Rais wa Poland kuwasili nchini kwa ziara ya siku mbili tarehe 8-9 February 2024

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
poland.jpg

Rais wa Jamhuri ya Poland, Andrzej Duda​

Rais wa Jamhuri ya Poland, Andrzej Duda anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kuanzia tarehe 8-9 February, 2024. Mh. Duja atawasili nchini tarehe 8 February, 2024 akiambatana na mwenza wake Bi. Agata Kornhauser-Duda na atapokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. January Makamba na viongozi wengine waandamizi wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Ziara hii ni ya kwanza kwa ngazi ya Rais kutoka Poland kuja nchini na inalenga kuimarisha ushirikiano wa uwili kati ya Tanzania na Poland. Kwa takribani miaka 62 Tanzania na Poland zimekuwa zikishirikiana katika miradi ya maendeleo kwenye sekta ya kilimo, fedha hususan masuala ya kodi, viwanda na biashara, utalii, elimu, usafiri, tiba za mifugo, afya na maji. Xiara hii pia inalenga kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kupitia sekta za ulinzi na usalama, nishati, madini, ulinzi wa mitandao, utamaduni na Uchumi wa buluu.

Tarehe 9 Februari, 2024 Mh. Duda atapokelewa rasmi Ikulu-Dar es Salaam na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwa na mazungumzo ya faragha, mazungumzo rasmi yatakayohusisha wajumbe wa pande zote mbili na baadaye watazungumza na waandishi wa habari kuelezea waliyokubaliana katika mazungumzo hayo.

Aidha, Mh. Rais Duda pia anatarajia kutembelea mradi wa matibabu yah arura katika Hospitali ya Aghakan, Dar es Salaam ambapo Serikali ya Poland imetoa msaada wa Dola za Kimarekani 1,136,703.71 kufadhili mradi huo. Mradi huu unalenga kutoa msaada kwa sekta ya matibaubu na kusaidia elimu ya wahudumu wa afya katika mkoa wa Dar es Salaam.

Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

Screenshot 2024-02-08 224406.png
 
Tuna mkatibisha sana.

Uzuri wa Tanzania inashirikiana na nchi ngingi zenye maendeleo makubwa, ushirikiano wa zaidi ya miaka 50 lakini maendeleo ya taifa letu hili hayaakisi mashirikiano hayo.
 
Back
Top Bottom