= waliofilisi
Waliofilisi ni wale wale waliofanya maamuzi ya kijinga ya kudhulumu (taifisha) na kuwakabidhi watu wasiojuwa kuendesha viwanda.
Naam, yalianza lini? msome Ludovick Utuoh kwa majibu sahihi.
Makosa yalifanyika kwenye misingi ya utawala, njia sahihi zimechukuliwa na hiyo misingi mibovu tuliyoirithi imebomolewa na ndiyo maana hutaona Serikali ikijenga tena kiwanda cha Umma, tumeondoka huko kwenye uozo.
Ni kweli siwezi kuona Serikali ikijenga tena kiwanda cha Uma, ila nitaendelea kuona series ya wizi wa fedha za umma bila kuruma. Kwa miaka michache tu iliyopita nimeshuhudia TTCL ikiwa mahututi kwa wizi, Meremeta, Kagoda, IPTL na ESCROW. Nasubiri wizi mwingine kupitia BVR, umeme vijijini na Internet mashuleni uanikwe. Naamini nitaendelea kushuhudia na kuchukua hatua kupitia anduku la kura. Naamini kuna siku kura zitatosha, na itakuwa mwisho wa kushuhudia wizi, uvivu, ubadhirifu, uongo, majungu, uchawi, upumbavu na ujinga.
Nitaendelea kushuhudia hatua za maendeleo ya kasi huku kwa upande mwingine laana ikiendelea kuwatafuna wanaowadhulumu kipindi hiki. Wakati huo, watawala wa sasa ambao kwa kipindi hicho hawatakuwa madarakani tena, mali zao zote zitarejeshwa mikononi mwa wamiliki (umma).