Zitto aweka pingamizi Mahakamani kuzuia Kikao cha Kamati Kuu kujadili rufaa yake kesho

Status
Not open for further replies.
Heheee kifo chake kisiasa ni kibaya sana,

Kwake kila kitu kigumu, maji moto, mboga mto, ugali moto,

Hahaa moja haikai, mbili haikai na hata free haikai,
 
Hivi si alisema anajiamini, kuwa anapendwa? Sasa si aache chama kiamue na akubaliane na maamuzi ya chama? ZZK atamwongoza nani, wakati hawamtaki?

Anafata nyayo za Rashi na Kafulila! Wako wapi leo?


Siamini kama ZZK anaweza kuwa na uelewa mdogo kiasi hicho. Nilidhani angejitetea kwanza na uamuzi ukitolewa angekwenda Mahakamani kupinga adhabu aliyopewa.

Kuzuia Kikao maana yake nini? Kama ana wafuasi wengi kwa nini ang'ang'anie CHADEMA? Si ajotoe na kwenda wanakomuhitaji au kule ambako watamruhusu afanye atakalo hasa kuitisha vikao bila idhini ya Chama tena nje ya Jimbo lake!

Sijui kama kuna Chama cha namna hiyo! Vinginevyo tuamini kwamba yupo kazini kwa manufaa yake binafsi.
 
Huyu si asubuhi kasema yuko tayari kwa maanuzi ya chama sasa imekuaje tena mbona huyu jamaa wenge sana!!!
 
Huyu dogo zumbukuku kweli,kwa kusikia tu yeye tayari mahakamani ...haya yote tulishayajua na kwanzia leo ajitambue yeye ni mbunge wa mahakama tu,CDM si mamaake wala shangazi yake
 
Wana Jf,

Taarifa ambazo zimenifikia hivi punde ni kuwa Zitto Kabwe ameweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha Kamati Kuu kesho.

Wanasheria wa Chama wakiongozwa na Tundu Lissu wanaenda Mahakamani kusikiliza pingamizi hilo ambalo litakuwa limeenda kwa hati ya dharura.

Nitawaletea kinachoendelea.

Ithangaledi

...ameenda kupinga nini wakati hajui matokeo ya kikao..? kama ni kikao halali si asubiri maamuzi ya kikao ndo apinge hukumu ya kikao dhidi yake..? sasa anataka kuzuia kikao ili chama kisifanye kazi zake..? na kwakufanya hivyo amejihukumu kuwa atafukuzwa so anajaribu ku buy time ili aingie bunge la katiba, st...pid boy....
 
Zitto si mjinga kama ninyi.
Yani aweke pingamizi kuzuia kikao kinacho sikiliza utetezi wake ulio jaa weledi?

Acheni ujinga wa kutunga story zisizo na maana yeyote.
Kwa hiyo aweke pingamizi alaf utetezi wake usikilizwe na nani?

Mna hangaika kufanyan lolote ili zitto aonekane mbaya lakini mnashindwa.

Naona msemaji wenu kawaumbua nyie watunzi.

Kwa utetezi wa zitto lazima ashinde labda mfanye hira nyie wenye chama na tunajua mlisha zunguka kwenye mikutano na kutangaza maamuzi ya kamati kuu.

We kweli hujielewi, eti kwa utetez wa zito lazima ashinde, we umeuona huo utetezi au uko kazin kwa ujira wa 7000?![/QUOTE]

Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia 100,ila naomba niongezee tu kidogo kwamba watu wa JF na wananchi kwa ujumla ambao hawamjui ZZK ndio wanaoongea sana vtu vya uongo dhidi yake,ila kwa wale wanaomfahamu,wanajua kuwa jamaa si mtu wa kukurupuka kabisa,ni mtu anayejipanga kwa kutumia akili sana pengine kuliko viongozi wote vijana hapa nchini.
Na ni mmoja wa viongozi vijana wachache sana anayeweza kujenga hoja na kuitetea hoja yake vizuri sana,sasa itakuwa jambo la ajabu sana kwa mtu kaka yeye ZZK eti kwenda mahakamani kuweka pingamizi la kikao cha CC ya CDM.Ni watu wenye matatizo ya akili tu ndio wanaoweza amini kitu cha namna hii.
 
hivi si alisema anajiamini, kuwa anapendwa? Sasa si aache chama kiamue na akubaliane na maamuzi ya chama? Zzk atamwongoza nani, wakati hawamtaki?

Anafata nyayo za rashi na kafulila! Wako wapi leo?

mafuta. Ya mawese y anaathari gani kwenye. Mfumo wa akili????
 
Taarifa sahihi Tupeane jamani kama wamefika mahakamani na maamuzi ya mahakama yamekuwaje?
 
Amrpewa ushsuri na CCM huyo!

Kumbe asubuhi wakati anaongea kupitia CHANEL 10 alikuwa anatuzuga tu pale aliposema anasuburi hatima yake baada ya kikao cha kamati kuu!
 
Mbona hii taarifa inagoma kutua akilini mwangu, inabaki ikielea elea hewani!! Kwa jinsi ilivyokuwa reported, inamaanisha anakwenda kuzuia chama kuendelea na shughuli zake....
eh!! Huyu jamaa sasa atakuwa amepinduka akili.
 
Mtu yeyote anayepingana na mpango wa Mungu basi Mungu umtia pofu. Ndicho kinachomtokea Zitto sasa hivi.

Wamiliki wa magazeti wajiandae kwa biashara nzuri ya magazeti jumamosi.
Mungu yupi kamanda?
 
Kipenga cha raund ya pili ndio kimepulizwa, bado Zitto anaitingisha chadema. Nliwahi kuwaambia hapa Zitto kawazidi uwezo viongozi wa chadema, pia hili ni somo kwa watu wote kuwa huwezi ku ignore mtu aliesoma hata siku moja, at one point, somewhere utagundua umuhimu wake.

Amekuwa gamba au mizigo? Ile ndo imeshindikana. Huyu ni mweupe mno! Kama jirani yake alitembea na magoti kuomba msamaha NCCR, sembuse CDM?
 
Kama ni kweli,ZITTO hatufai kwenye chama. Najiuliza anapata wapi ujasiri wa kuzuia kamati kuu wakati anajua kwamba maamuzi ya hatma yake na utetezi wake ndio utakaotolewa maamuzi.


Sasa anaweka pingamizi mahakamani kufanyika kwa kikao cha kamati kuu ili iweje??? Hatma ya jambo hili litamalizikaje????


Mimi nadhani angeweka pingamizi mahakamani baada ya maamuzi kufanyika na si kabla. Mfano,kama maamuzi yamefanyika kwamba avuliwe uanachama wake ndio angekwenda mahakamani kupinga kama anaona kaonewa.

ZITTO hakitakii mema CHADEMA, Tumpuuze.

nikweli mzee umenena, m2 huyu hatufai hata kidogo, lazima atakuwa anatumika kuiaribia chadema, lakini tupo imara zaidi ya maccm yanavyo dhani.
 
Viongozi wengi wa CHADEMA wana kesi mahakamani, nyingi ni za kubambikwa na vyombo vya dola kwa maelekezo ya CCM. Sina kumbukumbu kama Mh ZZK alishawahi kuwa na kesi kama wenzake; mf Lema,Mbowe,Slaa,Msigwa,Mbilinyi,Lissu,Kileo na wengine hata wa ngazi za chini pamoja na wanachama wa kawaida.

Wote uliowataja hapo ukitoa babu wa gongo wengne kichwan Ziro,ndo maana wanapelekagwa mahakan coz hata hoja ya msing wao hua wanaenda kichwa kichwa nao mapoliccm yapo kichwa kichwa pia ndo yanawadunda hao wavuta gongo na bangi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom