wakushanga
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 552
- 92
mmmm.............!!!!!!! mhh!!
Salaam wana JF,
Kwanza napenda kushukuru kwa michango iliyomo humu na inanihusu mimi. Kumekuwa na maneno mengi ya kweli na yasiyo ya kweli kuhusu suala la mimi kugombea nafasi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Ninaomba kusema ifuatavyo.
- Chama chetu kimepata viti vingi sana vya Bunge mara baada ya uchaguzi wa mwaka huu. Hii ni ishara njema sana kuwa sasa demokrasia nchini itakomaa kutokana na kuwa na Bunge Imara. Idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ndani ya Bunge inapunguza nguvu kwa kiasi kikubwa za CCM ndani ya Bunge. Tumejitahidi sana kukifikisha chama chetu mahala hapa. Nawapongeza sana viongozi wa chama chetu kwa mafanikio haya na hasa Mwenyekiti wa Taifa wa chama na Katibu Mkuu wetu ambaye alikuwa mgombea Urais.
- Chama chetu kimepata viti vya kuweza kuunda Kambi ya Upinzani Bungeni ama peke yake au kwa kushirikiana na vyama vingine vye wabunge. Kwa vyovyote vile atahitajika Mbunge mmoja wa Upinzani na hususani kutoka CHADEMA ambaye atakuwa KUB. CHADEMA bado haijatangaza utaratibu utakaotumika kupata KUB kutoka miongoni mwa wabunge wake. Nimewajulisha viongozi wangu wa chama kuwa nina nia ya kuomba ridhaa ya chama kuwa KUB. Suala hili linajadiliwa ndani ya chama na mara baada ya taratibu kuwekwa tutajua mwelekeo ni upi.
- Nimeomba ridhaa ya chama kuongoza wabunge wenzangu kwa sababu nina uzoefu wa kutosha ndani ya Bunge la Tisa. Tafiti zote zimeonyesha kuwa mimi ni mmoja wa wabunge bora kabisa ndani ya Bunge. Kwa miaka mitano mfululizo nimekuwa polled kama Mbunge Bora kuliko wote. Hii inatokana na michango yangu Bungeni ambayo wananchi wameona kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa sana ufanisi ambao wabunge wa CHADEMA wameonyesha. Nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na kuongoza kamati hiyo kwa umakini mkubwa na kurebisha mwenendo wa Mashirika haya. Fanikio langu kubwa sana na la kujivunia ni lile la kuweza kulirejesha Shirika la STAMICO katika Mashirika ya Umma na kurejesha mali zake zote ikiwemop mgodi wa Buhemba. Serikali ilikuwa imeamua kuua STAMICO kabisa! Nimekuwa pia mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge ambayo mwenyekiti wake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Haya yananipa uzoefu na maarifa ya kuwa Kiongozi bora wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
- Ninaamini kuwa Wabunge wengi wa CHADEMA wana uwezo wa kushika nafasi kama hii. Sina shaka hata kidogo na uwezo wa waunge 22 wa CHADEMA. Kwa kuwa uongozi ni ushirikiano, ninaamini kuwa nitaweza kuongoza kwa ubora kabisa Kambi hii na kuweka sura chanya ya CHADEMA mbele ya Umma wa Watanzania iwapo chama kikinipa ridhaa.
- Humu kwenye jukwaa hili kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakitunga uwongo wa dhahiri ili kunichafua mbele ya jamii. Ninawaomba wajue kuwa mimi ni mwadilifu sana. Udhaifu wangu mkubwa ni kupenda kusema ninaloliamini bila woga. Nimekuwa hivyo ndani ya Bunge na nimekuwa hivyo ndai ya chama siku zote. Sura ya kwamba mimi nimenunuliwa na CCM inajengwa makusudi na baadhi ya watu ili kunichafua na kunipunguzia heshima mbele ya jamii. Sura hii hujengwa kila ninapotaka kugombea nafasi ya uongozi na muda huo unapoisha shutuma hizo huisha. Naomba yeyote mwenye ushahidi wa jambo lolote aliweke wazi. Mimi sina V8, magari yangu yote second hand ya kununua kwa watu. Sijawahi kumiliku gari mpya. Mie sina nyumba Kimara (MTAKUMBUKA ILIWAHIWA KUSEMWA KUWA NINAISHI MASAKI..........), ninaishi kwenye nyumba ya kupanga NSSF Tabata na pia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mzazi mwenzangu ambaye ni Mwalimu pale Chuo Kikuu. Sio vizuri kwa kweli kunizushia uwongo kwa malengo ya kisiasa. Ninastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa UTU wangu. Kuchafuana hakusaidii kujenga nchi hii.
- Nina sababu zote na sifa zote za kuwa KUB. Ninasubiri ridhaa ya chama changu na Wabunge wa chama changu. Tuna ajenda moja kubwa, kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu ujao unafanyika kwa mujibu wa Katiba Mpya na mfumo mpya wa uchaguzi. Hii ndio kazi ya kwanza ambayo KUB anapaswa kuifanya. Kazi hiyo ninaiweza. Sijawahi kusimamia ajenda ikaishia njiani (mfano sheria mpya ya madini). Iwapo changu kikinipa ridhaa nitatoa uongozi uliotukuka, ee Mungu nisaidie.

Wise advice.Heshima kwako Zitto,
Mkuu kama umeomba ridhaa ya chama chako kwanini unaanza kampeni nje ya chama.Matangazo face book & JF ya nini ?.Nadhani umetumia njia sahihi kuomba nafasi hiyo muhimu tatizo langu ni jambo lenyewe kuwa public ukiikosa yatakuwepo malalamiko mengi yasiyo na msingi.
Heshima kwako Zitto,

Kuna mifumo miwili inayoweza kutumika kupata kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Mfumo wa kwanza ni ule wa Uingereza, ambapo kiongozi wa chama anakuwa moja kwa moja ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na waziri mkuu mtarajiwa. Kwa kufuata mfumo huu ina maana kuwa M/Kiti wa CHADEMA moja kwa moja anakuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na by extension anaweza kuwa ndio mgombea wa kiti cha urais katika chaguzi zijazo. Uzuri wa mfumo huu ni kwamba una-consolidate madaraka na mamlaka ya uongozi wa chama ndani na nje ya bunge. Ubaya au udhaifu wa mfumo huu ni katika maeneo mawili. Mosi, itakuwa vigumu kwa chama kuwaajibisha wabunge kwa sababu tayari M/Kiti wake ni kiongozi wa bunge. Vilevile ni vigumu sana kwa chama kuwaagiziza wabunge kutekeleza jambo fulani bungeni-kuna hatari ya wabunge kuwa wanatoa maelekezo kwa chama. Pili, mfumo huu unaenda kinyume na dhana ya CHADEMA ya kupinga kurundika madaraka kwa mtu mmoja. Kumbuka malengo mojawapo ya CHADEMA ni kumpunguzia Rais madaraka makubwa aliyo nayo.
Mfumo wa pili ni ule wa Amerika. Msingi wa demokrasia ya Amerika ni mgawanyo wa madaraka (separation of power). Wamerika hawapendi mtu mmoja arundikiwa madaraka. Kwa hiyo wao Kiongozi wa Chama sio lazima awe Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni, na kwa kweli siye. Ndio maana unaona leo aliyekuwa Spika wa Beraza la Wawakilishi Nancy Pelosi ndio anayegombea Minority Leadership. Wanachofanya wao ni kwa mbunge yeyote anayetaka kuwa kiongozi wao bungeni kugombea na wabunge wanamchagua mojawapo. Ni nafasi yenye ushindani mkubwa sana ndani ya wabunge wa Democrats au Republicans. Kama CHADEMA wataamua kutumia mfumo huu ina maana kwamba wabunge watakuwa huru kugombea nafasi ya kiongozi wa upinzani na wabunge wenzao kumchagua mojawapo.
Tatizo letu bado tumelewa siasa za umwinyi na uCCM. Tunaona kushindana ni jambo la hatari kwa chama. Kwa nini kushindana lionekana jambo la hatari na sio la kukuza demokrasiandani ya chama? Kuna ubaya gani kwa wanaotaka nafasi ya uongozi wa wabunge wapinzani kugombea na wenzao kuwachagua? Mambo ya kukwepa kushindana katika ngazi ya chama ndio yanayoletekeza uchakajuaji hata katika ngazi ya Taifa. Ni muhimu tukazoea siasa za ushindani ndani na nje ya vyama kwa sababu ndio msingi wa mfumo wa demokrasia ambao tumeamua kuufuata.
Kwa maoni yangu ni kwamba sifa moja muhimu sana kwa mtu atakayechaguliwa kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni awe ni mwenye uwezo wa kuwaunganisha wapinzani wengine katika bunge. Ni muhimu sana wapinzani wafanye kazi kama timu moja. Itakuwa ni balaa kama tutapata kiongozi ambaye yeye ana deal na wabunge wake tu na kuwatenga wengine. Ushirikiano bungeni uwe ni mwanzo wa ushirikiano mpana tunapojiandaa kwa uchaguzi wa 2015.
Mwisho, jambo la mtu kujitokeza mapema sio jambo la kulaaniwa. Ni jambo zuri na la kupongezwa. Kama unataka unasema sio unavizia au unataka watu wengine wakusemee. Tuna wabunge mahiri sana wa kambi ya upinzani na ninaamini jambo la nani awe kiongozi wao halitawayumbisha hata kidogo.
Wakuu zangu jamani mweee.. mbona Mama Anna Kilango,Chenge na wengine wamechukua fomu za kugombea Uspika na hakuna mtu alokuja hapa na kusema wao ni watu wa aina gani?..Heshima kwako Zitto,