Zitto Kabwe awanyima usingizi CHADEMA, viongozi wahaha nchi nzima kuzima moto wa ACT

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, hakika sasa si siri tena kwamba kitendo cha uongozi wa CHADEMA kumfukuza uanachama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kumekigharimu chama.

Mtakumbuka kuwa baada tu ya Tundu Lissu kutangaza kuwa Zitto Kabwe si mwanachama tena wa chadema baada ya Mahakama kufuta kesi aliyoifungua dhidi ya uongozi wake, Zitto Kabwe alitangaza kuachia madaraka ya ubunge na hatimaye kujiunga na ACT ambapo amechaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa chama hicho.

Kitendo hicho cha Zitto kuhamia ACT kilipokelewa kwa dhihaka na makada wa CHADEMA wakidhani kuwa Zitto Kabwe ndo anajimaliza kisiasa. Hata hivyo, baada ya Zitto Kabwe kuhamia ACT na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama hicho, alifanya ziara katika mikoa 10 nchini akiwa na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu Samson Mwigamba. Umati uliofurika kuhudhuria mikutano ya ZITTO umewashtua sana viongozi wa CHADEMA. Kilichowashtua zaidi ni maelfu ya wafuasi wa chadema walioacha chama hicho na kujiunga na ACT.

Hakika Zitto Kabwe amechafua hali ya hewa ya Kinondoni Mtaa wa Ufipa. Sasa viongozi wanaona viti vinawaka moto. Sasa wanaona kuwa chadema inaelekea kwa Buriani. Ni kutokana na amsha amsha ya Zitto Kabwe na mchaka mchaka aliouanza, Viongozi wa CHADEMA hawana namna nyingine zaidi ya kukabiliana naye kwenye majukwaa na njia za siri.

Kwa upande wa majukwaani, Kamati Kuu ya chama hicho imeagiza kuwa viongozi wote wasambae mikoani kuzima moto wa Zitto Kabwe. Haijapata kutokea viongozi wakuu wote wakaikimbia ofisi ya CHADEMA kama ilivyo sasa. Kuanzia Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Manaibu Katibu wakuu wote wanapita maeneo aliyolisha sumu Zitto Kabwe ili kujaribu kutoa maziwa ambayo wanaamini pengine yanaweza kukata sumu hiyo. Lakini wapi.

CHADEMA sasa wanalia na kusaga meno. CHADEMA wanajutia maamuzi waliyofanya. Wataalam wa masuala ya siasa wanaona kuwa nguvu ya Zitto Kabwe katika kushawishi inazidi mara dufu uwezo wa viongozi wote wa UKAWA. Washauri wa CHADEMA akiwemo Saed Kubenea wanaona kuwa Zitto Kabwe akiachwa aendelee atasababisha nguvu ya UKAWA kumezwa na ACT.

Kwamba ACT itageuka kuwa chama kikuu ya Upinzani baada ya uchaguzi wa Oktoba 2015 ambao bila shaka CCM itashinda kwa kishindo. Aidha, jaribio la kumshawishi Zitto Kabwe kujiunga na UKAWA zinaelekea kugonga mwamba hasa baada ya John Mnyika kujichanganya alipotangaza kuwa Zitto Kabwe ni adui namba moja wa CHADEMA.
 
mnahangaika sana....CHADEMA imekuwa kwa wananchi kwa muda mrefu sasa,....Tumefanya operesheni nyingi na tutaendelea kufanya

Huu ni mwaka wa Uchaguzi ...Focus yetu ni CCM

Na lazima mtoke
 
mnahangaika sana....CHADEMA imekuwa kwa wananchi kwa muda mrefu sasa,....Tumefanya operesheni nyingi na tutaendelea kufanya

Huu ni mwaka wa Uchaguzi ...Focus yetu ni CCM

Na lazima mtoke

focus yenu sio ccm kwasasa, ukitaka kuamini cdm hamgombani na ccm mnagombana na act angalia hutuba za viongozi wenu baada ya zito kufukuzwa cdm.

kila mikutano yenu hamuishi kuitaja act tambueni mnaitangaza zaidi mnavyoisema
 
Acha awachachafie tu , walidhani ni rahisi kummaliza ona sasa wanavyohangaika kufuata kufuta nyao zake kila anapokanyaga.
 
Tehetehetehe

Bado siku mbili mkuu mchakato uanze, Ilikuwa Miaka kumi (10), Ikawa miaka michache, ikawa miezi kumi na mbili (12), Zikawa wee na sasa ni siku. Kweli nimekubali kila kitu kina mwisho. Hata Roman Empire ilifikia mwisho. Your days my friend.
 
Fyeka misitu noma; mbowe yupo bukoba aeleweki????????
Vijana wamesema wamechoshwa ;wanataka kijana mwenzao km raisi kikwete alivyosema
zitto ; histori inamuhukumu kuwa ni kijana shupavu ; kaokoa mabilioni ya pesa through pic


kanyaga twende;
operation number 2 ; naije watakimbilia kenya ; kama slaa alivyokimbilia marekani
 
Naona umetimiza wajibu wako Lisbon kumbuka kujenga chama na kuimalika na kuwa taasisi imara sio mchezo,

Pili usiote ndoto ya mchana kweupe kuwa Act inaweza kuwa chama kikuu cha upinzani wauliza TLP hiyo kazi ilivyo ngumu .Tatu Viongozi wa Ukawa kwa pamoja wanajenga na kuamusha ari kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu kama alivyofanya Zzk kutangaza Act,

Kamwe Act haiwezi kuwa tishio kwa chadema fanya tafiti vzr sio kukurupuka bure.
 
Kwa hiyo katika maandishi yako uliyoweka hapa tishio la Zitto kwa CHADEMA ni nini? Mbona sioni hata hoja yenyewe inayohusu tishio la Zitto kwa CHADEMA? Zitto amefanya kitu gani huko alikopita ambacho kimewapa pressure CHADEMA? Kama ni viongozi wa CHADEMA kutoka ofisini na kuwa field, huo ndiyo utaratibu wa siku zote wa chama chetu. Sasa kinachokupa pressure wewe ni nini?

Ukitaka kujua kwamba CHADEMA haijatikisika, fanya tu ulinganifu wa idadi ya watu ambao Zitto alikuwa anakusanya baada ya uhamasishaji wa muda mrefu, na ile ambayo CHADEMA hivi sasa wanakusanya pasipo hata kuhamasisha watu kuhudhuria mikutano?

Fahamu jambo moja katika siasa, kwamba kuna wakati mwingine watu wanahudhuria mikutano kwa ajili tu ya kwenda kumfahamu huyo msaliti wa demokrasia anayesemwa kila upande wa nchi. Si lazima waende kwa ajili ya kumuunga mkono? Mbona hatuoni akisimamisha watu majukwaani wanaorudisha kadi za CHADEMA?

Mwambie Zitto amalize kwanza matatizo yake na viongozi wenzake ndani ya ACT. Na akirudishe chama cha ACT-Tanzania alichokipora kutoka kwa akina Limbu na kukibatiza jina la ACT- Wazalendo.
 
Fyeka misitu noma; mbowe yupo bukoba aeleweki????????
Vijana wamesema wamechoshwa ;wanataka kijana mwenzao km raisi kikwete alivyosema
zitto ; histori inamuhukumu kuwa ni kijana shupavu ; kaokoa mabilioni ya pesa through pic


kanyaga twende;
operation number 2 ; naije watakimbilia kenya ; kama slaa alivyokimbilia marekani
Zitto mtu mmoja anawapeleka puta Viongozi wote wa CHADEMA.
 
focus yenu sio ccm kwasasa, ukitaka kuamini cdm hamgombani na ccm mnagombana na act angalia hutuba za viongozi wenu baada ya zito kufukuzwa cdm.

kila mikutano yenu hamuishi kuitaja act tambueni mnaitangaza zaidi mnavyoisema

unatamani iwe hivyo lakini haiko hivyo na haitakuwa hivyo
 
Chadema wanataka kuwaonyesha act na ccm kuwa sio ya mtu mmoja kila kiongozi na mbunge wa chadema ni lulu kumtoa shibuda,letisia nyerere na huyo kibaraka zitto.
 
Back
Top Bottom