Zitto amwambia Makinda nipo tayari kuvua dagaa kijijini kwetu

W.J Malecela,
Mkuu wangu hapa utakuwa unakosea kabisa kuchanganya Ujamaa na malipo ya posho kubwa kwa Wabunge, jambo ambalo hata kiasilimia halina mvuto kabisa. Ebu fikiria tu, Marekani ni ndio Mabepari, halafu waambiwe kwamba viongozi na watumishi wa serikali wametengewa posho zinazozidi asilimia 7 ya bajeti nzima ya nchi kweli kutakalika?..

Sasa hawa ni Marekani ambao sisi hata ukubwa wa mkia wa mbuzi kiuchumi hatuna ukilinganisha nao iweje kweli tusahau kwamba matatizo yetu, umaskini wetu unatokana na UFISADI kwani ufisadi hauishii kwa kina magamba pekee bali hata sheria za kodi, posho, mikataba, urasimu, ukiritimba na mengineyo yote yanachangia ktk kudhoofisha uchumi wetu.

Halafu basi hivi kweli mnataka kunambia kwamba Liberal au Democratic kina Obama ni Wajamaa? (Masocialist) sio Mabepari?, naomba ushahidi tosha wa ku prove hili kimaandishi.

Katika swala la Zitto nimemwona mhuni tu pale aliposema yupotayri kwenda kuvua dagaa! mhhh mbunge wangu Sharobaro kweli ataweza kuvua dagaa au ndio ktk kuchangana madawa!
 
safi sana zitto, watu wamagamba wameshachanganikiwa sasa, maana kiukweli watu hao hii posho inawatoa balaa na ndomaana wengine atleat wameanza kumuunga mkono kabla haijala kwao.
 
Wandugu ebu nisaidieni,atafukuzwa bungeni kwa kosa lipi hasa?kwani kukataa posho ni kinyume cha sheria au kanuni za bunge?utovu wa nidhamu?
Mkuu,Kukataa posho siyo kinyume cha sheria bali msingi wa hoja ni kwamba ili uhesabiwe umehudhuria vikao sharti usaini kitabu cha mahudhurio, kitendo ambacho automatically kinakufanya uhesabiwe kwenye mgao wa posho za siku uliyohudhuria. Sasa Kamanda Zitto kuambiwa hivyo akaona bora asisaini na aende akavue dagaa kijijini kwao kuliko kulazimishwa apokee posho ambayo kwa mtazamo wake na wengi wetu hastahili kupokea kwa maana kukaa kikao ni sehemu ya majukumu yake kama mbunge.Binafsi nam-support 100% maana hakuna kosa lililotendeka isipokuwa tu wanaMagamba wakiongozwa na Spika wao wa kupachikwa na mapacha watatu kwa tamaa zao zisizo na kikomo wanataka kumfanyia zengwe ambalo bila shaka litagonga mwamba. Halafu sipati picha wachangiaji wa bajeti yetu wanatatuchukuliaje baada ya kugundua kwamba sehemu kubwa kama si yote ya mchango wao wa kifedha kila mwaka kwenye bajeti yetu unaishia kulipana posho miongoni mwa wabunge na watendaji wengine wa kiserikali. Natabiri, posho isipoondolewa, bila shaka nao watagoma kuchangia bajeti ijayo. Si tuliona ile ishu ya EPA. Yangu macho.Kalaghabhao.
 
Tatizo ni kwamba hazitaki na huku anazitaka ,kwa maana kwamba anataka ziende kwenye mfuko wa maendeleo kigoma badala ya kubaki mfuko wa serikali. Zikienda kigoma maana yake amezichukua, na hapo naungana na spika kwamba azichukue halau azipeleke kigoma mwenyewe, kinyume chake fedha hizo aziache kwenye mfuko wa serikali.
Mkuu nadhani hukumuelewa Zitto kupitia ile barua yake.Yeye alisema kwamba posho zipelekewe kwenye mfuko wa taasisi ya Kigoma Development Initiative iwapo Bunge halitasitisha ulipwaji wa posho. Na zisimamishwe kupelekwa KDI pale utaratibu wa kulipana posho utakapokufa. Alipoambiwa achukue yeye azipeleke KDI, akajibu ni bora asichukue kabisa. Vipi tena mkuu? Unataka zibaki kwenye mfuko wa serikali ili ziendelee kuchakachuliwa na mafisadi nn?
 
Mi naona kamanda zitto yupo sahihi kabisa kwani hizo hela zikipelekwa kigoma ama kwenye taasisi nyingine zitakuwa zimefanya kazi sahihi ya kuusaidia umma wa Tanzania, ni hayo2
 
Maskini Zitto.
Anatetea matumizi mabaya ya fedha za serikali lakini shukrani yake ni kuambiwa ooh eti mara anajuitafutia umaarufu etc etc.
Mimi naona sasa angejikalia kimya.

Serikali iendelee kuzitafuna hela kadri itakavyo. Mafisadi waendelee kuikomba hii nchi hadi ifilisike na kuwa a failed state. Wabunge wajiongezee salary na wajilipe TSHS 50 Million a month.

Sitting allowances ziongezwe toka 70K to 500K. Per diem yao iwe 500K. Speaker Makinda aongezwe mshahara kuwa 100 Million a month!!
Nchi iendelee kutafunwa na kutafunika weeeeeeeeeeeeee hadi icollapse kabisaaaaaaaaaa chaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Bankrupt!!

Labda baada ya hapo ndio wabongo na akina Nape et al tutatia akili sasa na ule mgando wa akili yetu utayeyuka na kuacha ushabiki wa vyama na kuweka maslahi ya nchi mbele ya maslahi ya chama.

Mkulu
Tuwe makini na wanasiasa.
Zitto siyo mkweli kwnye hili , naomba akatae ile 5ml anayolipwa kama posho ya mwezi , badala ya kukataa 70,000 ya sitting allowance.
Mshahara wa Zitto na wabunge ni 2.3 ml basic plus 5ml posho which makes 7.3 ml gross salary.

Je mtumishi wa umma au mfanyakazi wa kima cha chini kwenye private sector analipwa kiasi gani????!!!!!!


NITAMPINGA KWENYE HILI, NA KWA KUWA YUPO HUMU , MARA ATAKAPOSOMA POST ZANGU ON THIS PARTICULAR SUBJECT ,AJARIBU KUJIBU HILI SUALA.

NCHI HII INA MATATIZO MAKUBWA SANA YA KUJADILINA KUCHUKUA HATUA NA AMBAYO HAYAJAFIKA MWISHO.
 
Nimemsikia Zitto Kabwe akiongea na BBC. Anasema msimamo wake upo palepale hatasaini karatasi ya mahudhurio, hatapokea posho na yupo tayari kurudi kijijini kwake kuvua dagaa baada ya kufukuzwa ubunge.

My take: Kwa hali ilivyo sasa ni wazi msimamo huu unaelekea kuungwa mkono na wananchi wengi. Najiuliza sana sipati jibu, mimi ambaye mshahara wangu unaisha baada ya siku 10 hizo bilioni 900 zinapotea kwa ajili ya posho zinanifikia kweli? Tafakari

THEY SAY THAT SUUCCESSFUL LEADERS RECOGNIZE THAT GREAT INNOVATION COMES FROM OBSERVING THE SAME IDEAS S EVERYONE ELSE AND SEEING SOMETHIGN DIFFERENT. it is not rocket science!!!!!!!!!!!
 
acheni ushabiki wa vyama vyenu,Kabwe Zitto yuko sahihi kwa maslahi ya taifa nzima ,mbona kuna wabunge wamekaa bungeni miaka nenda rudi lakini hawajakumbuka hilo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom