Zitto asikitika wanaombeza Nape

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
By.
Zitto Kabwe: Kwenye siasa ya nchi Kama zetu busara ya mapambano ni Jambo la msingi sana. Kama Nape wa CCM anaunga mkono hoja ya upinzani kuhusu posho, asibezwe wala kuzodolewa.

Anapaswa kuungwa mono ili kuongeza Jeshi na kumkinga dhidi ya wapenda posho ndani ya chama chake. Akibezwa, siku nyingine Batak ga mono Jambo hata Kama ni jema kwa nchi.

Hii ndio huitwa hekima za harakati. Nimesikitishwa sana na wanaobeza kauli ya Nape kuhusu posho za Wabunge
 
wasioelewa siasa ndo watakaombeza nape, lakini mpevu yeyote wa siasa (kama mimi) hawezi kumbeza nape hata kidogo, kwani nape anastahili kupongezwa yeye na chama chake kwa kuuuonesha umma wa watanzania juu ya msimamo wa chama hicho cha kijani na njano....!!
 
Zitto mambo ya CCM hayakuhusu kaimarishe cdm yako na endelea kuibomoa NCCR
 
Pale neno harakati linapokosa maana, na neno UFANISI likachanganywa na kupata maana sawa na neno UFISADI kisha fikra pevu ikawa kupinga kila kitu huku walio wengi (hasa VIJANA) wakiona njia pekee ya kuungwa mkono ni kudandia ubishi pasipo kubangua bongo zao kufiri BASI ujue kama ni vita ya ukombozi wa nchi inabidi urudi nyuma kuanza na ukombozi wa fikra za wananchi. Omutwale Kanyigo
 
wasioelewa siasa ndo watakaombeza nape, lakini mpevu yeyote wa siasa (kama mimi) hawezi kumbeza nape hata kidogo, kwani nape anastahili kupongezwa yeye na chama chake kwa kuuuonesha umma wa watanzania juu ya msimamo wa chama hicho cha kijani na njano....!!

Mawaziri wa ccm na wabunge wa ccm ambao miongoni mwao ni wajumbe wa NEC na Kamati kuu wamekuwa wakitetea kwa nguvu zote suala la nyongeza ya posho. Si leo tu, tangu mkutano wa bajeti uliokwisha walisimama kidete posho, na sasa wameamua kuziongeza.

Kitendo cha nape kujitokeza kusema ccm inapinga ongezeko la posho ni baada ya kuona wananchi wa kila aina na kutoka kila kona wanapiga kelele za kutaka wabunge wasiongezewe posho, wanataka zifutwe. Katika mtiririko huo huo wa kupinga posho wafanyakazi nao walikuwa wanajiandaa kuishinikiza serikali iwaongezee kipato, nadhani ulimsikia mgaya wa tucta, na usisahau kwamba tayari chama cha walimu kilishasema sasa basi.

Kwahiyo nape hajaongea kupinga posho kwa kuwa inamtoka moyoni bali amefanya hivyo shingo upande kwa kuogopa shinikizo za wananchi wa makundi mbalimbali. Sasa anastahili kupongezwa kwa lipi? na kwa kipi?
 
Naungana na Zito kuhusu kauli ya Nape juu ya kukataza kuongezwa posho za wabunge si za kubezwa hata kidogo. Zito keep on going..... Nape keep on going....... achaneni na hawa wapumbavu wanaoponda kila kitu.
 
once again, namuunga mkono zitto ingawa mie humbeza nape, maana kwa mwanasiasa kila kauli anayotoa, changanya na vyako na ujue aliitolea wapi

akimaliza hapo ataisikitikia kafu

wanasema usitukane wakunga na uzazi ungalipo
 
Kwani huo ni msimamo wa Nape au CCM? Nape amewakilisha tu maoni na msimamo wa chama baada ya kupima upepo.

Kama yeye Zitto anaona msimamo huo wa CCM ni halisi hauna bendera fuata upepo basi aisifu CCM na si Nape, maana Nape ni mtoa ujumbe tu.
 
By.
Zitto Kabwe: Kwenye siasa ya nchi Kama zetu busara ya mapambano ni Jambo la msingi sana. Kama Nape wa CCM anaunga mkono hoja ya upinzani kuhusu posho, asibezwe wala kuzodolewa. Anapaswa kuungwa mono ili kuongeza Jeshi na kumkinga dhidi ya wapenda posho ndani ya chama chake. Akibezwa, siku nyingine Batak ga mono Jambo hata Kama ni jema kwa nchi. Hii ndio huitwa hekima za harakati. Nimesikitishwa sana na wanaobeza kauli ya Nape kuhusu posho za Wabunge

Kwani tunatakiwa kumbembeleza Nape aunge mkono hoja za upinzani au zenye mantiki kwa Taifa letu? Huo ni wajibu wake kama kiongozi, kama haoni hilo hatupaswi kumbembeleza na kumbebabeba aunge mkono hoja za kitaifa!
 
Yahitajika akili ya tatu kuliona hili:
Haiwezekani katibu wa bunge aseme posho haijaongezwa ni uzushi tu wa vyombo vya habari kutaka kuwagombanisha wabunge na wapiga kura wao! siku moja baadaye SUPIKA anasema posho zimeongezwa sababu ya ugumu wa maisha! siku nne baadaye Nepi anasema chama kinapinga! Duuh! kweli sisi mazuzu tunabaki kucheka tu! Yani asibezwe Nepi kwa nini? Serikali iliyopo madarakani ni yake na inajua usanii inaowafanyia wana wa nchi hii kwa kutumia chama cha majoka! Ni usanii tu huu!! yani " ng'ata hapa puliza pale" ndiyo mtindo wao huo! ebu tuamkeni jamani tuache kuchekacheka kama mazuzu!
 
Sasa mnambeza kwanini?.... yeye anachukua posho kwani.
Acheni siasa za maji taka wapuuzi nyie!
Kudos! Zitto and Nape.
But Zitto, stay away from our land, let Sita handle that, the old man knows Kenyans very well, he spent his youth working there.
 
bi kiroboto sijui alipata wapi nguvu ya kulianzisha. Au kuna kifungu kinampa nguvu hiyo?
 
Zitto,

Ningependa Ujue hapa Hakuna anayembeza Nape.

Sisi kama jamii ya wasomi, Lazima Tuangalie Mambo from all Directions.

Wote tunajua Nape katumwa na CCM. Wote tunajua asilimia kubwa ya Wabunge ni CCM na hawa wabunge ndio vinara wa kutetea hii Posho.

Leo uje utuambie CCM inapinga Posho? Big No. Ukiniambia hiyo ni Kauli ya Nape Hapo nitamuunga mkono.

Mimi nimekosa Imani na Misimamo ya CCM tangu ulipoanza msemo wa ''Kuvua gamba'' This is just a very interesting comedy.
 
By.
Zitto Kabwe: Kwenye siasa ya nchi Kama zetu busara ya mapambano ni Jambo la msingi sana. Kama Nape wa CCM anaunga mkono hoja ya upinzani kuhusu posho, asibezwe wala kuzodolewa. Anapaswa kuungwa mono ili kuongeza Jeshi na kumkinga dhidi ya wapenda posho ndani ya chama chake. Akibezwa, siku nyingine Batak ga mono Jambo hata Kama ni jema kwa nchi. Hii ndio huitwa hekima za harakati. Nimesikitishwa sana na wanaobeza kauli ya Nape kuhusu posho za Wabunge

Yaani bado kuna watu wanaona Kauli ya Nape inatoka moyoni! kweli wa-Danganyika bado tunasafari ndefu ya kujua mbivu na mbichi. CCM wanachofanya ni kuwachanganya wananchi kuhusu wanachokisimimamia. Tukumbuke hata wakati wa malipo ya Dowans, serikali inataka ilipe huku Nape anasema malipo si halali!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Yaani bado kuna watu wanaona Kauli ya Nape inatoka moyoni! kweli wa-Danganyika bado tunasafari ndefu ya kujua mbivu na mbichi. CCM wanachofanya ni kuwachanganya wananchi kuhusu wanachokisimimamia. Tukumbuke hata wakati wa malipo ya Dowans, serikali inataka ilipe huku Nape anasema malipo si halali!

Katika binadamu, (mimi na wewe) nani amewahi kuyajua ya moyoni kwa mwenziwe? Sote twajadilia kitokacho kinywani! Tuhukumu kauli iliyotoka kinywani na si Roho ya Nape.
 
Zitto unanishangaza! Nadhani haujamsoma nini kilichomsukuma nape (ccm) kupinga posho. Yeye na ccm wana woga unawasumbua, kwamba sehemu kubwa ya umma yapinga posho. Wanacheza siasa. Lakini kwanini unaamini wana dhamira safi na kukerwa na hili. Kumbuka walivyoliteka suala la richmond - wakaishia kumlinda mkubwa wao! Ufisadi wa epa, ni hadithi, sukari, ndo kwanza yapanda, wakavamia issue ya petrol, nayo bei yapanda kwa mtindo wa homa za vipindi, katiba wameliteka kwa hiyo jk anatuandikia, kupanda kwa maisha na mfumuko wa bei wakaishia kukoroma na sasa kimya. Name any serious issue. Wameipora kwa kuonesha wana uchungu nayo kisha wanazima kisanii. Nape huyu aliyeikana id yake jamii forums anaaminika? Nape huyu aliyelivalia njuga na kuapa mafisadi kushughulikiwa kwa kuwavua magamba, lakini sasa kimya anaaminika? Na wasiwasi dhamira yako pia. Huyu c mpiganaji ktk kambi yako ya kupinga posho. Angekuwa makamba junior ningekubali. Angalau kwa vitendo kasimamia msimamo wake!
 
Back
Top Bottom