- Thread starter
- #61
Wakati wanaingia mikataba, wameingia kimya kimya na kila mtu kivyake....mbona wanataka kutoka kwa kelele na kama kundi? Hii press release ina nguvu gani ya kisheria hasa ukizingatia uwepo wa mikataba...isije ikawa ni kupoteza muda na rasilimali (hasa kama watakubali kutumika kwa manufaa ya wanasiasa bila kuwa makini na kuwa na uhakika wa kile wanachikipigania).
Mikataba yao inasemaje kuhusiana na kuvunja/kuvunjika? Kwa kuwa muziki ni biashara, je suala hili wanamuziki linaendana vipi na sheria ya ushindani wa kibiashara (The Fair Competition Act, 2003)? Ni vema wasanii wakawa makini katika masuala haya yahusuyo mikataba ambayo inaweza ku-back fire kwa individual musicians na sio kwa group (maana sio group la hao wanamuziki 153 lilioingia mkataba na makampuni ya simu)
Well said. Wasijekuwa wamekurupuka kuvunja mkataba na makampuni ya simu bila kuzingatia legal issues zinawabanaje kwenye huo mkataba wa kinyonyaji. Kuingia mkataba ni kitu kimoja na kuvunja mkataba ni kitu kingine, one party must suffer the consequences of breaching the contract, in our case, the artists.