Zitto aweka pingamizi Mahakamani kuzuia Kikao cha Kamati Kuu kujadili rufaa yake kesho

Status
Not open for further replies.
Ni kweli kuwa ZITTO anaonekana anajifanya ni zaidi ya CDM lakini ukweli ni kwamba ZITTO ni mwanasiasa mkubwa, kwa mfumo wa siasa za chadema anakuwa kama kontena kubebwa na vitz. ZITTO anatakiwa awe kwenye chama kikubwa au akibadilishe CDM kiwe kikubwa na viongozi mbumbumbu kama MBOWE, MSIGWA na SLAA ambao hata elimu zao hazieleweki wakae pembeni. Majembe kama Prof. BAREGU, Dkt. MKUMBO, Prof. SAFARI, advocate MARANDO na wengne washke chama. Hakuna atakaekuwa na wazo kuwa anasalitiwa. Woga wa MBOWE na vilaza wenzake ndo unaleta mambo ya kuona KABWE ni zaidi ya chama.

Umenena mkuu
 
zitto zuberi kabwe kiukweli aeleweki anataka nini ndani ya chadema na siasa kwa ujumla anaongea mengi sana na akiwa huko kigoma aliongea mengi sana kuhusu viongozi wake wakuu wa chama sasa huko mahakamani amefuata nini

Mkuu zitto anaeleweka mkuu, msome vuta nkuvute.
 
NB: Na katika kazi za Kamati Kuu, hakuna kazi au majukumu ya kuwasimamisha viongozi uongozi wao.

Kawadanganye hao hao buku saba unusu wenzako, katiba ya Chadema hujaisoma, na kama umeisoma hujaielewa ndiyo maana unakurupuka tu kuandika utumbo.

7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisha
ripoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.
(b) Kuteua Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu
(c) Kuteua Makatibu wa Wilaya na Mikoa
(d) Kuthibitisha uteuzi wa Sekretarieti za Wilaya.
(e) Kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu juu ya rufaa za uchaguzi na kinidhamu.
(f) Kuandaa na kutoa Mapendekezo kwa Baraza Kuu, Mikakati ya kuendesha shughuli
za Chama kwa kila mwaka na kwa kipindi cha miaka mitano.
(g) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa baraza Kuu , Mikakati ya kupata mahitaji ya
raslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali.
(h) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Baraza kuu ratiba na maelekezo ya uchaguzi wa
kichama.
(i) Kupitia na kutoa kwa Baraza Kuu mapendekezo ya haja ya kuzifanyia marekebisho
au maboresho Kanuni za Chama ama Katiba ya Chama.
(j) Kujadili taarifa za Sekretarieti ya Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa
utekelezaji.
(k) Kusimamia utendaji kazi wa Sekretarieti ya Kamati Kuu
(l) Kufanya mapitio ya Sera za Chama na kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu kwa
kuzingatia matokeo ya Utafiti uliofanywa na Sekretarieti ya Kamati Kuu.
(m) Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza Kuu na Mkutano
Mkuu.
(n) Kuwa kiungo na kudumisha mahusiano mema kati ya Chama na vyama vingine vya
siasa nchini, Afrika Mashariki na nchi nyingine.
(o) Kuthibitisha ajira za watumishi wakuu wa Chama ngazi ya Taifa.
(p) Kuteua kamati au tume za kushughulikia masuala maalum ya kichama kwa muda
maalumu.
(q) Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama kwa kila mwaka
(r) Kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge na Baraza la wawakilishi
Zanzibar
(s) Kuandaa agenda za Baraza Kuu na Mapendekezo ya agenda za Mkutano Mkuu.
(t) Kufanya uamuzi juu ya mpendekezo ya kufukuza Mwanachama.
(u) Kuandaa hoja za kupelekwa Bungeni na Wabunge wa Chama
(v) Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na
katiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.
(w) Kuratibu utendaji wa ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar.
(x) Kusimamia utendaji kazi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.
(y) Kuteua wajumbe maalum wawili kuingia Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya.
 
Embu Tuone Scenarios zilivyo,
Ikitokea ZZK akashinda kesi ya Pingamizi na kuweza kuzuia ajenda namba 2 Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao. Kesi hii itapelekwa kwenye Baraza kuu na ZZK atakuwa na nafasi nzuri ya kushinda Rufaa yake ndani ya Baraza Kuu na Baraza kuu litakuwa na uwezo wa kutengua maamuzi yote ya KK tusishangae kuona kuwa ZZK anarudishiwa vyeo vyake vyote na in long run Mh. Mbowe Uenyekiti wake unawekwa Rehani.

Na ikitokea Mahakama ikakataa hoja za Mh. ZZK hii ina maana kuwa Ajenda namba 2 itwakilishwa na kujadiliwa na KK. Na kutokana na hatua ya ZZK kwenda mahakamani wajumbe wa KK watakuwa na hasira zaidi kiasi cha Kumpiga kura hata ya kumvua ZZK uanachama wake. ZZK atakuwa kwenye wakati mgumu zaidi.

Umeongea point,lakini sidhani kama mahakama wanaweza kuwa wajinga kiasi hicho suala liko wazi mkuu
 
Nashangaa sana kuona ZZK,kuzidi kujipalia kaa la moto...bas ndg endeleza sinema ili pia siku zako ndani ya chama zisogee sogee,ila kwa ujumla nafsi za wanachama zishatoka kwako,tuachie chama chetu.
 
Mbona hamuandiki kilichoamuliwa mahakamani? au mpaka sasa mahakama inaendelea?

Mie nasikia kikao cha kesho jaji kakipiga stop ili kupatikane time ya kutosha ya kusikiliza malalamiko, na kimesimamishwa sasa mbona hamsemi?

Yericko Nyerere kaamua kukaa kimya.. Alijigamba yupo mahakaman
 
Last edited by a moderator:
Vijana wengi wenye upeo wa kuona mbali, wameamua kuachana na CHADEMA sababu ya fitina na umbumbumbu wa viongozi wa CHADEMA.

Vijana wenye upeo ndo akina nani?.....wakina msalani au?kweli nchi hii ni moja ya kivutio tosha ambacho chatakiwa kuwa miongoni mwa seven wonders of the world......wasomi wasaliti?jitoweni mapema na shut up ur mouth.......
 
kwa sasa anasubiriwa jaji utamwa kutua maaamuzi, hii ni baada ya kupokea hoja za kila upande na kupata wasaa wakuzipitia,


chadema shangilieniiiiiii kirusi kinatibiwa

wewe ni wa kuonea huruma tuu hadi uli amua kuiba jina la kina nyerere
 
Nashangaa sana kuona ZZK,kuzidi kujipalia kaa la moto...bas ndg endeleza sinema ili pia siku zako ndani ya chama zisogee sogee,ila kwa ujumla nafsi za wanachama zishatoka kwako,tuachie chama chetu.


Watu wengibe bwana, wewe nani? Eti Chama chenu! Kwani yeye hana haki wewe ndo mwenye hali huko?
 
Walioko mahakamani mbona hawasemi kuwa mahakama wamepiga stop kikao cha kk kesho?? Au wanafikiri kukaa kimya kutabadili maamuzi
 
Mbona hamuandiki kilichoamuliwa mahakamani? au mpaka sasa mahakama inaendelea?

Mie nasikia kikao cha kesho jaji kakipiga stop ili kupatikane time ya kutosha ya kusikiliza malalamiko, na kimesimamishwa sasa mbona hamsemi?

kama unachosema hapo juu ndiyo kweli ni verdict ya presiding judge, ina maana mahakama haikuzingatia haki ya mlalamikiwa kuwa endapo mlalamikaji tayari alikwishapewa taarifa muda mrefu kwa nini alete pingamizi saa chache kabla ya kikao?

je, mahakama haioni kuwa hii si kutafuta haki kwa mlalamikaji bali ni kutaka tu kumhujumu mlalamikiwa?

mimi ni layman kwenye sheria....nifundisheni wajuzi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom