Zipi faida na hasara iwapo nchi itaacha kutumia pesa yake na kuamua kutumia dola ya Marekani?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,238
12,751
Argentina wamemchagua Javier Milei kuwa Rais wao mpya. Ni jamaa mwenye msimamo mkali wa kulia. Moja ya malengo yake ya kukabiliana na hali mbaya ya uchumi na mfumuko wa bei ni kuiua pesa ya Argentina(Peso), kuvunja benki kuu na kuanzisha matumizi ya Dola ya Marekani kama pesa rasmi ya nchi. Jamaa ni msomi wa uchumi hivyo bila shaka anajua anachokifanya.

Ni nini faida na hasara za nchi kuamua kuanza kutumia dola ya Marekani kama pesa ya nchi?
 
Kwa nchi maskini watu watakufa njaa , Dola hairuhusu manunuzi ya fungu la mchicha la Tsh 100 , labda uvunje kuanzia 2500 ambayo ndo kianzio cha Dola , huku chini uziachie silesile nawaza tuu 😁😁😁
 
Kwa nchi maskini watu watakufa njaa , Dola hairuhusu manunuzi ya fungu la mchicha la Tsh 100 , labda uvunje kuanzia 2500 ambayo ndo kianzio cha Dola , huku chini uziachie silesile nawaza tuu 😁😁😁
Sio kweli mkuu,Zimbabwe wanatumia usd, zar hadi pula na maisha yanaendelea, ningekua na mamlaka, mimi ningefutilia mbali noti zote, ningebakisha noti ya 100 tu (Zambia ni mfano mzuri, leo hii ukiwa na 1ZWK =104 tsh, hii ni craze)
 
Zimbabwe walipoamua kutumia Dola ya Marekani shida kubwa ipo kwenye matumizi madogo. Fikiria mkate ununie kwa Dola 10. DR Congo kinawatesa hichohicho, vocha ya dola 10 huwezi kupigia watu wawili, mmoja tu salio lishakata na mbaya kule hawana bando kama zetu. Maana kule Dola unatumia popote bila hata kubadilisha.
Hivyo tatizo kubwa ni kwa wananchi wa kipato cha chini
 
Kwani si tuondoe masifuri 3 kwenye fedha yetu ili fedha yetu nayo iwe na thamani.

Yaani 10,000/= iwe 10/= ziwepo na senti kama ilivyokuwa wakati tunapata uhuru
 
Uchumi wako utafanyiwa maamuzi na Benki Kuu ya Marekani (Federal Reserve).

Mambo kama riba yataamuliwa na nchi nyingine. Riba inaathiri upatikanaji wa pesa.

Kifupi hutakuwa na maamuzi kuhusu pesa zinazotumika katika uchumi wako.

Benki Kuu yako itakosa nguvu za kuwa mkopeshaji wa mwisho kwa benki nyingine,hii ni kazi muhimu ya Benki Kuu.
 
Back
Top Bottom