Zitto aibua Ufisadi mpya BOT, ni wa karibu 620bil

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Hotuba ya waziri kivuli Zitto iliyosomwa kwa niaba yake na Silinde imeibua ufisadi mwingine BOT pamoja na hasara waliyopata BOT mwaka jana.

2.1.2 Taarifa ya ukaguzi wa hesabu za BOT ya mwaka 2011/2012.

Mheshimiwa Spika,mnamo mwezi April 2013 Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilitoa tarifa yake yaukaguzi wa hesabu za mwaka wa fedha 2011/2012, miongoni mwa mambo ambayoyaliweza kuainishwa katika ripoti hiyo ni pamoja na taarifa ambayo ni ya kustuakwani Benki kuu imepata hasara kubwa katika mwaka huo wa fedha ya kiasi chashilingi bilioni 52.431ikilinganisha na mwaka uliotangulia 2010/2011 ambao BOT walipata faida kubwa yakiasi cha shilingi bilioni 727.793.

Aidha,katika taarifa hiyo ya ukaguzi ya BOT yapo mambo mbalimbali ambayo yaliainishwakama vile uwepo wa fedha za EPA, Mikopo mikubwa ya wakurugenzi na wafanyakaziwa Benki Kuu, fedha za IPTL katika ‘Tegeta Escrow account' ya BOT, kufungwa/kufilisiwa kwa kampuni la ubia la Mwananchi Company ltd na mengineyo mengi.

Kambi rasmi ya UpinzaniBungeni, inataka kupata majibu yakina kuhusiana na masuala yafuatayo yaliyoibuliwa na ripoti hiyo ya ukaguzi;

i. Ni utaratibu gani unatumika katikakuwakopesha wafanyakazi fedha kwa ajili ya nyumba na kununulia magari binafsina kukokotoa riba ya mikopo kwa wafanyakazi na viongozi wakuu wa BOT kwanimpaka tarehe 30 Juni ,2012 walikuwa tayari wamejikopesha shilingi bilioni 55.668 ,ikilinganishwa nashilingi bilioni 38.965 mwaka 2011 .

Aidha,tunataka kujua kama fedha hizi ni tofauti na kile kinachoitwa ‘staffHousing Fund' ambao ni mkopo kwa wafanyakazi unaotokana na faida yakila mwaka inayopatikana kutokana na shughuli mbalimbali za BOT, 2012 mfukoulikuwa na kiasi cha shilingi bilioni34.170 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa BOT kwa ajili ya nyumba

ii. Mfuko wa Elimu wa Mwl.Nyerere (Mwl.Nyerere Scholarship fund) , mnamomwaka 2009 BOT ilianzisha mfuko huo kwa ajili ya kuwapa udhamini wasichanakusoma shahada ya kwanza kwa wale ambao watafaulu vizuri masomo ya Sayansi naHisabati na hadi mwezi Juni 2011 Mfuko ulikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 1.715 .Aidha , katikamwaka wa fedha 2012 mpaka tarehe 30 Juni mfuko ulikuwana shilingi 0 Je,ni utaratibu gani huwa unatumika katika kupatafedha hizi na ni wanafunzi wangapi mpaka mwaka huu wa fedha wamesomeshwa namfuko huu na wanasoma vyuo gani?

iii. Akaunti ya malipo ya nje (EPA),Mpaka tarehe 30.06. 2012 kwa mujibu wa ripoti hiyo akaunti hii ilikuwa na kiasicha shilingi Bilioni 205. 743, jefedha hizi zina usalama gani mpaka sasa na je, hazitachotwa kama ilivyofanyikamwaka 2005? Aidha, mpaka sasa ni wakina nani (orodha ya majina ya watuwaliorejesha fedha )na ni kiasi gani cha fedha kimerejeshwa kutokana na Ufisadiwa shilingi bilioni 133 uliofanyikakatika kipindi cha mwaka 2005? Maamuzi ya Serikali ilikuwa ni kuondoa kabisaakaunti hii ya EPA kutoka Benki Kuu. Kwa nini bado akaunti hii ipo Benki Kuu?

iv. Kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi wahesabu za BOT Katika mwaka wa fedha 2011/2012 ni kuwa BOT ilipata hasara yashilingi bilioni 52.431ikilinganishwa na faida ya shilingibilioni 727.793 iliyopatikana mwaka 2011 .Tunataka majibu ya kina kuhusianana hasara hii kwani haiwezekani taasisi nyeti kama hii ipate hasara na taifalisiweze kupewa taarifa za kina kuhusiana na chanzo cha hasara hii na ni hatuagani zimechukuliwa mpaka sasa katika kukabiliana na hasara hii.

Kuhusiana na deni la taifa nako kuna madudu haya , hotuba ilisema hivi;

3.0 FUNGU 22- DENI LA TAIFA

MheshimiwaSpika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni tunatambua kuwanchi nyingi duniani kama sio zotezinakopa ili kuboresha huduma na kwa ajili yamiradi mbalimbali ya kimaendeleo, na hutumia fedha za walipakodi katikakuendesha shughuli za serikali.

Mheshimiwa Spika,Kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, deni la taifaliliongezeka kwa asilimia 38 kutoka Shilingi trilioni 7.6 mwaka 2008 mpaka Tshstrilioni 10.5 mwaka 2009/2010,

Mheshimiwa Spika,Mwaka 2010/2011 deni hilo liliendelea kuongezeka kutoka shilingi Trilioni 10.5 na kufikia kiasi chashilingi Trilioni 14.441 .Katikamwaka wa fedha 2011/2012 deni la taifa liliendelea kuongezeka kutoka shilingi Trilioni 14.441 na kufikia kiasi chashilingi Trilioni 16.975

Mheshmiwa Spika, Katikahali isiyokuwa ya kawaida deni la taifa limeongezeka kwa kasi sana na hadi Disemba 2012 lilikuwa limefikia kiasicha shilingi Trilioni 21.028 kutokakiasi cha shilingi Trilioni 18.258Disemba mwaka 2011 na kati ya hizo asilimia 75.97 zilikuwa ni deni la nje .

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmiya Upinzani Bungeni, ina taarifa kwamba takwimu hizi zaDeni la Taifa hazihusishi dhamana ambazo Serikali imezitoa kwa Mashirika yaUmma na Kampuni binafsi. Aidha, ni lazima Dhamana katika siku za usoni ziwe nisehemu ya deni la Taifa maana tumeshuhudia sasa ambapo Kampuni nyingi binafsizimeshindwa kulipa mikopo iliyodhaminiwa na Serikali. Mfano ni malipo ya denilenye thamani ya shilingi bilioni 60 la kukodisha ndege ya Airbus kwa Shirikala ATCL kutoka kampuni ya Wallis Traders ya Lebanon na Deni lililochukuliwa naKampuni ya Kiwira Coal and Power limited ambayo mbia wake alishindwa kuendeshamradi wa Makaa ya Mawe Kiwira licha ya kudhaminiwa na Serikali Mkopo kutokakwenye taasisi za Fedha hapa nchini ambapo sasa Serikali imelipa shilingi bilioni40 katika Bajeti ya mwaka 2012/13.Aidha,tunatambua kuwa serikali ina madeni ambayo hayajajumuishwa kwenye deni la taifana hiyo inalipelekea deni la taifa kuwa kubwa kuliko linaloonyeshwa kwenye taarifambalimbali za Serikali na ile ya CAG, kwa mfano kuna madai ya PSPF ya shilingi 716,600,000,000 kati ya madai yashilingi trilioni 6.5 ambayoserikali inadaiwa na imekubali kuyalipa madeni hayo, vilevile kuna madeni yashirika la ndege la Afrika ya Kusini naCiti Bank kiasi cha dola 4,129,298.38 na dola 1,460,000 sawa na shilingi bilioni 8.8 kwa ujumla wakeambazo hazijajumlishwa kwenye deni la taifa wakati zitalipwa na serikali, Aidha kuna dhamana mbalimbalizilizotolewa na serikali kwa ajili ya idara, wizara na mashirika ya ummazinazofikia shilingi trilioni 1.250(chanzo: ripoti ya CAG ).

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani haina tatizo na uhimilivu wa Deni la Taifa (Debtsustainability) kwani tunajua kuwa mataifa makubwa yanakopa sana na yana uwianomkubwa wa Deni kwa GDP kuliko sisi. Tatizo letu ni namna ambavyo fedha zamikopo zinatumika. Matumizi ya mikopotunayochukua sio endelevu maana sehemu ya mikopo hiyo hutumika kwa matumizi yakawaida badala ya matumizi ya uzalishaji au kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha.

Mheshimiwa Spika, pamojana umuhimu wa kukopa kama ambavyo mataifa mengine hufanya hivyo, kwetu sisi hiini kasi kubwa mno ukilinganisha na ukuaji wa uchumi wa nchi yetu kwa sababuukopaji unategemea uwezo wa kulipa pia. Hii itasababisha mzigo huu wa madenikubebwa na kizazi cha sasa na kijacho. Ukilinganisha na nchi nyingine za AfrikaMashariki, Tanzania bado ina viwango vidogo vya mikopo kama sehemu ya Pato laTaifa (debt/GDP ratio). Hata hivyo, wakati wenzetu wanakopa ili kuongeza uzalishaji(capital investments), sisi tunakopa kwa matumizi ya kawaida. Kambi ya Upinzaniinapendekeza kuwepo kwa namna bora zaidi ya kuamua kuhusu mikopo ambayo Taifalinaingia ili kuhakikisha inaelekezwa katika uzalishaji mali.

Mheshimiwa Spika,katika taarifa ya CAG ya mwaka 2012, kuna jumla ya shilingi bilioni 619 ambazozipo kwenye deni la Taifa lakini hazina vithibitisho. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali ameandika "Uhakikiwa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30 Juni 2012 ulibainikuwepo kwa marekebisho ya Deni ya shilingi 619.8 bilioni ambao uongozihaukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha" Mwisho wa kunukuu. Kambi ya UpinzaniBungeni imeshtushwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha deni ambalo halinavielelezo. Tunataka maelezo ya kina sana na sahihi kuhusu taarifa hii kwaharaka.

Mheshimiwa Spika,Dhamana za Serikali kwa ajili ya makampuni yanayouza bidhaa nje (ExportGuarantee schemes) zilianzishwa ili kuwezesha makampuni yetu kumudu kuuzabidhaa nje na kuingizia Taifa mapato ya Fedha za Kigeni. Hata hivyo katikampango huu Serikali inaelekea kupoteza jumla ya shilingi bilioni 300 kutokanana makampuni yaliyopewa dhamana kutolipa mikopo yao kwenye mabenki. Hiiinaongeza deni la Taifa kwa kiwango hicho cha fedha.

Kambi Rasmi ya Upinzaniinaendeleza wito wake wa kutaka Fungu 22 la deni la Taifa lifanyiwe ukaguzimaalum (Special Audit) na Mdhibitina mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili tuweze kujua mikopo hii tunayochukua kila wakati inatumika kufanyianini, na miradi iliyotekelezwa kama ni miradi ya kipaumbele kwa mujibu wampango wa taifa wa maendeleo. Aidha, ukaguzi huu maalum utatuwezesha kama taifakujua kiwango halisi cha deni la taifa ambalo tunadaiwa.

3.1 Malipo ya riba na Deni la Taifa.

Mheshimiwa Spika,kwa miaka mingi mfululizo tumekuwa tukitenga fedha kwa ajili ya kulipia deni laTaifa pamoja na riba mbalimbali zitokanazo na deni hilo la taifa .Kwa mujibu waripoti ya ukaguzi ya CAG iliyoishia Juni 2012 ni kuwa tumekuwa tukilipa riba yadeni la taifa kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2007 hadi 2012 jumla ya kiasi cha shilingi Trilioni 1.523, (tazama jedwali01)Jedwali 01:


Malipo ya riba kwamiaka mitano iliyopita (tarakimu katika billion):
Wadeni
2007/08
2008/09
2009/10
2010/11
2011/12
Multilateral
20.29
26.75
26.32
51.41
62.58
Bilateral
8.07
4.06
1.47
11.07
2.61
Commercial /Exp
-
5.09
0.81
2.58
20.42
Jumla ndogo
28.36
35.90
28.60
65.06
85.61
Domestic
241.64
208.35
229.39
271.64
328.75
Jumla kuu
270.0
244.25
257.99
336.70
414.36


Mheshimiwa Spika,
kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014 fungu 22 programme 10 utawala kasma 1001 kifungu kidogo 820300 inaonyesha kuwajumla ya shilingi 357,304,000,000zimetengwa kwa ajili ya kulipia deni halisi la taifa (Principal). Vilevilekatika kifungu 250500 kwa mwaka huu wa fedha zimetengwa jumla ya shilingi 425,700,000,000 kwa ajili ya kulipiariba ya madeni ya muda mrefu ‘Interestpayments on long-term debt to other General Government'Aidhakatika kifungu 250100 fedha zilizotengwa kwa ajili ya kulipia riba itokanayo nadeni la taifa ni kiasi cha shilingi 323,154,880,000na katika kifungu 250600 zilizotengwa kwa ajili ya kulipia riba ya deni lataifa la ndani ‘other domestic interestpayments not elsewhere classified' kiasi cha shilingi 3,087,837,000

Mheshimiwa Spika, kwaujumla ni kuwa fedha iliyotengwa kwa ajili ya kulipia deni halisi la taifa (loanspayment principal,fungu 820300) kwa mwaka huu wa fedha ni shilingi 357,304,000,000 wakati fedhailiyotengwa kwa ajili ya kulipia riba itokanayo na deni la taifa la nje nandani kasma 22, (fungu 250100,250300, 250400, 250500 na 250600 )kwamwaka huu wa fedha ni shilingi 1,021,942,717,000.00

Mheshimiwa Spika, kutokanana hali hii ya kutenga trilioni za fedha kwa ajili ya kulipia riba za deni la Taifa,Kambi rasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa kuna haja ya kufanyika kwa ukaguzimaalum (special audit) ili taifa liweze kujua kama mikataba ya madeni hayainafuata utaratibu mzuri wa kiwango cha riba ambayo tunatozwa kila mwaka.

Mheshimiwa Spika,tunasisitiza ukaguzi maalum kufanyika kutokana na ukweli kuwa mpaka sasaSerikali haina kitengo maalum kwa ajili ya deni la taifa na hii inathibitishwa na taarifa ya waziri wafedha ya tarehe 25 Machi 2013 ‘maelezoya waziri wa fedha kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasilishaMwongozo, matazamio na Upeo wa Bajeti ya 2013/14' uk.4, aya ya pili alisema, nanukuu "….Serikali iko katikamchakato wa kuanzisha Idara ya Madeni ambayo pamoja na mambo mengine itakuwa najukumu la kujenga uwezo wa kufanya upembuzi yakinifu na kuhakikisha usimamizimadhubuti wa deni la Taifa"

Kambi rasmi ya upinzani Bungeni,haiwezikuendelea kukubaliana na utaratibu huu wa kukopa bila hata kuwepo kwa idarainayofanya uchambuzi yakinifu wa deni hilo na riba husika kama mkopounazingatia thamani halisi ya fedha ‘value for money' ya mradi unaokopewa fedhahizo, hatuwezi kuendelea kulipia deni ambalo hatujui limewekezwa kwenye mradigani wa maendeleo na manufaa ya mradi husika kwa taifa letu.
 
Mpaka wa tuchune ngozi BOT badala ya kulinda thamani ya fedha yetu wao wamefanya shilingi yetu kama dabwada badala ya kusimamia mabenki wao wanaidhinisha mabenki kuhamisha na kutorosha fedha kupeleka nje,badala ya kudhibiti mfumuko wa bei wao ndio biashara holela we need immediate change to proctect our land
 
Yaani wafanyakazi BOT wanajikopesha bilioni 55, pesa nyingi kuliko pesa zote za wizara ya Afrika Mashariki,Wanawake jinsia na watoto, huwa wanatumia vigezo gani hawa watu?
 
Hivi BOT kuna wafanyakazi wangapi? Maana wakiwa wako jumla ya wafanyakazi 5000 kila mmoja atakuwa amepata wastani wa shilingli milioni 100 kama mkopo kwa mwaka ....this is a hell of money......
 
Hivi BOT kuna wafanyakazi wangapi? Maana wakiwa wako jumla ya wafanyakazi 5000 kila mmoja atakuwa amepata wastani wa shilingli milioni 100 kama mkopo kwa mwaka ....this is a hell of money......

sidhani hata 1000 wanafika
 
Na hapo waliojikopesha n vigogo tu wasiozidi hata 20, wakati kuna shule hazina madawati, walimu nk. Hii ndio Tanzania chini ya uongozi wa CCM
 
Kaka Fastjet nitafutie kazi BOT na mimi nipate mkopooooo. Hivi deni la trilioni 21 hizo hela zimefanya kazi gani wakati kuna watu bado wanakufa kwa malaria,wanavijiji hawana maji safi,barabara na umeme vijijini hamna? what the hell has the serukambaing money haa done?
 
Si ndo maana unambiwa hadi upate ajira huko lazima uwe mtoto wa kigogo,jaribu kufuatilia utalijua hilo,sasa kwa nini wasijikopeshe 55bn,ndo uzuri wa kuwa mtoto wa kigogo bwana RITZ umechota ngapi wewe huko?pamoja na kwamba haufanyi kazi hukoi lakini wale uliowaingiza wamekupa share ya kiasi gani au ndo mambo ya 20%
 
Huko BOT inabidi tuanze kuajiriwa kwa kupokezana jamani hayo mamilioni mbona ni mengi sana? Shilingi Biloni 55 kwa mwaka mmoja? hakyanani ndio maana magamba wamejaza watoto wao huko BOT. Inawezekana hizo fedha sio mkopo kwa wafanyakazi bali ni wazee wa ufisadi wamezivuta na Prof. Ndulu akaamua kuita mikopo ya wafanyakazi.

Chini ya ccm ufisadi umeshakuwa wimbo wa Taifa, kila kukicha ni ufisadi juu ya ufisadi.
 
jamani hii sasa imezidi...afadhali katiba mpya itawawajibisha hawa hawa viongozi!
 
Hivi JF siku hizi kuna watu wa aina gani? hata kugawa bilioni 55 kwa say 1000 mtu hawezi?Jamani tuache majung fitna na kushadadia tuuuu. Ninavyojua mimi BOT inawafanyakazi kama 1,500 hivi nchi nzima. Sasa bil 55 gawa kwa hao ni sh.milioni kama 37 hivi. Huo ni mkopo wa nyumba. Sasa tuwe wa kweli na kumuogopa Mungu wetu hivi mfanyakazi kukopeshwa 37m mkopo wa nyumba ni hela nying sana kweli? hivi hiyo 37 m unajenga nyumba ya hadhi gani? hiyo si bei ya kiwanja tu?hebu fanyeni utafiti jamani acheni kuchukua vitu blindly sababu tu kasema Zito.Jamaa ni mjanja ndio maana hakuenda kwenye details alijua low thinkers watashadadia tu.
 
Bilioni 55 mikopo ya wafanyakazi ambao hawafiki 1000? hii inatisha

Hivi ni macho yangu au vipi au ? kama ni kweli ni Billion 55 na wafanyakazi 1,000 na kama hizo hela zigawane sawa sawa

ina maana kila mfanyakazi angepata mkopo wa Tshs. 55,000,000 au milioni hamsini na tano (55,000,000,000/1000)

Tuwe wawazi kwa mambo mengine.
 
Back
Top Bottom