Salaam, Shalom,
Itakumbukwa kuwa, uteuzi wa Katibu Mwenezi wa CCM, ulifanyika siku ya utiaji Saini kati ya Serikali na Kampuni ya DP World, hatujasahau Bado!!!
Hivi sasa tunaona ziara na misururu mirefu ya magari yakiambatana maeneo mbalimbali nchini, viongozi wa chama,akiwamo Katibu Mwenezi, wanapita wakisema wanatatua kero za wananchi.
Tatizo la mfumuko wa Bei za bidhaa nchini, una mahusiano ya moja kwa Moja na Bandari yetu ya Dar es Salaam maana shehena zinapita pale kwenda Kwa wananchi Nchi nzima.
Tuliambiwa Kwa mbwembwe kuwa, ujio wa DP World utasaidia uharaka wa upakuaji wa mizigo bandarini na kupunguza mfumuko wa Bei za bidhaa nchini.
Nchi yetu inakabiliwa na upungufu wa Sukari na simenti na bidhaa zingine muhimu nchini, tungetegemea uwepo wa kampuni hii, ungewezesha wafanyabiashara ufaulishaji wa mizigo Kwa haraka kuliko mwanzo.
Mizigo imezidi kuchelewa , na siku za Kutoa mizigo bandarini zimeongezeka Badala ya kupungua ilhali kampuni hii tayari imepewa mkataba wa utendaji.
Viongozi Walio katika ziara mbalimbali, watueleze hatua zinazoendelea kufanywa na kampuni hii kuongeza ufanisi wa Bandari yetu kupunguza Bei za bidhaa nchini Kwa kusaidia mizigo ya wafanyabiashara Kutoka haraka bandarini.
Ikiwa wapo wanaoona harakati zozote za kampuni hii hapo bandarini Kwa sasa watujuze.
Karibuni🙏