Zitto Kabwe: Mayanga Construction ni kampuni ya hayati Magufuli!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,168
142,295
Akiongea na waandishi wa habari KC Zitto Kabwe wa ACT wazalendo amesema kampuni ya Mayanga Construction iliyoshiriki ujenzi wa Chato International Airport ni ya hayati Magufuli.

Je, taarifa hizi zina ukweli wowote au ni uzushi uliozoeleka wa Zitto?

Nchi ngumu sana hii!
 
Legacy ya JPM si ya kimchezo mchezo, yani hadi leo hii hawaamini mwamba wa dunia miaka 6 tu maendeleo tele kuliko awamu zote

Yani Mtu ni Fisadi, Mwizi, Nduli lakini bado katoboa hadi kuifikisha TZ uchumi wa kati

TZ inahitaji Marais aina ya JPM wengi sana ili irudi tena uchumi wa kati
 
Mbona Zitto yuko busy sana na Magufuli?

Kama Mayanga Construction ni ya Magufuli atoe vielelezo kuthibitisha hilo, aweke documents mezani, sio hizi kelele zake za kila siku kumuhusu marehemu, huyu mtu anatumwa.

Naamini Zitto anamtumia Magufuli kama ngao yake ili kuficha uswahiba wake na mtawala aliyeko madarakani sasa.

Ajue tunataka Katiba Mpya ile rasimu ya Warioba, na wala sio tume huru; asitucheleweshe na lawama zake kwa marehemu za kila siku.

Kama ni kashfa hata Zitto alikuwa na zake pia, yale mapesa aliyopewa akiwa mwenyekiti wa PAC hatujasahau, pia anapewa mapesa na serikali iliyoko madarakani ili kudhoofisha upinzani, ajibu haya.

Ripoti ya CAG imetoka juzi, upigaji kila kona, amwambie rafiki yake awachukulie hatua wezi, sio kuimba Magufuli kila siku.

Tatizo lake Magufuli hakumuhonga kama anavyohongwa sasa na marafiki zake walio madarakani, ndio maana ameamua kuwa chawa wao ili kuwalinda, unafiki hata kama ni kipaji chake, apunguze kidogo.
 
Akiongea na waandishi wa habari KC Zitto Kabwe wa ACT wazalendo amesema kampuni ya Mayanga Cinstruction iliyoshiriki ujenzi wa Chato International Airport nu ya hayati Magufuli.

Je, taarifa hizi zina ukweli wiwote au ni uzushi ulioxoeleka wa Zitto?

Nchi ngumu sana hii!

Hizi taarifa zina ukweli KUWA Jiwe owned Mayanga Construction company through his brother in law! Kama vile Kikwete alivyomtumia Subash Patel kuiba na kuficha mali zake huko. Hawa wote ni wezi haijalishi kama ni waislam au wakisto! Wameihujumu nchi vibaya sana.
 
Back
Top Bottom