Zitto aenda kutibiwa Ujerumani

labada ni zile kamati za bunge na ubunge ametengeneza fortune ya kutosha so kichwa tu, why not go to germany for treatment! sasa mtu kama uyu hata uongozi wa juu hajakamata ananza mbewembwe izi! peremende aliyopewa na ccm inapeleka puta! ama kweli wahenga walisema, penye uzia, penyeza rupia
 
nazani Zito anatakiwa ajue kwamba pamoja na kuumwa kwake na kujisikia vibaya kitendo cha kutangazia wananchi unaenda Germany kwa check up ya afya lakini akisisitiza ni fatigue inaleta maswali mengi na anajenga taswira mbaya kwenye jamii, hata Mheshimiwa raisi alipoanguka hakupelekwa nje.....nazani kuna haja ya kupima kwanza taarifa kuliko kusema tu na kuacha maswali, yaani uchoovu ukupeleke Germany for chek up? hell NO...ni dharau kwa hospital zetu na madoctor wetu hapa nchini lakini pia ni ufujaji wa rasilimali za taifa hata kama unajilipia mwenyewe....hayo sio maisha ya mtanzania na mpigania haki za wanyonge....gharama zote hizo zingeweza hata kujenga darasa au kusaidia maji kule jimboni.....
kuna haja ya Zito kutoa ufafanuzi wa wananchi juu ya hili bila hivyo atakuwa amewakebehi waTanzania....
 
siasa za tanzania haziwezi kufanana na nchi za nje .....hatujafika huko jamani! waacheni kina zitto wajitangaze wanaenda kutibiwa kipele Marekani pia, uelewa wa wananchi unawaruhusu kufanya hivyo.

wabunge tanzania wana watoto out of wedlock ......hakuna tatizo ( ingekuwa ulaya, angepata tabu kuwa mbunge au kuendelea na ubunge wake ( kama amepata akiwa mbunge)


wabunge wengi sana wana nyumba ndogo.....................but wananchi hatujali.

wabunge wengi ni mafisadi even.....................na wananchi hawajali wanawachagua hao kwa hao

sioni sababu ya kupiga kelele hili, la mtu kutumia pesa zake kwenda hospitali ujerumani........hakutomnyima kura.

Mkuu
Mimi nafikiri tunachanganya mambo hapa, hao unaosema wabunge wa ulaya ni kweli haita make sense kwa mbunge ama senata kutoka ulaya kwenda africa kutibiwa. Ila hao hao wabunge wa ulaya na maseneta wanatoka ulaya kwa mbwebwe zilezile za kuacha kuona wanyama kwenye zoo zao na kuja Tanzania kuangalia wanyama ktk bunga za serengeti.

Swala la wake, hilo unaongelea sheria za nchi na sio maadili kama unavyotaka tuamini. Nchi nyingi za ulaya haziruhusu ndoa za mme/mke zaidi ya mmoja, wakati sisi Tz sheria ya nchi inaruhusu kuwa na wake hata zaidi ya kumi.

Sasa utanitia je ktk kundi la watu wasio na maadili kama niko ktk mchakato wa kuongeza mke? Kwa namna nyingine nikiwa ktk mchakato wa kusaka mke wa pili ukaniita sina maadili hii inamaanisha serikali haina sheria zenye maadili.
 
mkamaP...
Wanaacha zoo kutembelea sio zoo ya Tanzania ....bali mbuga za wanyama ambazo kwao hazipo. mheshimiwa zitto angesema anaenda kutibiwa ugonjwa mzito kwa tanzania tusingeshangaa lakini kutibiwa fatigue Ujerumani ndo kulikowacha watu mdomo wazi.

kuwa na nyumba ndogo ndo utaratibu wa kutafuta mke? .....utaratibu wa kuwa na mke unajuulikana na kuwa na nyumba ndogo kunajuulikana. isitoshe wabunge kuwa na watoto nje ya ndoa pia sheria na maadili ya tanzania yanaruhusu?

lets be realistic..................tanzania kwetu kuna big big line baina ya mambo tunayoyaita personal na siasa........hli la kwenda kutibiwa nje naona tumeliingiza kwenye personal kama mtu anavyotafuta mke wa pili kwa kupika na kupakua nyumba ndogo na kuzaa watoto huko huko
 
mkamaP...
Wanaacha zoo kutembelea sio zoo ya Tanzania ....bali mbuga za wanyama ambazo kwao hazipo. mheshimiwa zitto angesema anaenda kutibiwa ugonjwa mzito kwa tanzania tusingeshangaa lakini kutibiwa fatigue Ujerumani ndo kulikowacha watu mdomo wazi.

kuwa na nyumba ndogo ndo utaratibu wa kutafuta mke? .....utaratibu wa kuwa na mke unajuulikana na kuwa na nyumba ndogo kunajuulikana. isitoshe wabunge kuwa na watoto nje ya ndoa pia sheria na maadili ya tanzania yanaruhusu?

lets be realistic..................tanzania kwetu kuna big big line baina ya mambo tunayoyaita personal na siasa........hli la kwenda kutibiwa nje naona tumeliingiza kwenye personal kama mtu anavyotafuta mke wa pili kwa kupika na kupakua nyumba ndogo na kuzaa watoto huko huko

Mkuu
Nafikiri alisema ana uchovu, ila kwa vile aliweweseka bungeni ameamua kwenda kufanya advanced medical checkup. si unajuwa hospitali zetu check up yao wenda wangemshikaka tu . LAkini ya ujerumani wanaifanya kwa kina kwa mi-computer ya uhakika.

Kuwa na nyumba ndogo nafikiri kwa tanzania sheria yake ina halalisha tayari kuwa ni mke. Nafikiri Sheria ya Tz haizungumizi kuwa na nyumba dogo si maadili, bali nafikiri inasema ukiwa na nyumba dogo kwa kipindi fulani, kama miezi sita hivi tayari huyo ni mkeo.
 
Sasa ina mana kweli tangu tupate uhuru tumeshindwa kuwa na hospitali yenye vifaa vya kisasa,kiasi kwamba hata ukiwa na fatigue unapoteza imani na hospitali zote nchini?

Mbona wanasiasa wanapenda kuwatusi watanzania namna hii jamani? Halafu nakumbuka Dr.Slaa alivotaka mishahara ya wabunge ipunguzwe basi wabunge wote CCM na baadhi wa upinzani wakalalamika.Nina wasiwasi kama kweli wanasiasa wetu wa sasa wa CCM na wa upinzani kama kweli wapo kwa ajili ya wananchi

Ile misamaha ya kodi ,plus hela zote za EPA,chenji ya RADAR, hela za kuilipa RICHMOND nk hazingeweza kutuokoa ktk hii kadhia jamani?na bado kuna watu wanataka kuchangisha hela 50 billion kwa ajili ya kujikita madarakani bado

Hizi mbwembwe za kutibiwa nje ndo zinasababisha hata suala la kuwa na hospitali za kisasa lionekane sio urgent sana. Nitakapopata wanamapinduzi 12,tutaibadili Tanzania.Kwa sasa na kwa mfumo huu,hatuna future kama taifa
 
Hivi ni wapi Zitto Kabwe amesema ama amenukuliwa akisema kuwa anakwenda Ujerumani kutibiwa?

Omarilyas
 
Hivi hii mentality ya viongozi wa Tanzania kuwa wakiumwa kidogo tu wanaenda nje kutibiwa itaisha lini? Kwa nini asitibiwe kwenye ile zahanati yake kule Kigoma kaskazini.

Regards
 
Hivi hii mentality ya viongozi wa Tanzania kuwa wakiumwa kidogo tu wanaenda nje kutibiwa itaisha lini? Kwa nini asitibiwe kwenye ile zahanati yake kule Kigoma kaskazini.

Regards

Yawezekana wanaogopa wazee wa busara
 
Uandishi na Uhariri wa Tanzania unahitaji ukarafati wa hali ya juu. Huu ni mfano mmojawapo wa utoaji taarifa mbaya (bad reporting). Kwa majuma kadhaa nimekuwa nikifuatilia matukio ambayo nilikuwepo na kulinganisha na jinsi yalivyoripotiwa. Inaonekana kuna makosa ya kiufundi lakini pia kunakuwa na makosa ya makusudi kabisa yanayopelekea mtu ahitimishe kuwa mwandishi ama mhariri wake wana majungu. Ni hatari tukiendelea na utamaduni huu wa kutumia matukio yasiyohusiana, kama hili la kuumwa Bungeni na hilo la kwenda Ujerumani, kuuza magazeti. Kimantiki taarifa hiyo hapo juu haithibitishi kuwepo kwa uhusiano huo japo inahitimisha hivyo. Jamani tusome haya magazeti 'katikati ya mstari'!
 
Hivi ni wapi Zitto Kabwe amesema ama amenukuliwa akisema kuwa anakwenda Ujerumani kutibiwa?

Omarilyas

Amesema anaenda kuangaliwa Afya yake...huoni tatizo hapo mkuu?

Hili ni kosa kubwa sana,unajua viongozi wa opposition tunashindwa kufanya matendo tofauti na wa Old ruling Club CCM kisha tunaonekana sisi ni walele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom