Ukoloni wa Ujerumani Afrika

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,646
3,936
Mwaka 2021, baada ya zaidi ya miaka 100, Berlin ilikiri kufanya mauaji ya kimbari nchini Namibia.

Wakoloni wa Ujerumani waliwaua zaidi ya Waherero na Wanama 70,000 kati ya 1904 na 1908. Yanaelezwa kuwa ndio mauaji ya kwanza ya kimbari katika karne ya 20.

Rais wa Namibia, Hage Geingob alisema hivi karibuni, "serikali ya Ujerumani bado haijalipa kikamilifu fidia kwa mauaji ya kimbari iliyofanya katika ardhi ya Namibia."

Baada ya Ujerumani kukiri ukatili ilioufanya, iliipa Namibia kiasi cha pesa kama fidia. Ujerumani ilikubali kulipa zaidi ya dola bilioni moja.
"Kwa kuzingatia wajibu wa kimaadili na historia, tutaomba radhi kwa Namibia na vizazi vya waathiriwa," Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani wa wakati huo Heiko Maas alisema 2021.

Waziri huyo aliongeza kuwa nchi yake, katika kutambua mateso makubwa waliyopata waathiriwa, itaunga mkono maendeleo ya taifa hilo la Afrika kupitia mpango unaotarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.3.

Kiasi hiki kitalipwa kwa muda wa miaka 30 na kuwekezwa katika miundombinu, matibabu na programu za mafunzo kwa manufaa ya jamii zilizoathirika.

Ukoloni wa Ujerumani Afrika​

dc
 
FIDIA KWA UTU WA NINI? Km wamekiri nakuomba msamaha c inatosha.wajerumani walikuwa wakatili sna ndyo mana makolon yote yalinyanganywa bila kujua ilikua mpago wa MUNGU
 
Wazungu wanakili kuhusu ukoloni, na wa naomba msamaha na kutoa hadi fidia ila mwarabu hata kabla ya yeye kuhojiwa vile aliua indonegius wa africa ya kaskazini na kujimilikisha ilo eneo waislam weusi watakushukia kama Mwewe kabla ya kumhoji Mwarabu.
 
Back
Top Bottom