Townchild
JF-Expert Member
- Aug 29, 2018
- 15,409
- 17,209
Acha wazito kabwela wangatuke,ila mwepesi mjanja bado tunakazi naye hadi wenyewe tuseme😎Uongozi ni kuachiana Kijiti. Hivyo ndivyo amefanya bwana Zitto Kabwe baada ya kung'atuka nafasi ya Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Ili damu changa na Mpya zishike hatamu.
Zitto anaachia ngazi ikiwa amekijenga chama hicho kujikita kwenye hoja na mambo ya msingi(issues) badala ya kile Chama Kingine Cha Matukio na kisicho na ajaenda yaani Chadema.
Chadema imekuwa chama Cha Matukio na upepo Kwa sababu ya kuwa na Kiongozi Sultani bwana Mbowe ambae kimsingi hana jipya, kiasi kwamba kadiri anavyozeeka ndivyo na chadema kinazeeka 😁😁
Alichosema Zitto akiwa katika kipindi cha Power Breakfast, Clouds FM
My Take
Hongera bwana Zitto kwa Kufuata misingi ya Baba wa Taifa.
ACT imeonesha Uongozi kwenye mambo mengi hasa kwenye uchambuzi wa kiuchumi na jambo la Bima ya Afya, kule mna hoja za msingi sana Serikali ifuate ushauri wao.