifa, nina uzoefu wa kutosha katika siasa kuweza kuiongoza nchi yetu kupiga hatua mbele, lakini siwezi kusema moja kwa moja kuwa nitagombea Urais waka 2025

“Uamuzi wa kugombea unatokana na kudra za Mwenyezi Mungu chama lazima dhamana na baadaye wananchi watoe dhamana.

“Pia kuna kilio cha ushirikiano wa vyama vya upinzani ili kupambana dhidi ya Chama Cha Mapinduzi, kama tutashirikiana inawezekana mgombea nikawa mimi au nisiwe akawa mwingine,” Zitto

Video: Mwananchi
Zitto anasema ana uzoefu? Uzoefu gani? Ukimsikiliza vizuri utagundua anatamani madaraka ... ile hali ya kutukuzwa na siyo kubadilisha maisha ya Watanzania. Kama nchi tuna tatizo, maana kijana mdogo kama Zitto hajawahi kufanya kazi zaidi ya utalii wa kisiasa.
 
Ataambulia kura za akina Kuga, Spunda,Muttamwega na Dovutwa labda agombee kupitia ushirika wa vyama vyote vya upinzani.
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa ndoto yake siku moja ni kuiongoza Tanzania akiwa katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Mimi urais nautaka, sababu naamini nina uwezo, nina maarifa, nina uzoefu wa kutosha katika siasa kuweza kuiongoza nchi yetu kupiga hatua mbele, lakini siwezi kusema moja kwa moja kuwa nitagombea Urais waka 2025

“Uamuzi wa kugombea unatokana na kudra za Mwenyezi Mungu chama lazima dhamana na baadaye wananchi watoe dhamana.

“Pia kuna kilio cha ushirikiano wa vyama vya upinzani ili kupambana dhidi ya Chama Cha Mapinduzi, kama tutashirikiana inawezekana mgombea nikawa mimi au nisiwe akawa mwingine,” Zitto

Video: Mwananchi
Lini kama ni 2025 haiwezekani kwani chama chake kilisema kitafanya kazi na mama kwa miaka 9
 
Hahahahah labda wa Mwandinga tu. Zitto ana tabia za kirundi kirundi. Yaani ni kama mhutu mhutu, chuki zisizokuwa na maana. Yaani uutake urais wakati unamtukama mtu ambaye alikuwa rais na kipenzi cha watanzania?? Hakika Zitto atakufa bila kuwa rais na it will never happen under the system, maana kauli zake zipo rekodedi vizuri kabisa na zitabaki kizazi hadi kizazi. Mnafiki sana mdini na mkabila na hafai
Sema kipenzi Chako,
Aliekwambia kwamba watu wote walimkubali mwendazake ni nani?
Binafsi hakupata kura yangu usitujumuishe
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Mb

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa ndoto yake siku moja ni kuiongoza Tanzania akiwa katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Mimi urais nautaka, sababu naamini nina uwezo, nina maarifa, nina uzoefu wa kutosha katika siasa kuweza kuiongoza nchi yetu kupiga hatua mbele, lakini siwezi kusema moja kwa moja kuwa nitagombea Urais waka 2025

“Uamuzi wa kugombea unatokana na kudra za Mwenyezi Mungu chama lazima dhamana na baadaye wananchi watoe dhamana.

“Pia kuna kilio cha ushirikiano wa vyama vya upinzani ili kupambana dhidi ya Chama Cha Mapinduzi, kama tutashirikiana inawezekana mgombea nikawa mimi au nisiwe akawa mwingine,” Zitto

Video: Mwananchi

Mbona alisema atagombea 2015 akiwa CHADEMA? Huyo huwa anaangalia upepo. Kwa Sasa hata aligombea hawezi kushinda kwa sababu mvuto kwa watu umeisha.
 
Ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania anayejiona ana uwezo wa kutosha kiakili, kiafya na kiushawishi na aliyejiandaa vya kutosha kutamani kuwa Rais wa nchi siku moja.

Zitto Kabwe ni mtanzania na anaonekana kujipanga kwa lengo hilo tangu zamani.

Baada ya kuona amegundulika mapema mpango wake wa kufanya mapinduzi ya ndani ya CHADEMA ili awe na uwezo wa kujiamulia mambo mwenyewe kushindikana, akakimbilia kuanzisha chama chake.

Sasa njia ipo wazi kugombea atakavyo bila kuwa na mtu yeyote wa kumzuia ndani ya chama chake alichokiita ACT.

Aendelee na harakati zake japo wengi tunaona kuwa bado hajaweza kuwa na ushawishi wa kutosha kumfanya awe Rais wa nchi.
 
Kama anamchukia alokuwa Rais wetu kipenzi cha watanzania alotangulia mbele za haki Jemedari, Jembe, Jeshi (JPM), labda awe Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB)
Zito anakubalika sana huku kusini Lindi na Mtwara mtaji wa kuanzia anao haswaa na si wengine Bali ni sisi Wana korosho wa Kusini, tuna commonality flani Kati yetu wanakusini na Wanakigoma, kiufupi tuna historia ya kutengwa kwenye mikakati ya maendeleo kwenye hii nchi tangu ukoloni hadi uhuru.
 
Yupi aliyedai kuwa COVID 19 haukuwepo Tanzania? Huwa unafuatilia mambo kweli wewe? Kuna wakati ni bora kukaa kimya!
Sasa unataka tubishane juu ya hili pia? Muda huo huwezi kuutumia kufanya jambo jingine la maana?

Kwa hiyo wewe unajiona ni mfuatiliaji wa mambo, na kuelewa hayo unayofuatilia, au unaona maluweluwe ya kupoteza akili yako kwa kuwa chizi wa kutetea mtu mwingine bila hata kufikiri?
 
Hakuna mahali magufuli aliwahi sema corona haipo.

Alichokua anapingana nacho ni njia za kupambana nayo. Ambayo alikua sahihi.

Ambapo baada ya muda zimekuja kutumika na wengine.
Mkuu, hakuwahi kuwa "sahih"i kwa lolote.
Ni shukrani tu kwa Mwenyezi Mungu, katuepusha na janga. Hakuna ajuaye hadi sasa ilikuwaje nchi nyingi za kiafrika tuliponea chupuchupu. Huenda kuna siku tutajua, baada ya tafiti kufanyika.
Usitafute kumpa sifa ambazo hakuwa nazo kabisa, na zaidi ya yote, kiburi chake ndicho kikawa mwisho wake.

Bila COVID-19, leo hii akina Mbowe wangekuwa katika hali ngumu sana.
 
Back
Top Bottom