Zitto apendekeza Dowans itaifishwe; Serikali yapinga! Mgao waendelea...

Hii ndio gharama ya umaskini wa akili na utajiri wa mali ya kifisadi.Hakuna maelezo ya kueleweka kuhusu nishati hii. Hili tatizo limeanza wakati wa awamu ya pili mpaka leo. Je mipango ya Muda mrefu ya serikali iko wapi toka wakati huo?

Kila siku mipango ni ya muda mfupi tu au viongozi wetu hawa wanatarajia kuishi muda mfupi na hivyo kujali tu kipindi watakachoishi? Ufisadi! mmm kimya wasisikie
 
du kazi kweli safari tunayo nayo ni ndefu,jamani ZITTTO hivi umeona IPTL sijui na DOWANS ndo suluhisho?jamani tununue mitambo mipya na tuanze programs za kufikiria njia za kumaliza kabisa tatizo la umeme.tufikirie vyanzo vingine vya umeme na sio maji tu na majenereta.Jamani kuna Geotherms,nukilia sijui na makaa ya mawe jamani wanageologia mko wapi sasa tunahitaji utaalaam na sio porojo hizi za kisiasa

Tatizo kubwa ni kutokusikilizwa na kutothamini michango na mawazo ya wataalamu wa nchi yetu. Siasa zimetawala kuliko utekelezaji. Geothermal energy is a long term process ambayo itachukua muda kutake off. Je tuendelee kukaa gizani
 
Haya mambo ya kutaifisha kwenye ulimwengu wa sasa wa good governance hayana nafasi. If anything yata tuingiza katika migogoro ya kimahakama na hatimae ni kushindwa kesi na hasara kubwa zaidi ( refer IPTL na City water kesi )

Talk about mikataba ya kifasadi, hivi IPTL leo ni wasafi hivyo? kweli watanzania wepesi kusahau.

Hoja ya msingi ni ya rafiki yangu Waberoya, acha siasa pembeni taifa lipo kwenye kiza tunafanya nini? Hii habari ya mitambo hii ya kifisadi sijui sheria ya manunuzi and all that rubbish tunaangamia jamani we.

Walau sasa wengi tunakubaliana kuwa nchi ipo kwenye crisis inayo fanana na vita. Kama ni hivyo lets act now badala ya kuanza kutafutana mchawi nunua Dowans, nunua IPTL washa umeme halafu tukutane Dodoma tuanze kulumbana nani kala 10% nani kafanya nini lakini viwanda, mahospital, mashule nk yanapata umeme.

Masatu,
Nchi za kawaida ni kuwa Wahusika waliochangia kutufikisha hapo inabidi kuwasimamisha ukutani na kuwafunga vitambaa vyeusi........

Kwani Dowans ina mwenyewe? Si mwenyewe hadi leo "eti" hajulikani? Sasa tukifilisi, tutadaiwa na nani? Mwisho kuna hela zetu nyingi tu tunawadai na sidhani kama wamelipia eneo ilipo mitambo hiyo tangu izimwe...... Kuna sababu nyingi tu ya kuitaifisha. Wanaitwa mahakamani na wasipofika, hukumu inatolewa. Wakifika mnawakamata kwa UFISADI......
 
Mkuu Zitto Kabwe heshima mbele.

Napenda kuchukua nafasi hii kukupa pongezi kutoka chini ya uvungu wa moyo wangu.Nimesoma hotuba yako fupi lakini yenye kutoa majibu ya muda mfupi ya tatizo la umeme hapa nchini.Nimesema ya muda mfupi si kwa bahati mbaya bali kwa mujibu wa ripoti ya waziri na wataalamu wa TANESCO matumizi ya umeme yanaongezeka kwa kasi kubwa hivyo kutegemea umeme wa maji na mitambo ya IPTL pekee yake hakutotufikisha mbali.

Zitto umenifurahisha sana kwa kuishauri serekali itaifishe mitambo ya Dowans.Muungwana na timu yake yote ya uongozi najua wamekusikia nategemea watachukua hatua kwa haraka bila kujali nani katoa ushauri.

Kuhusu IPTL ushauri wako pia si mbaya lakini naomba kutoa angalizo hasa kwa wanasheria,je serekali ikifuata ushauri wa Mheshimiwa Zitto hakuna madhara ya kisheria yanaweza kuja kuigharimu serekali katika hukumu.
 
Mkuu heshima mbele,
Hivi wewe unaelewaje haya maneno EMERGENCY or CRISIS?
Hiyo mitambo mipya unayoongelea itakuja baada ya siku moja au wiki moja??? Jamani hivi tunaelewa sasa tuko kwenye hali mbaya sana kutokana na kukosa umeme. Sio wakati wa kusubiri plan ni wakati wa kufanya maamuzi ya haraka na machungu basi.
This is what we call state of emergency...
heheheh Emergence kwani umeme mgawo umeanza mwaka huu?
 
Tatizo Kamati ya madini haikuwa inatoa proposal. ilikuwa inapinga tu...mara ya kwanza zitto alikuja na proposal kuwa mitambo inunuliwe....ikapingwa bila kutoa pendekezo mbadala....leo kaja na pendekezo tutaifishe....akina mwakyembe wako wapi?

That is where the proble is. Na ndo tulikofikia kwa kuwa hawakuja na solutions.

Haya mambo ya kutaifisha kwenye ulimwengu wa sasa wa good governance hayana nafasi. If anything yata tuingiza katika migogoro ya kimahakama na hatimae ni kushindwa kesi na hasara kubwa zaidi ( refer IPTL na City water kesi )

Talk about mikataba ya kifasadi, hivi IPTL leo ni wasafi hivyo? kweli watanzania wepesi kusahau.

Hoja ya msingi ni ya rafiki yangu Waberoya, acha siasa pembeni taifa lipo kwenye kiza tunafanya nini? Hii habari ya mitambo hii ya kifisadi sijui sheria ya manunuzi and all that rubbish tunaangamia jamani we..

Mkuu kama sikosei kwenye kesi ya City water tulishinda.
Zaidi ya hayo tunaposema tunataifisha si tunafanya tu hivyo kwa kuwa tumetaka kufanya hivyo. Kuna-grounds nyingi sana ambazo ziko wazi na hatutakuwa na tatizo. Hii ilishajadiliwa huko nyuma... vitu kama breach of contract terms by dowans, dealing with un-existing company etc etc ambavyo hata wanasheria wa JF walikubaliana kimsingi. So kuna grounds za hilo la kutaifisha.
 
suluhu aliyoitoa zitto kuhusu mgao wa umeme mi naona ni ya muda tu..kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyika! kwani kabla ya mgao si dowans na IPTL ilikua haifanyi kazi? then mitambo ya umeme imeharibika ndo maana tukapata huo upungufu wa 90MW. Kama critical issues hazitafanyiwa kazi hata akichukua hiyo Dowans na IPTL ifnaye kazi halafu baada ya muda ikaharibika then tatizo litabaki palepale. Ishu ni serikali kujipanga na kutafuta suluhu muhimu ni kimaanisha utendaji wa tanesco uwe wa kitaalamu sio kusubiri mtambo uharibike tuanze kutafuta mchawi.
 
du kazi kweli safari tunayo nayo ni ndefu,jamani ZITTTO hivi umeona IPTL sijui na DOWANS ndo suluhisho?jamani tununue mitambo mipya na tuanze programs za kufikiria njia za kumaliza kabisa tatizo la umeme.tufikirie vyanzo vingine vya umeme na sio maji tu na majenereta.Jamani kuna Geotherms,nukilia sijui na makaa ya mawe jamani wanageologia mko wapi sasa tunahitaji utaalaam na sio porojo hizi za kisiasa

Mkuu Mama 5J's,

Ni kweli kwamba serikali inapashwa ifanye kazi na ipate ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme. Nafikiri alichosema Zitto ni katika kuhakikisha tunakuwa na suluhu ya haraka ya tatizo hili na kwa muda huu.

Tiba
 
I would like to point out that all those cheering Zitto:
- Amebadili msimamo wake wa kung'ang'ania eti Dowans innunuliwe kwani amekubali kuwa imetokana na mkataba wa KIFISADI, kitu ambacho amekuwa aki-deny until now na alisema eti akina Mwakyembe wanaleta siasa. And what is he doing now? So, kwanza tutambue kwamba he has BACKPEDALED on this issue, so this means he has no backbone, no principal ni bendera hufuata upepo.
- Ameendelea kushikilia a FALLACY eti matatizo ya sasa ya umeme ni kutokana na Dowans, something that is propagated by Mafisadi, because matatizo ya umeme ni siasa mbovu ya CCM, so just drop it and forget about Dowans.
- Ametoa ushauri wa kutaifisha Dowans, ushauri ambao si ye wa kwanza kusema hata akina Mwakyembe na wanasiasa wengine walishawahi kutamka nadhani wakati wa Richmond pia, lakini imeonekana kuwa hatua hii italeta kesi tu na mwisho kufaidisha mafisadi
- Hajatoa suluhisho yoyote about the LONG TERM solution

Kwa hiyo in summary, siwezi kumfagilia Zitto, na ningempenda kumshauri, next time atulie kabla hajaanza kuongea hovyo.
Ningefurahi kuona pale ambapo angeweza kutumia muda huu kuonyesha ni kwa jinsi gani serikali ya CCM kwa miaka zaidi ya 40 imeshindwa kuzalisha umeme wa kutosha kwa nchi kama hii ya kwetu ambayo haina hata viwanda vingi.
Zitto awe wa kwanza kuonyesha mfano kwa kuacha kupiga siasa and trying to cover his behind with semantics!
 
Pia kumekuwa na shutma mbalimbali, mojawapo ikidai kuwa baadhi ya watendaji wa TANESCO wanajaribu kuthibitisha madai yao ya kitaalumu ya kununua mitambo ya DOWANS. Shutma kama hizi, ni dhahiri zinauelewa finyu juu ya vyanzo vya mgao wa umeme uliopo sasa, ambao unasababishwa na uhaba wa mashine na upungufu wa maji. Uelewa huu finyu si tu hauna manufaa, bali hautoi ufumbuzi juu ya tatizo lililopo sasa ili kuepuka madhara ya kiuchumi kwa taifa na wananchi wake.​

KABWE ZUBERI ZITTO,MB
Dar es Salaam.
Shutma hizi ni sahihi na kweli kwa sababu baada ya kujua kuwa mitambo ya dowans haiwezi kununuliwa na serikali kwa kuwa sheria hairuhusu serikali kununua mitambo chakavu, tanesco ilipaswa kuanza mara moja mchakato wa kununua mitambo mipya! Kwa nini walinyamaza tu kama siyo hujuma?

Mheshimiwa Zitto uelewa wetu siyo finyu, tunaelewa vyema vyanzo vya mgao wa umeme - uhaba wa mashine na upungufu wa maji kama ulivyoeleza; kwa kuwa suala la ukame linaweza kuwa liko juu ya uwezo wetu kwa kiasi fulani, hili la mashine liko 100% ndani ya uwezo wetu, na ndiyo maana tunailaumu tanesco kwa kutonunua mitambo mipya kama sheria ya manunuzi inavyotaka - labda Zitto uende bungeni uombe sheria ibadilishwe ili serikali iruhusiwe kununua vitu chakavu - nina imani ruhusa hiyo itakuwa na madhara makubwa pia kwani thamani yake itakuwa ni subjective tu!

Uelewa wetu huu, ambao wewe unauita finyu, unasaidia sana kutafuta suluhu, maana ukijua umejikwaa wapi, basi unapakwepa ili usijikwae tena.

Mimi naamini kabisa kuwa watendaji wakuu wa tanesco wangeweza kuepusha janga hili kwa kuwahi kununua mashine mpya lakini wakang'ang'ania chakavu za dowans wakati wakijua sheria hairuhusu - hakika hii ni janja yao ya kutaka kuhalalisha dowans kwa mlango wa nyuma.
Ninachokubaliana na wewe ni hiki ulichosema:
"Kwa kuwa mitambo ile inaweza kuingiza 125MW katika gridi ndani ya siku moja na kumaliza kabisa mgawo uliopo hivi sasa na kuliokoa Taifa na kuhami uchumi wetu, na kwa kuwa mitambo ya Dowans inahusishwa na mkataba wa kifisadi wa Richmond, ninaishauri serikali itaifishe mara moja kampuni ya Dowans."
 
Hili la kutaifisha mitambo ya Dowans sijui Serikali inasubiri nini. Kama kampuni iliyoileta hii mitambo ilikuwa hewa, kigugumizi kinatoka wapi cha kuichukua bure kwa manufaa wa watanzania!

Hili la kutaifisha mitambo hata mimi naliunga mkono. Huyo papa fisadi RA alilipwa karibu $200 million katika mkataba wake na TANESCO pamoja na kuwa hakuzalisha hata tone la umeme na wala hakuna anayefuatilia ili pesa hizo zirudishwe hivyo kutaifisha mitambo hiyo itakuwa ni kama kurudisha baadhi ya malipo ya peza za walipa kodi wa Tanzania ambazo papa fisadi RA alilipwa bila kuzifanyia kazi.
 
Kwa taarifa hii "Ngeleja" alitakiwa awe ameshajiuzulu U-waziri??? hivi anasubiri nini? hopeless waziri...
 
Kwa kuwa mapendekezo ya TANESCO ya kununua mitambo ya kampuni ya Dowans yalipingwa na baadhi ya wanasiasa wenzangu na hatimaye kutonunuliwa na hivyo kusababisha mgawo uliopo hivi sasa, na kwa kuwa mitambo ile inaweza kuingiza 125MW katika gridi ndani ya siku moja na kumaliza kabisa mgawo uliopo hivi sasa na kuliokoa Taifa na kuhami uchumi wetu, na kwa kuwa mitambo ya Dowans inahusishwa na mkataba wa kifisadi wa Richmond, ninaishauri serikali itaifishe mara moja kampuni ya Dowans.

Mwanakijiji alisema hii Mitambo ya DOWANS lazima inunuliwe ndicho kinachoendelea hapa! Sidhani kutonunuliwa ndicho chanzo cha mgawo wa umeme ama ndilo suluhisho, kuna watu wamependekeza pamoja na kuwa tupo kwenye shida tutafute mbinu ya kudumu, tuna Uranium, Upepo etc etc Hii Dowans inawalakini na harufu ya Ufisadi!
 
Mkuu heshima mbele,
Hivi wewe unaelewaje haya maneno EMERGENCY or CRISIS?
Hiyo mitambo mipya unayoongelea itakuja baada ya siku moja au wiki moja??? Jamani hivi tunaelewa sasa tuko kwenye hali mbaya sana kutokana na kukosa umeme. Sio wakati wa kusubiri plan ni wakati wa kufanya maamuzi ya haraka na machungu basi.
This is what we call state of emergency...

Mara zote tumeambiwa EMERGENCY or CRISIS tuling'atwa? Nini kinakufanya uamini sasa hivi hatung'atwi? Aliyeng'atwa na nyoka hata akiona jani tu, anastuka. Watu wanastuka mtu mzima.

Si kwamba nasema mitambo hiyo isinunuliwe, lakini inanishangaza pale mnapoamua kuuweka pembeni ukweli kwamba na hapa tunaweza kung'atwa vile vile.

Na mnanishangaza zaidi pale mnaporuka ukweli kwamba toka washauriwe kutonunua mitambo hiyo hawajaanza utaratibu wowote wa kununua hiyo mitambo mipya ambayo wewe unaona haichukui siku moja au wiki moja?

Yaani kama vile walikuwa wanasubiria "MERGENCY or CRISIS" ili wapate sababu ya kuinunua. Na tulivyo madunya hatuulizi kwamba walikuwa wanasubiri nini mda wote huo hata ku-place order tu. Yaani wanatufanya kama watoto vile, yaani kama vile tuna-udumavu wa akili.

Ushabiki pembeni, swali la msingi la kujiuliza ni je gharama ya hii "crisis" ambayo kwa kiasi kikubwa ni ya kujitakia itazidi gharama ya kununua hiyo mitambo? Historia inaonyesha gharama za kuwa na IPTL and the like ni kubwa kuliko gharama ya ile crisis iliyotumika kushawishi kufanya kilichofanyika.

Na kwa maoni yangu kuna kila dalili ya kutokuwa na nia njema katika dili hii ya kutaka kununua mitambo ya DOWANS.

Mvua zitaanza kunyesha mda simrefu tuvute subira bandugu. Mean while awajibishwe yeyote ambaye alitakiwa awe ameshapeleka order ya mitambo mipya.
 
Hili la kutaifisha mitambo hata mimi naliunga mkono. Huyo papa fisadi RA alilipwa karibu $200 million katika mkataba wake na TANESCO pamoja na kuwa hakuzalisha hata tone la umeme na wala hakuna anayefuatilia ili pesa hizo zirudishwe hivyo kutaifisha mitambo hiyo itakuwa ni kama kurudisha baadhi ya malipo ya peza za walipa kodi wa Tanzania ambazo papa fisadi RA alilipwa bila kuzifanyia kazi.
Babu hapa tunatakiwa tutumie legal process, kuwashtaki wahusika , mahakama i-amue na ni mkosa ndipo unaweza kupewa na mahakama fidia stahili au kuwa na huo upenyo wa kutaifisha, ama sivyo serikali itakuwa kwanza kama inataka kuficha kitu kwa kufanya hivyo , pili itakuwa ni prosecutor wao na judge ni wao. ni sawa na kutumia maguvu.
 
Kweli zitto "EXTRA ORDINARY CIRCUMSTANCES REQUIRES EXTRA ORDINARY DECISIONS....hili JK hajui, kidogo mkapa pamoja na wizi wake, alikuwa na uwezo wa kuchukua mamuzi magumu....Bravo Zitto....2015 sio mbali...vuta subira, na hao akina mbowe wasibomoe chama.
 
Kwa taarifa hii "Ngeleja" alitakiwa awe ameshajiuzulu U-waziri??? hivi anasubiri nini? hopeless waziri...

Mkuu Tumain, Kwa maoni yangu Serikali nzima inatakiwa ijiuzulu maana imeshindwa kazi katika maeneo mbali mbali si hili la umeme tu.
 
Haya mambo ya kutaifisha kwenye ulimwengu wa sasa wa good governance hayana nafasi. If anything yata tuingiza katika migogoro ya kimahakama na hatimae ni kushindwa kesi na hasara kubwa zaidi ( refer IPTL na City water kesi )

Talk about mikataba ya kifasadi, hivi IPTL leo ni wasafi hivyo? kweli watanzania wepesi kusahau.

Hoja ya msingi ni ya rafiki yangu Waberoya, acha siasa pembeni taifa lipo kwenye kiza tunafanya nini? Hii habari ya mitambo hii ya kifisadi sijui sheria ya manunuzi and all that rubbish tunaangamia jamani we.

Walau sasa wengi tunakubaliana kuwa nchi ipo kwenye crisis inayo fanana na vita. Kama ni hivyo lets act now badala ya kuanza kutafutana mchawi nunua Dowans, nunua IPTL washa umeme halafu tukutane Dodoma tuanze kulumbana nani kala 10% nani kafanya nini lakini viwanda, mahospital, mashule nk yanapata umeme.

Masatu,

Kununua mitambo ya Dowans no please!!!!!. Tutaifishe tu na wakitaka waende mahakamani kwanza nani ataenda kushitaki wakati aliyewaachia mitambo hiyo Dowans si kampuni halali? Huu ulikuwa ni utapeli wa hali ya juu sana kwani nafikiri hata hawa Dowans waliingizwa mjini na Richmond.

Tunataka suluhisho la haraka.

Tiba
 
Emergency ya kununua umeme "Ilizaa Richmond" , Richmond ikazaa Doawns...wakati huo wote emergency haikushughulikiwa...sasa imezaa mgawo..nao umelata emergency...sasa hii emergency itazaa "RichPinda" (yaani kama Richmond)...kitakochofuata uchaguzi.....tumie solar"
my Take: Bottom line -safisha serikali yote lete nyingine..blah blah nyingi
 
suluhu aliyoitoa zitto kuhusu mgao wa umeme mi naona ni ya muda tu..kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyika! .

tusaidie hayo mkuu, inonekana unajua

- Hajatoa suluhisho yoyote about the LONG TERM solution

Kwa hiyo in summary, siwezi kumfagilia Zitto, na ningempenda kumshauri, next time atulie kabla hajaanza kuongea hovyo.
!

Zito ni wa kutoa long term solution, wakati kama huu, maoni yako ni nini?? kuhusu kutatua hili tatizo??

Mwanakijiji alisema hii Mitambo ya DOWANS lazima inunuliwe ndicho kinachoendelea hapa! Sidhani kutonunuliwa ndicho chanzo cha mgawo wa umeme ama ndilo suluhisho, kuna watu wamependekeza pamoja na kuwa tupo kwenye shida tutafute mbinu ya kudumu, tuna Uranium, Upepo etc etc Hii Dowans inawalakini na harufu ya Ufisadi!

Are you serious, wakati kama huu, unataka suluhisho liwe nini?? kuna watu wanakufa ndugu!inaonekana MKJJ angekuwa na msimamo mwingine ungekuwa upande wake.

Babu hapa tunatakiwa tutumie legal process, kuwashtaki wahusika , mahakama i-amue na ni mkosa ndipo unaweza kupewa na mahakama fidia stahili au kuwa na huo upenyo wa kutaifisha, ama sivyo serikali itakuwa kwanza kama inataka kuficha kitu kwa kufanya hivyo , pili itakuwa ni prosecutor wao na judge ni wao. ni sawa na kutumia maguvu.

That have never happened?
 
Back
Top Bottom