Zijuwe dalili za kabla ya kuachwa.

Mkwaruzo

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
563
98
Dalili ya mvua ni mawingu ingawaje baadhi ya wakati inaweza kunyesha bila ya hata kuonekana mawingu ya kuridhisha kama dalili yake. Na ni kama hivyo, kabla ya kuachwa huwa zipo dalili tofauti ambazo wengi wetu kwa kuona ni vitu vya kawaida, huwa hatuchukuwi tahadhari za mapema.
Baadhi ya dalili hizo ni hizi zifuatazo ila na wewe ongezea nyengine kwa kujuzana zaidi.

1. Mwenza kukosa raha mnapokuwa pamoja.
2. Kutopenda kutembelewa ikiwa mnakaa sehemu tofauti au kukutaka utowe taarifa kabla ya kumtembelea.
3. Kutoipa umuhimu mitoko yenu ya week end au mengineyo kama ilivyokuwa awali.
4. Kuanzisha majibu ya mkato.
5. Kukujibu kwa kujiamini zaidi.
6. Kutozijibu text zako kwa wakati tofauti na ilivyokuwa awali.
7. Kupenda kuzima simu kwa muda mrefu bila ya sababu za msingi na kutoyajali mawasiliano.
8. Kwenda pembeni kupokea call iliyoingia au kwenda kujibu text.
9. Kuchukizwa na kuishika simu yake.
10. Kutojiamini mnapokuwa pamoja.
Hivyo zinapojitokeza ishara kama hizo ni vyema kuuimarisha upya uhusiano wako kabla hayajakukuta.
 
Aksante mwayego angalau utatusaidia kupunguza maumivu.....ila nadhani kuna wengine wanaamua tu ghafla bila warning wala nini..nakumbuka nyamayao alisema wake alimwacha ghafla bin vuuu..........tena jana yake tu alitolewa out kwa vicheko na bashasha....wakarudi na kuagana kwa mabusu moto moto kwa ahadi ya kuwasiliana kesho yake (mh hapa pa mabusu nimeongezea) halafu keshoye ghaaaah simu hazipokelewi, sms hazijibiwi kabla ya kulibwaga its over!!

Sasa sijui ni kushindwa kusoma alama za nyakati au kuna wanaoendesha hisia zai kwa reflex actions/thoughts.
 
kawaida nikiona hizi dalili,mapema namaliza mahusiano hata kama nimependa kupita maelezo,bora nikalilie mbele ya safari kabla mahusiano hayajafika pabaya zaidi
 
.....ila nadhani kuna wengine wanaamua tu ghafla bila warning wala nini..nakumbuka nyamayao alisema wake alimwacha ghafla bin vuuu..........tena jana yake tu alitolewa out kwa vicheko na bashasha....wakarudi na kuagana kwa mabusu moto moto kwa ahadi ya kuwasiliana kesho yake (mh hapa pa mabusu nimeongezea) halafu keshoye ghaaaah simu hazipokelewi, sms hazijibiwi kabla ya kulibwaga its over!!.

ya nyama yao ndiyo kama hayo ya mvua bila ya mawingu ila hayo siyo sana kutokea.
 
Jamani hii imenigusa sana
mpenzi wangu niliyempenda kwa dhati na nilidumu nae miaka 2 ndipo nilipoanza maandalizi ya kumwoa mara ghafla alianza kunionyesha dalili kama hizo!
Baada ya muda tuliachana na mpaka sasa nshazoea na nayachukia sana mapenzi!
thanx kwa kutupa alama hizo za nyakati,itamsaidia aliye na mpenzi kutambua njaa iliyoko mbele yake.
 
Umesema ukweli me mume wangu alikuwa hadi kuoga anaenda na simu ,sa ya kulala anailalia kwenye mto. Jioni kuanzia saa 1 hadi 4 anazima simu. Mwisho nililetewa kabinti ka form six kamefukuzwa kwao kana mtoto mchanga . Habari ikaishia hapo. Thanx kwa ujumbe mzuri.
 
Pole .. Kwanini usingesamehe yakaisha? Badala ya kuishia hapo?
 
Umesema ukweli me mume wangu alikuwa hadi kuoga anaenda na simu ,sa ya kulala anailalia kwenye mto. Jioni kuanzia saa 1 hadi 4 anazima simu. Mwisho nililetewa kabinti ka form six kamefukuzwa kwao kana mtoto mchanga . Habari ikaishia hapo. Thanx kwa ujumbe mzuri.

Chetuntu, hebu nipe mwongozo wa hiyo past tense kwenye red hapo..........

Na hapo kwenye bluu pia panahitaji ufafanuzi, kabla sijaanza kufanya logistics flani hivi............
 
Nadhani hizi ni dalili za mtu ambae ameshakupatia msaidizi/mtu wa kuchukua nafasi yako zaidi kuliko anaetaka kukuacha tu.Katika hali ya kawaida mtu anaetaka kukuacha kwa sababu nyingine tofauti na kupata anaemuona bora kuliko wewe hatakua na haja ya kuficha simu au kuikumbatia kama mtoto.Ila wa kuogopwa ni wale ambao leo mnacheka na kufurahi alafu kesho unaambiwa bye bye.Hii ndo hua inawafanya watu wachanganyikiwe maana bila dalili huwezi kujiandaa unakua hukutegemea!
 
Aksante mwayego angalau utatusaidia kupunguza maumivu.....ila nadhani kuna wengine wanaamua tu ghafla bila warning wala nini..nakumbuka nyamayao alisema wake alimwacha ghafla bin vuuu..........tena jana yake tu alitolewa out kwa vicheko na bashasha....wakarudi na kuagana kwa mabusu moto moto kwa ahadi ya kuwasiliana kesho yake (mh hapa pa mabusu nimeongezea) halafu keshoye ghaaaah simu hazipokelewi, sms hazijibiwi kabla ya kulibwaga its over!!

Sasa sijui ni kushindwa kusoma alama za nyakati au kuna wanaoendesha hisia zai kwa reflex actions/thoughts.

Last edited by MwanajamiiOne; Today at 03:01 AM. Reason: Mi sijui bana...........kwani we hukuona ka nilikosea spelling bana?

Mjukuu hapa ulikuwa unamjibu nani?

Marunyagi bana! Dah!
 
Chetuntu, hebu nipe mwongozo wa hiyo past tense kwenye red hapo..........

Na hapo kwenye bluu pia panahitaji ufafanuzi, kabla sijaanza kufanya logistics flani hivi............

Ridhika na ulichonacho...utakufa siku si zako.Alafu ukichukua wote wajukuu zako wa kiume wataenda wapi?
 
Jamani hii imenigusa sana
mpenzi wangu niliyempenda kwa dhati na nilidumu nae miaka 2 ndipo nilipoanza maandalizi ya kumwoa mara ghafla alianza kunionyesha dalili kama hizo!
Baada ya muda tuliachana na mpaka sasa nshazoea na nayachukia sana mapenzi!
thanx kwa kutupa alama hizo za nyakati,itamsaidia aliye na mpenzi kutambua njaa iliyoko mbele yake.

Pole sana kwa yaliyokukuta lakini inatakiwa usiyachukie mapenzi.
 
Back
Top Bottom