Zitto Kabwe kuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni?

- Mkuu Dr. Kitila, maneno mazito sana isipokuwa tatizo moja ni kwamba kwanza Congress ya US wanajali sana Seniority ya mgombea, na pia heshima yake mjengoni hasa kwa upande wa pili kama ataweza ku-reach out na kusikilizwa, pia ability yake na compromise kwa masilahi ya taifa, bila kuathiri msimamo wa chama chake.

- Ushindani ndani ya vyama vya siasa ni muhimu sana, lakini ukweli ni kwamba masilahi ya chama ni lazima siku zote yawe mbele kuliko ukubwa wa kiongozi, infact hata huku US vyama hutumia tabia ya kulinda chama, ndio maana Gavana wa sasa anayemaliza muda wake New York State, alipotaka kugombea tena Rais Obama alimtumia ujumbe kwamba asichukue fomu kukilinda chama, Tent Lot aliambiwa na chama chake Republican kwamba asichukue fomu ya Minority Leader kwa sababu ya kashfa yake on Blacks kulinda chama, Gingrich aliweza kuwapenya Republicans bila kuchunguzwa vizuri mwennendo wake, matokeo yake akaishia kuwaingiza kwenye matatizo makubwa sana na kuishia kushindwa uchaguzi uliofuata wa Congress.

- Otherwise, Dr. Kitila una points nyingi sana na nzito sana, isipokuwa ninaomba kusema hivi, kwa maoni yangu tatizo linalotusumbua wa-Tanzania sio ushindani ndani ya vyama, isipokuwa kuambiana ukweli kiongozi anapokosea akiwa kwenye nafasi ya juu ya uongozi, ni wakati muafaka sasa tukajiwekea system ya kumuondoa kiongozi yoyote wa nafasi ya juu anapokosea, badala ya kusubiri mpaka uchaguzi ufike halafu kuanza kuchakachuana, kiongozi akikosea na kukiletea chama hasara kubwa mbele ya wananchi awajibishwe hapo hapao na haraka sana, Wenzetu ukitokea uchaguzi mdogo chama kikishindwa wahusika wanajiondoa au wanaondolewa haraka sana, sisi tunaanza kutafutana uchawi na kelele nyingi na yote ni kukwepa tu uwajibikaji.

Thanks.


William.

Brilliant! Ahsante sana. Nami nakubaliana kabisa mtu anayechaguliwa awe ni mtu anayeweza ku-command respect from all corners of the house. Mjadala mzuri na hoja ni murua. Ni vizuri mjadala wetu ukajikita kwenye misingi ya hoja, tuachane na majina kwa sasa. Tukishakuwa clear na principles za mtu tunayemtaka kuwa kiongozi wa upinzani bungeni, then tutaangalia ni nani katika waliopo anaye-fit katika hizo principles.
 
Kwa kweli zitto ni mbinafsi na anataka sifa siku zote. Zamani niliona kama mchapa kazi lakini sasa hivi si mwamini kabisa. hata ukifuatilia vikao vya mwisho vya bunge alikuwa ni mtu wa kubezwa kwa hoja zisizo za msingi hata kwenye mtu hawezi kunuunu hoja zake kama ni za msingi baada ya kikao. Nafikiri ni mtu aliye lewa madaraka na kqwa hiyo ccm lazima watamtumia. Hana hekima maana hata mama yake anamshangaa. Si dhani kama zitto atakuwa maarufu bunge lijalo, maana kuna wengi vijana watakao chukua sehemu yake. Ni mtu ambae anaona ni bora kuliko wenzake kumbuka amesha tangaza eti anagombea urahisi 2015 wakati hata umri wemyewe haumruhusu. Kwenye kampeni kila siku alitumia rugha hii eti wawa chague wabunge wengine wa upinzani ili wamsaidie bungeni kana kwamba yeye ndoo mpiganaje pekee wakati kuna wazee wa vijimambo wametulia. Kiongozi bora ni yule anaye jinyenyekeza kupata kibali cha viongozi wenzake na wanachi. Kuna siku tena alisha sema atagombea kwa chama asicho kijua pengine siyo chadema. na hili chadema wanajua na wamelipigia mstari mwekundu. mekaa kama mpita njia na ninahisi anajipendekeza ccm ili siku moja agombee uraisi kwa kupitia hii chama mfu. Zitto katengeneze huko upstaire ukiona kupo fiti na busara za kumwaga tutakupa ceho tena. Amina.
 
Safari hii demokrasia ichukue mkondo, atakayeshindwa amuunge mkono mwenzake.

Binafsi ninaamini Zitto ana uwezo wa kuwaunganisha wabunge wa vyama vyote vya upinzani vilivyoko bungeni kuliko Mbowe, na ni muhimu sana kwa wabunge wote wa upinzani kuwa na sauti moja.
maybe you dont know him, actually he is very intelligent
 
Zitto hafai kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwa sababu: 1. alikubali kuingia kwenye tume ya madini ya JK, 2. alisisitiza TANESCO kununua mtambo chakavu ya Dowans kinyume na sheria ya manunuzi ya serikali, hivyo atafagilia ufisadi, 3. amekuwa akiwavuruga wana-Chadema na kufagilia sana CCM, ataudhoofisha upinzani.

Ni heri kama Mbowe hataki na aseme sababu za kukataa basi ni heri Tundu Lissu afanye kazi hiyo kwa sababu ni mpiganaji toka siku nyingi na ni jasiri.

Pia kama Chadema watashirikisha vyama vingine kwenye kambi hiyo kama walivyofanya CUF kwenye kipindi cha mwisho basi TLP kisishirikishwe.
 
Ni wazi kabisa kwamba mtu yeyote anayeweka maslahi binafsi mbele (waziwazi na bila aibu) akikabidhiwa upinzani basi hakuna sababu ya kuwa na Uchaguzi 2015. Hapa namaanisha mrema, zitto, cheyo, n.k
 
Kati ya jambo ambalo litaidumaza CHADEMA, ni kuendekeza utengano kati ya Zito na Mbowe. Binafsi naona wote ni kitu kimoja ndani ya CHADEMA. Misimamo ya kila mmoja wao iheshimiwe, hakuna haja ya kumshambulia mtu kwa sabau ya msimamo wake.

Kwa upande wangu naona Zito anaweza sawa na ilivyo Mbowe, kuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni...
 
Zitto apewe nafasi kujifunza, anajifunza nini na ataelimika lini? Kuwa mature maana yake nini?
Hapo kwenye nyekundu. Hiyo ndio demokrasia unless kama mnaiga mfumo wa KiCCM. Pia mbona kuna wengine wamegombea Urais wakati Rais bado? Yaani Demokrasia iwe nje ya CHAMA lakini ndani ya CHAMA ni makosa enh!

Nahisi Mkuu huelewi mengi kuhusu Zitto na wala huelewi sababu iliyopelekea akajitoa kugombea Uenyekiti kipindi kile akichuana na Mbowe! Nisingependa kukueleza mengi kwa sababu inaonesha wewe ni muumini wa Zitto, ama labda hauko hapa TZ na hivyo hujui mambo mengi behind the scene, ila kwa kifupi ni kwamba Zitto is so corrupted na aliioneshwa vithibitisho hadi yeye kupelekea kutoa jina lake. CHADEMA wenyewe hawana imani na Zitto kwani ni zaidi ya Msaliliti. Au huna taarifa kwamba alikuwa anaendesha hadi V8 ya Mkono na bila kubadilisha namba, kama unabisha chukua namba ya v8 ya Zitto (kama bado anayo) nenda TRA ukaangalie jina. Kuna vouchers kibao alisaini toka Dowans, Barrick na hadi mafundi wa Caspian(ya R.A) kutumika katika ujenzi wa nyumba yake ya Kimara. Huyu mtu ni msaliti ndani ya CHADEMA. Kashikiliwa ma mafisadi na huenda akakiua chama kama ataendelea hivi. Hivi inakuwaje anajitangaza Facebook ati anagombea bila hata idhini ya chama chake?
 
Chadema ni lazima wawe careful kwani nimekwisha ona mbinu za ccm zikianza kutaka kuwagawa hawa wabunge katika makundi kupitia kuutafuta uongozi wa upinzani!! Zitto ana baggage nyingi za ccm toka enzi za Dowans haaminiki; kama sio Mbowe basi hata Halima Mdee ana uzoefu anaweza kuwa kiongozi wa upinzani na akamudu zaidi ya Zitto!!

Hapo umezungumza. Jamani, hivi vyeo ni dhamana. wananchi tumepiga kura kuwaweka tukiwaamini, unaposikia habari za wasaliti inauma sanaaa. I hope viongozi wa CHADEMA mnasoma maoni yetu. Tumewaamini mnapofika huko na kuwa vinginevyo mnatukwaza. Tunajua kuna wanaopandikizwa kuomba vyeo ili wanapozuiliwa ionekane kuwa chama hakina demokrasia, tunaelewa. Kila mara mkumbuke watu waliocha shughuli zao kuwapigia kura wakiamini kuwa ninyi mnaweza kuwawakilisha. Please dont make mistake in this.
 
Nahisi Mkuu huelewi mengi kuhusu Zitto na wala huelewi sababu iliyopelekea akajitoa kugombea Uenyekiti kipindi kile akichuana na Mbowe! Nisingependa kukueleza mengi kwa sababu inaonesha wewe ni muumini wa Zitto, ama labda hauko hapa TZ na hivyo hujui mambo mengi behind the scene, ila kwa kifupi ni kwamba Zitto is so corrupted na aliioneshwa vithibitisho hadi yeye kupelekea kutoa jina lake. CHADEMA wenyewe hawana imani na Zitto kwani ni zaidi ya Msaliliti. Au huna taarifa kwamba alikuwa anaendesha hadi V8 ya Mkono na bila kubadilisha namba, kama unabisha chukua namba ya v8 ya Zitto (kama bado anayo) nenda TRA ukaangalie jina. Kuna vouchers kibao alisaini toka Dowans, Barrick na hadi mafundi wa Caspian(ya R.A) kutumika katika ujenzi wa nyumba yake ya Kimara. Huyu mtu ni msaliti ndani ya CHADEMA. Kashikiliwa ma mafisadi na huenda akakiua chama kama ataendelea hivi. Hivi inakuwaje anajitangaza Facebook ati anagombea bila hata idhini ya chama chake?
Ndugu yangu siasa si ugomvi. Hivi kuendesha gari ya fulani ni makosa. Yaani ukiwa chama fulani basi wewe huhitajikii kuongea na wale waliovyama vingine. Tusizikubali siasa za namna hii. Mara nyingi huwa ni siasa za chuki. Hivi kutuma kampuni/mafundi wa caspian kwenye ujenzi ni tatizo? Hizi ndio evidence za corruptions? Amesaini vocha kuhusu nini? Kama kuna evidence za rushwa kama unavyosema na kwa kuwa CHADEMA ni wapiganaji kwanini hawakumkabidhi kwenye vyombo vya sheria? Nakumbuka pia mgombea Urais (katibu wa CHAMA) alisema M/kiti wa CHADEMA Iringa amepewa rushwa kule Isimani ili asigombee. Tena hili alitamka hadharani. Sasa hata haya ya ndani ya vyama CHADEMA wanashindwa kuyafikisha kwenye vyombo husika? Tuepuka saana majungu, tufikirie kujenga nchi yetu sote.
 
Sikatai wala sihoji uwezo wa Zito Kabwe Bungeni, lakini kwa wale waliokaribu nae naomba mumuombe asigombee hicho cheo, kwa sababu zifuatazo,
  1. akumbuke kuwa yeye kipindi cha Kafulila alikiweka chama pabaya kiasi cha kuchafua hali ya hewa, ingawa jitihada za makusudi zilifanyika kukinusuru chama
  2. kipindi cha kugombea uenyekiti, Zito vilevile alisababisha mchafuko wa hali ya hewa kwenye chama
  3. kipindi cha uchaguzi kulikuwa na tetesi kuwa alimuunga mkono Kafulila badala ya mgombea wa Chadema (hili sipingi zaidi)
ninachotaka kuamini, tangu achaguliwe kuingia kwenye kamati ya madini, anaonekana kupunguza uwezo wake wa kuhoji mambo, na hivyo kuonekana kama amechakachuliwa na kuandaliwa kukivunja chama.
ombi langu, chama kitafakari kwa kina faida na hasara za kumuweka au kutokumuweka Zitto katika nafasi hiyo, Chama cha C kitakuwa kimejiandaa kuchafua hali ya hewa kwa kuwatumia watu mbalimbali na hasa wale watakaosababisha sisi tugawanyike, jambo la msingi tuwe na ushirikiano na tushikamane katika kipindi hiki cha uteuzi wa mgombea wa Kambi ya Upinzani. Zitto kama anaamini hatachakachua basi atuhakikishie, lakini si mwamini sana katika hicho kiti cha mkuu wa kambi ya upinzani bungeni (siwezi kueleza kwa nini). lakini namwamini kuwa ni mpiganaji na anaweza kupigana vizuri akibaki kuwa mbunge wa kawaida.
 
jamani mnatuchanganya na hili swala la zito, hebu wekeni bayana tuelewe, tunasika tu mara anaarufu ya ccm mara anaendesha V8 ya mkono
kulikoni jamani!!!???
 
Zitto ana harufu ya CCM, i don't trust him anymore esp baada ya hoja zake kuhusu mitambo ya Dowans! Pia ni mfagiliaji mzuri wa CCM siku hizi!
I, too, don't trust that boy.
He has JK painted all over him (almost his mirror image)!
 
mpangamji

nimekuelewa vizuri nafikiri kama ushauri huu unge upeleka kwenye box la maoni ya chadema au website yao kwa masilahi ya chama

yasije yakawa ya ''SIASA MCHEZO MCHAFU''

tukawa tunafanya kazi ya :frusty:
 
mpangamji

nimekuelewa vizuri nafikiri kama ushauri huu unge upeleka kwenye box la maoni ya chadema au website yao kwa masilahi ya chama

yasije yakawa ya ''SIASA MCHEZO MCHAFU''

tukawa tunafanya kazi ya :frusty:

Asante, Tusaidiane kuelimishana,nafungua website ya Chadema nitoe mawazo yangu
 
Kuna mifumo miwili inayoweza kutumika kupata kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Mfumo wa kwanza ni ule wa Uingereza, ambapo kiongozi wa chama anakuwa moja kwa moja ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na waziri mkuu mtarajiwa. Kwa kufuata mfumo huu ina maana kuwa M/Kiti wa CHADEMA moja kwa moja anakuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na by extension anaweza kuwa ndio mgombea wa kiti cha urais katika chaguzi zijazo. Uzuri wa mfumo huu ni kwamba una-consolidate madaraka na mamlaka ya uongozi wa chama ndani na nje ya bunge. Ubaya au udhaifu wa mfumo huu ni katika maeneo mawili. Mosi, itakuwa vigumu kwa chama kuwaajibisha wabunge kwa sababu tayari M/Kiti wake ni kiongozi wa bunge. Vilevile ni vigumu sana kwa chama kuwaagiziza wabunge kutekeleza jambo fulani bungeni-kuna hatari ya wabunge kuwa wanatoa maelekezo kwa chama. Pili, mfumo huu unaenda kinyume na dhana ya CHADEMA ya kupinga kurundika madaraka kwa mtu mmoja. Kumbuka malengo mojawapo ya CHADEMA ni kumpunguzia Rais madaraka makubwa aliyo nayo.

Mfumo wa pili ni ule wa Amerika. Msingi wa demokrasia ya Amerika ni mgawanyo wa madaraka (separation of power). Wamerika hawapendi mtu mmoja arundikiwa madaraka. Kwa hiyo wao Kiongozi wa Chama sio lazima awe Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni, na kwa kweli siye. Ndio maana unaona leo aliyekuwa Spika wa Beraza la Wawakilishi Nancy Pelosi ndio anayegombea Minority Leadership. Wanachofanya wao ni kwa mbunge yeyote anayetaka kuwa kiongozi wao bungeni kugombea na wabunge wanamchagua mojawapo. Ni nafasi yenye ushindani mkubwa sana ndani ya wabunge wa Democrats au Republicans. Kama CHADEMA wataamua kutumia mfumo huu ina maana kwamba wabunge watakuwa huru kugombea nafasi ya kiongozi wa upinzani na wabunge wenzao kumchagua mojawapo.

Tatizo letu bado tumelewa siasa za umwinyi na uCCM. Tunaona kushindana ni jambo la hatari kwa chama. Kwa nini kushindana lionekana jambo la hatari na sio la kukuza demokrasiandani ya chama? Kuna ubaya gani kwa wanaotaka nafasi ya uongozi wa wabunge wapinzani kugombea na wenzao kuwachagua? Mambo ya kukwepa kushindana katika ngazi ya chama ndio yanayoletekeza uchakajuaji hata katika ngazi ya Taifa. Ni muhimu tukazoea siasa za ushindani ndani na nje ya vyama kwa sababu ndio msingi wa mfumo wa demokrasia ambao tumeamua kuufuata.
Kwa maoni yangu ni kwamba sifa moja muhimu sana kwa mtu atakayechaguliwa kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni awe ni mwenye uwezo wa kuwaunganisha wapinzani wengine katika bunge. Ni muhimu sana wapinzani wafanye kazi kama timu moja. Itakuwa ni balaa kama tutapata kiongozi ambaye yeye ana deal na wabunge wake tu na kuwatenga wengine. Ushirikiano bungeni uwe ni mwanzo wa ushirikiano mpana tunapojiandaa kwa uchaguzi wa 2015.

Mwisho, jambo la mtu kujitokeza mapema sio jambo la kulaaniwa. Ni jambo zuri na la kupongezwa. Kama unataka unasema sio unavizia au unataka watu wengine wakusemee. Tuna wabunge mahiri sana wa kambi ya upinzani na ninaamini jambo la nani awe kiongozi wao halitawayumbisha hata kidogo.

Asante mkuu, imetulia !
 
Ndugu yangu siasa si ugomvi. Hivi kuendesha gari ya fulani ni makosa. Yaani ukiwa chama fulani basi wewe huhitajikii kuongea na wale waliovyama vingine. Tusizikubali siasa za namna hii. Mara nyingi huwa ni siasa za chuki. Hivi kutuma kampuni/mafundi wa caspian kwenye ujenzi ni tatizo? Hizi ndio evidence za corruptions? Amesaini vocha kuhusu nini? Kama kuna evidence za rushwa kama unavyosema na kwa kuwa CHADEMA ni wapiganaji kwanini hawakumkabidhi kwenye vyombo vya sheria? Nakumbuka pia mgombea Urais (katibu wa CHAMA) alisema M/kiti wa CHADEMA Iringa amepewa rushwa kule Isimani ili asigombee. Tena hili alitamka hadharani. Sasa hata haya ya ndani ya vyama CHADEMA wanashindwa kuyafikisha kwenye vyombo husika? Tuepuka saana majungu, tufikirie kujenga nchi yetu sote.


Inawezekana unashabikia tu bila kujua undani wa suala lenyewe ama U-muumini wa Zitto ndio maana ni ngumu kubadili imani yako. Kuna vithibitisho vingi zaidi ya hivyo na hayo niliyowekea REd ni circumstancial evidence kujazia proof za usaliti uliokuwapo. Suala la CHADEMA kutolitolea tamko ilikuwa ni katika kukinusuru chama ukizingatia nguvu ya Zitto aliyokuwa nayo. Na hadi anagombea uenyekiti tayari alikuwa financed na hao mafisadi kiasi cha kwamba uongozi wa CHADEMA hasa mikoani walikuwa wana-msapoti yeye, na kwa sababu kuna watu wa aina yako wasioamini sidhani kama ingekuwa busara kwa chadema kwenda public.
 
Salaam wana JF,
Kwanza napenda kushukuru kwa michango iliyomo humu na inanihusu mimi. Kumekuwa na maneno mengi ya kweli na yasiyo ya kweli kuhusu suala la mimi kugombea nafasi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Ninaomba kusema ifuatavyo.
  1. Chama chetu kimepata viti vingi sana vya Bunge mara baada ya uchaguzi wa mwaka huu. Hii ni ishara njema sana kuwa sasa demokrasia nchini itakomaa kutokana na kuwa na Bunge Imara. Idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ndani ya Bunge inapunguza nguvu kwa kiasi kikubwa za CCM ndani ya Bunge. Tumejitahidi sana kukifikisha chama chetu mahala hapa. Nawapongeza sana viongozi wa chama chetu kwa mafanikio haya na hasa Mwenyekiti wa Taifa wa chama na Katibu Mkuu wetu ambaye alikuwa mgombea Urais.
  2. Chama chetu kimepata viti vya kuweza kuunda Kambi ya Upinzani Bungeni ama peke yake au kwa kushirikiana na vyama vingine vye wabunge. Kwa vyovyote vile atahitajika Mbunge mmoja wa Upinzani na hususani kutoka CHADEMA ambaye atakuwa KUB. CHADEMA bado haijatangaza utaratibu utakaotumika kupata KUB kutoka miongoni mwa wabunge wake. Nimewajulisha viongozi wangu wa chama kuwa nina nia ya kuomba ridhaa ya chama kuwa KUB. Suala hili linajadiliwa ndani ya chama na mara baada ya taratibu kuwekwa tutajua mwelekeo ni upi.
  3. Nimeomba ridhaa ya chama kuongoza wabunge wenzangu kwa sababu nina uzoefu wa kutosha ndani ya Bunge la Tisa. Tafiti zote zimeonyesha kuwa mimi ni mmoja wa wabunge bora kabisa ndani ya Bunge. Kwa miaka mitano mfululizo nimekuwa polled kama Mbunge Bora kuliko wote. Hii inatokana na michango yangu Bungeni ambayo wananchi wameona kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa sana ufanisi ambao wabunge wa CHADEMA wameonyesha. Nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na kuongoza kamati hiyo kwa umakini mkubwa na kurebisha mwenendo wa Mashirika haya. Fanikio langu kubwa sana na la kujivunia ni lile la kuweza kulirejesha Shirika la STAMICO katika Mashirika ya Umma na kurejesha mali zake zote ikiwemop mgodi wa Buhemba. Serikali ilikuwa imeamua kuua STAMICO kabisa! Nimekuwa pia mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge ambayo mwenyekiti wake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Haya yananipa uzoefu na maarifa ya kuwa Kiongozi bora wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
  4. Ninaamini kuwa Wabunge wengi wa CHADEMA wana uwezo wa kushika nafasi kama hii. Sina shaka hata kidogo na uwezo wa waunge 22 wa CHADEMA. Kwa kuwa uongozi ni ushirikiano, ninaamini kuwa nitaweza kuongoza kwa ubora kabisa Kambi hii na kuweka sura chanya ya CHADEMA mbele ya Umma wa Watanzania iwapo chama kikinipa ridhaa.
  5. Humu kwenye jukwaa hili kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakitunga uwongo wa dhahiri ili kunichafua mbele ya jamii. Ninawaomba wajue kuwa mimi ni mwadilifu sana. Udhaifu wangu mkubwa ni kupenda kusema ninaloliamini bila woga. Nimekuwa hivyo ndani ya Bunge na nimekuwa hivyo ndai ya chama siku zote. Sura ya kwamba mimi nimenunuliwa na CCM inajengwa makusudi na baadhi ya watu ili kunichafua na kunipunguzia heshima mbele ya jamii. Sura hii hujengwa kila ninapotaka kugombea nafasi ya uongozi na muda huo unapoisha shutuma hizo huisha. Naomba yeyote mwenye ushahidi wa jambo lolote aliweke wazi. Mimi sina V8, magari yangu yote second hand ya kununua kwa watu. Sijawahi kumiliku gari mpya. Mie sina nyumba Kimara (MTAKUMBUKA ILIWAHIWA KUSEMWA KUWA NINAISHI MASAKI..........), ninaishi kwenye nyumba ya kupanga NSSF Tabata na pia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mzazi mwenzangu ambaye ni Mwalimu pale Chuo Kikuu. Sio vizuri kwa kweli kunizushia uwongo kwa malengo ya kisiasa. Ninastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa UTU wangu. Kuchafuana hakusaidii kujenga nchi hii.
  6. Nina sababu zote na sifa zote za kuwa KUB. Ninasubiri ridhaa ya chama changu na Wabunge wa chama changu. Tuna ajenda moja kubwa, kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu ujao unafanyika kwa mujibu wa Katiba Mpya na mfumo mpya wa uchaguzi. Hii ndio kazi ya kwanza ambayo KUB anapaswa kuifanya. Kazi hiyo ninaiweza. Sijawahi kusimamia ajenda ikaishia njiani (mfano sheria mpya ya madini). Iwapo changu kikinipa ridhaa nitatoa uongozi uliotukuka, ee Mungu nisaidie.
 
Inawezekana unashabikia tu bila kujua undani wa suala lenyewe ama U-muumini wa Zitto ndio maana ni ngumu kubadili imani yako. Kuna vithibitisho vingi zaidi ya hivyo na hayo niliyowekea REd ni circumstancial evidence kujazia proof za usaliti uliokuwapo. Suala la CHADEMA kutolitolea tamko ilikuwa ni katika kukinusuru chama ukizingatia nguvu ya Zitto aliyokuwa nayo. Na hadi anagombea uenyekiti tayari alikuwa financed na hao mafisadi kiasi cha kwamba uongozi wa CHADEMA hasa mikoani walikuwa wana-msapoti yeye, na kwa sababu kuna watu wa aina yako wasioamini sidhani kama ingekuwa busara kwa chadema kwenda public.

Ukithibisha tuhuma hii, nitajiuzulu Ubunge leo. Ninaomba uweke wazi ushahidi wako.

Pili, ukithibitisha tuhuma yeyote uliyoisema hapa nitajiuzulu ubunge mara baada ya kuweka ushahidi wako. Tuhuma yeyote iliyopo hapa ni propaganda chafu dhidi yangu inayoendeshwa na watu wasio kitakia mema chama chetu. Ninaomba uweke ushahidi wako wazi hapa
 
Back
Top Bottom