Zimamoto yatoa stika

Mimi nafikiri kuan umuhimu wa kuwa na chama cha wenye magari binafsui lol huu ni uonevu kabisa sasa uuziwe stika alfu 20 wakati ndani ya gari huna hiyo zimamoto stika ndo itazima moto ukitokea? hawa bwana naona ndio maana hawajazitangaza kama wanavyofanya wiki ya nenda kwa usalama ah mie ningegoma hadi wanipe maelekezo vizuri

Usiponunua faini yake ni ipi?

elfu ishirini, nadhani sawa na faini ya kosa lolote la usalama barabarani.
 
Watanzania Mbona tunaendeshwa kama watu wasio na mwelekeo?
kwanza hawa jamaa wa fire wameanza kutuchanganya kuhusu viwango halisi vya kulipia hizi stika za fire. Hii ni moja ya ishara kuu ya ufisadi.
Naomba kuuliza Tanzania kuna magari mangapi??
Tuelezeni basi haya mabilioni mnayokusanya ni ya nini?
Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali naomba ukae chonjo!!! Kuna kila dalili za ufisadi hapa!!!!
Watanzania!!! Mhhh!!!
 
Mkuu hata mi sijaelewaelewa. Jana trafic alinisimamisha akaulizia stika za fire. Kwa kweli nilipigwa na butwaa. Hizi stika hasahasa zina malengo gani? Stika za road licence, usalama barabarani, bima, TLB, Fire nk. kioo si kitajaa? Nilimwonyesha traffic yule fire extinguisher ambayo bado haijaeksipaya lakini yeye akang'ang'ania stika. Muhimu kipi pale, stika au fire extinguisher? Naungana mkono na wewe mlachake, hapa kuna harufu ya ufisadi kama ule wa ufungwaji wa vidhibiti mwendo.

Kuna mtu kafungua mradi hapo! Oroko Mangi!
 
Mkuu hata mi sijaelewaelewa. Jana trafic alinisimamisha akaulizia stika za fire. Kwa kweli nilipigwa na butwaa. Hizi stika hasahasa zina malengo gani? Stika za road licence, usalama barabarani, bima, TLB, Fire nk. kioo si kitajaa? Nilimwonyesha traffic yule fire extinguisher ambayo bado haijaeksipaya lakini yeye akang'ang'ania stika. Muhimu kipi pale, stika au fire extinguisher? Naungana mkono na wewe mlachake, hapa kuna harufu ya ufisadi kama ule wa ufungwaji wa vidhibiti mwendo.

Kuna mtu kafungua mradi hapo! Oroko Mangi!
Mkuu muhimu pale haikua stika wala fire extinguisher...muhimu ilikua ni yeye utamwacha vp?? Trafic wa bongo balaaa!!
 
Watanzania Mbona tunaendeshwa kama watu wasio na mwelekeo?
kwanza hawa jamaa wa fire wameanza kutuchanganya kuhusu viwango halisi vya kulipia hizi stika za fire. Hii ni moja ya ishara kuu ya ufisadi.
Naomba kuuliza Tanzania kuna magari mangapi??
Tuelezeni basi haya mabilioni mnayokusanya ni ya nini?
Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali naomba ukae chonjo!!! Kuna kila dalili za ufisadi hapa!!!!
Watanzania!!! Mhhh!!!
Acha kulalamika wewe!! hebu changia huko!!! we hujui kwamba EPA account haina kitu na mwakani ni General Election? Kwani hujui vyama vya siasa vinatakiwa kuwa creative kwenye kubuni miradi?! Usitake kuniambia kwamba hujui mkuu wa kaya na genge lake wanatakiwa kuwa na mkwanja wa kutosha wa kwenda kubomoa iliko CHADEMA!! changia wangu, changia!!! Inauma sana wangu, lakini hamna jinsi-changia!!! kwani hujui ilipita hadi bungeni?! Changia mlachake ili CCM nao wale chao!!!
 
Tar 04 Nov 2009, nikiwa maeneo ya kituo cha daladala mwenge, na-endesha gari kuelekea Posta, nikitokea Sam Nujoma, mara napigwa mkono, na trafiki POLICE!. Kama kawaida yao, nikaambiwa niegeshe kushoto!.

Mama weeeee!!. Mara anakuja trafiki POLICE wa Kiume, kwa bahati mbaya , sikuchukua namba yake. Fuatilia mazungumzo yetu hapo:

POLICE TRAFIKI (PT): Sticker ya fire iko wapi?

SISIMIZI: Sina!

POLICE Trafiki: Ndiyo tunawataka, watu kama ninyi!

Sisimizi: Kivipi?

PT: Huoni gari hiyo STK (Landcruiser) iko kwenye operesheni hii?

Sisimizi: Ok!

PT: Haya nionyeshe fire extingusher (Kifaa cha zima moto)

Sisimizi: Hiki hapa!

PT: Ok! Una habari kwamba jeshi la zima moto limepiga marufuku aina hii ya kifaa cha zimamoto na unatakiwa ununue za Powder za Kilo moja ,1kg?

Sisimizi: Sina habari!

PT: Ok! Sasa wewe, umekumbwa na oparesheni!

Sisimizi: Ok!

PT: Unaelewa faini yake?

Sisimizi: Sielewi!

PT: Ni TZS 20,000 + 20,000 ya kununua kifaa kipya!

Sisimizi: Ok! Lakini kwa bahati mbaya sikutembea na pesa hiyo yote, siku ya leo!.

PT: Ndiyo maana ya Oparesheni!. Haya lete TZS 5,000 nikuachie uchomoke kabla sijakuchomekea kwa watu wa fire brigedi!!.

Sisimizi: Ndg, unamaanisha rushwa?

PT: Hapana, namaanisha senti ya maji ya kunywa!. Fanya haraka kabla sijakuchomekea kwa mama (Askari wa jeshi la zimamoto wa kike)!. Ukitia mguu kwake hautoki!

Sisimizi: Poa nichomekee tu!

PT: (Kwa sauti kubwa) Afande, njoo umsikie huyu raia!, (anamwita askari wa kike wa zimamoto).

Askari Zimamoto (Wa kike): Umeshindwa kumalizana naye??. Chukua fomu hii (napewa fomu ya kujaza). Nenda kalipie pale kwenye STK (Landcruiser)!.

Sisimizi: (Nachukua fomu kwenda kulipia TZS 20,000 ya sticker, nakurejea kuibandika kwenye gari).

PT: Yaani umeingia gharama 20k kwa ubahili wako!. mbona, haujanunua fire extingusher?

Sisimizi: Nimeelekezwa kwenye gari, ninunue ndani ya muda mfupi ujao!

PT: (Anaachana nami na kuendelea na kamatakamata!!)

WITO: PCCB wamlike oparesheni za jeshi la zimamoto! Limeanza kuzima moto wa kupambana na rushwa!
 
Huu ni wizi mkubwa na serikali imekaa kimya. hivi hizi sticker za kuuzwa barabarani ndiyo zina zima moto? siku zote walikuwa wapi kuzuia fire extinguishers ambazo haziruhusiwi kuingia nchini, maana wananchi wamenunua na serikali imechukua kodi za hizo fire extinguishers zinazoitwa fake leo.

PCCB fanyeni kazi ya kukamata hao wala-rushwa haraka
 
Alafu hawa jamaa wanazo stiker feki wenye magari kuweni macho unapewa feki siku ingine wanakukamata wanakunyang'anya wanakuuzia original sasa lakini pesa unakuwa umesha toa.
 
Stika elfu 20!!, na mtungi pia ni elfu 20!!!! Jumla elfu 40!!!!!!!!kweli nchi hii haina mwenyewe. Kila kukicha wanakuja na jipya, na kwakuwa uchaguzi umekaribia tutaona mengi.
 
mtoe way forward, kama vp tuandamane. na kwa jinsi nilivyomiss kunji, i will be glad.
 
Je mnajua kuwa Makao makuu yenyewe ya zima moto pale Ushirika building hakuna vifaa vya kugundua na kuzimia moto vya kisasa (fire detection and fighting equipment). Jengo limeshaungua mara nyingi. Kweli nyani haoni kundule maana walikuwa wanatakiwa kuanza kwenye ofisi zao.

Huu ni mradi tu, hakuna lolote
 
hizo stika ni muhimu sana...
mnataka mpaka watu wangapi wafe kwa moto ndo muone umuhimu?
unajua wabongo mmezowea kuendeshwa kwa matukio!
nunueni bila kelele bana, ni kwaajili ya faida yenu wenyewe...eboo!

hivi stika ndiyo inazua moto au mtungi wa gesi?!!!!! Au ukinunua stika unapewa mtungi wa gesi?!!!!
 
Back
Top Bottom