Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amesema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho.

Anasema Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge. Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.

=========
ndugai zitto.jpg

Leo Ijumaa Januari 31, 2020 bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wanamsubiri Zitto awaeleze kwa nini aliandika barua hiyo.

“Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.”

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai.

Katika kusisitiza hilo, Spika Ndugai amesema, “ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”

Hata hivyo hapo jana Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Joseph Kakunda alisema kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuandika barua ya kutaka kuzuia mkopo wa elimu unaotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni kituko nani aibu.

Kakunda aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa za kamati za Bunge za bajeti na Uwekezaji na Mitaji ya Umma.

“Naomba nizungumze masikitiko yangu dhidi ya barua moja ambayo mwenzetu mmoja (Zitto) ameiandika kutaka kuzuia fedha za miradi ya elimu ni kituko na ni aibu sana kwetu sisi wabunge kuona mwenzetu ameandika barua,” alisema Kakunda ambaye pia ni Mbunge wa Sikonge (CCM) mkoani Tabora

Alisema barua hiyo wangekuwa wameandika watu wa mashirika yasiyo ya kiserikali yeye asingestuka sana lakini kuandikwa na mbunge mwenzao wakati Serikali imepeleka Sh1 bilioni kwa ajili ya kukarabati Sekondari ya Kigoma iliyoko kwenye jimbo lake ni jambo la kusikitisha.

“Sasa hivi Sekondari ya Kigoma ni kama mpya. Na vilevile Serikali imepeleka zaidi ya Sh4 bilioni kwa ajili ya kuboresha elimu. Sasa anazuia zisije kwa haraka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kitanzania nieleze masikitiko makubwa sana,”amesema.

“Nilitamani nipaze sauti huko aliko anisikie lakini kwa sababu yuko mbali naachia hapo lakini atasikia kutoka kwenye Hansard (kumbukumbu Rasmi za Bunge)" alisema Mh. Kakunda
 
Akasema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho. Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge.

Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.
Kwa bunge lipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akasema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho. Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge.

Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.
Nani angemsikiliza? Sana sana angezomewa na wagonga meza. Kwani ni mikataba mingapi ya hovyo imepitishwa pale bungeni? Wapinzani wakipinga na kutaka maboresho wanazomewa na kutolewa nje. Leo hii supika ndiyo anasema angemsilikiliza Zitto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom