TASAC Yapongezwa Kwa Usimamizi na Udhibiti Makini wa Vyombo vya Usafiri Majini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Naibu Waziri Kihenzile aipongeza tasac kwa usimamizi na udhibiti makini wa vyombo usafiri majini

WhatsApp Image 2023-09-28 at 10.42.20.jpeg

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa usimamizi na udhibiti makini wa vyombo vinavyotumia usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa haraka wa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wadau mbalimbali hivyo kuwahakikishia usalama wao.

Akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya TASAC, Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kahenzile wakati wa ziara yake ya kujifunza, kujitambulisha na kukagua ofisi za Shirika hilo pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya udhibiti na usimamizi wa vyombo vya usafiri Nchini kikiwemo kituo cha Kuratibu shughuli za Utafutaji na Uokoaji Majini (MRCC) vyote vilivyopo Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Septemba, 2023.

WhatsApp Image 2023-09-28 at 10.42.19.jpeg


Mhe. Kihenzile ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miradi ya kimkakati nchini ikiwemo upanuzi wa bandari, ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo pia kuendelea kutafuta wadau binafsi wa kushirikiana nao kuziendesha hali itakayosababisha ujio wa meli zaidi Nchini na kuwahakikishia Maji ya Tanzania yako salama.

“Nimepata fursa pia ya kutembelea kituo cha kuratibu Shughuli za utafutaji na uokoaji majini, vituo hivi vinajengwa nchi nzima kwenye bahari zetu na maziwa hivyo niwahakikishie wadau na watumiaji wa vyombo vya usafiri majini, maji ya Tanzania yako salama, bahari zetu na maziwa yetu ni salama katika usafirishaji kwa njia ya maji tumieni fursa hii kuwekeza zaidi kwenye njia hii ya usafirishaji kwani ni rahisi, salama na ya gharama nafuu". Amesisitiza Kihenzile.

WhatsApp Image 2023-09-28 at 10.42.20(1).jpeg


Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali alimshukuru Naibu Waziri kwa kuchukua hatua ya kutembelea Taasisi zote zilizo chini ya Wizara na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Shirika ikiwemo uanzishwaji wake, mafanikio, miradi mbalimbali, changamoto pamoja na Mikakati ya kukabiliana nazo.
 
Back
Top Bottom