Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,554
- 1,382
NAIBU katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ametinga wilayani Kibaha kuwaomba wananchi kumuongezea nguvu bungeni kwa kuwachagua wabunge wengi kadri iwezekanavyo wa kambi ya upinzani ili kwa pamoja waweze kwenda kuibana serikali ili iweke mazingira mazuri ya maisha wa Watanzania.
Kuna tatizo kubwa hapa. Yaani mnataka kuniambia Zitto anafikiria kubaki UPINZANI bado? Kwa nini anataka wabunge wengi wa kwenda kuibana serikali? Hajajua bado serikali ijayo itaongozwa na CHADEMA, na CCM itakuwa upinzani? Tena itakuwa a discredited opposition party?
Tuko katika mabadiliko makubwa, na nategemea Zitto achague maneno yake vizuri zaidi. Mazoea yana tabu! Zitto, please catch up!