Ziara ya Kansela wa Ujerumani nchini China yaonyesha juhudi za Ujerumani kurejesha uhusiano wa awali wa na China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,014
1,039
1713409036803.png

Konsela wa Ujerumani Olaf Scholz hivi karibuni alifanya ziara nchini China ambapo alitembelea Manispaa ya Chingqing, ikiwa ni kituo chake cha kwanza katika ziara hiyo ya siku tatu. Hii ilikuwa ziara ya pili ya Scholz nchini China tangu ashike wadhifa huo, ziara ambayo inaleta ishara nzuri inayoonyesha kuwa, Ujerumani inafanya juhudi za kivitendo kujenga na kupanua uhusiano wa kimkakati na China.

Scholz ni kiongozi wa kwanza wa nchi za Magharibi kufanya ziara nchini China kwa mwaka huu, hivyo ziara hii inamaanisha kuwa, ule wito wa Marekani wa ‘kuepuka hatari’, ambao baadhi ya nchi za Magharibi zinauzingatia, unawekwa pembeni kwa ushirikiano ni muhimu na nchi za Ulaya zinajitahidi kudumisha uhuru wa sera.

Ziara hii inafanyika wakati kuna mvutano katika uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya baada ya Ubelgiji kuongeza mvutano wa kibiashara na China katika sekta mpya ya viwanda. Ziara hii inatarajiwa kusaidia kukabiliana na mivutano hii na kupunguza hatari ya ‘vita ya kijani ya kibiashara,’ na kuleta uwiano kwa sauti zinazoipinga China ndani ya Umoja wa Ulaya, na hivyo kufanya uhusiano kati ya China na Umoja huo kuwa katika njia tulivu na yenye afya.

Wawakilishi wa uchumi na kampuni za Ujerumani wanatarajia ziara hiyo itakuwa na matokeo mazuri kwa kuwa pande zote mbili za Ujerumani na China zimeonyesha wazi matakwa ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati yao.

Akizungumzia ziara hiyo, mkurugenzi mkuu wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Ujerumani nchini China, Maximilian Butek amesema, matokeo muhimu yatakuwa ni kuanzisha msingi imara kwa ajili ya ushirikiano na mabadilishano, na kwamba wanatarajia kuwa mawasiliano ya watu na watu katika masuala mbalimbali, na maelewano katika masuala muhimu yanaweza kutimizwa.

Mji wa Chongqing, ambao ni kituo cha kwanza cha ziara ya Scholz, ni kituo muhimu kwa safari za treni za mizigo kati ya China na nchi za Ulaya, na hivyo ziara hiyo inafungua njia kwa ushirikiano wa baadaye wa pande mbili katika sekta muhimu ya miundombinu.

Mtafiti mwandamizi katika Taasisi ya Elimu ya Ulaya katika Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China, Sun Yanhong anasema, Chongqing ni maskani ya uwekezaji mkubwa wa Ujerumani nchini China, hivyo ziara hiyo pia inaweza kuwa ni jibu la wito wa jamii ya wafanyabiashara wa Ujerumani, ambao wanatarajia kuimarisha maingiliano ya kiuchumi na China.

Sun anasema, wakati Ujerumani inakabiliwa na changamoto kadhaa katika lengo lake la matumizi ya nishati ya kijani, ni wazi kuwa watengenezaji wa magari wa Ujerumani watatumia ziara hiyo kuimarisha uratibu na wenzao wa China, nchi ambayo inaongoza katika utengenezaji wa magari yanayotumia nishati mpya.

Jamii ya wafanyabiashara wa Ujerumani nchini China pia wanaichukulia ziara hiyo kama Konsela Scholz kuleta mtazano wa uwiano kati ya sauti mbalimbali katika serikali yake inayoundwa na vyama vitatu na kuimarisha uhusiano wa kina na China kupitia mabadilishano ya wazi na majadiliano. Jamii hiyo inasema ziara hiyo inaendana na pingamizi lao kwa baadhi ya wanasiasa wa Ulaya wanaochochea hatua ya ‘kuepuka hatari,’ na badala yake, wanasisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pande zote kati ya China na Umoja wa Ulaya.

Kuhusu utawala wa dunia, wachambuzi wanasema China na Ujerumani pia zinaweza kujadiliana kuhusu kufanya kazi pamoja katika malengo ya pamoja kama usalama wa nafaka, maendeleo endelevu na kilimo cha ikolojia.

Jambo moja muhimu katika ziara hii ni jinsi nchi hizi mbili, China na Ujerumani, zitakavyojadili na kushughulikia kile kinachoitwa na Marekani na wanasiasa wa Umoja wa Ulaya, “uzalishaji kupita kiasi” kuhusu bidhaa za nishati mpya zinazotengenezwa na China.

Naibu meneja mkuu na Ofisa Mwandamizi wa Uhasibu kwa kampuni ya Karcher China, Rainer Kern, anasema ushindani wenye afya ni muhimu, lakini wito wa kujitenga na kuepuka hatari hauna maana kwa sababu kuna haja ya kufanya kazi kwa pamoja. Ametolea mfano wa mazingira, na kusema hakuna nchi moja inayoweza kutatua tatizo hilo, na ni lazima kushirikiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa karibu kwenye masuala kama hayo.

Mwaka jana, uwekezaji wa moja kwa moja wa Ujerumani nchini China ulifikia rekodi ya juu katika historia ya Euro bilioni 11.9, sawa na dola z kimarekani bilioni 12.7, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.3 ikilinganishwa na mwaka 2022. Wakati huohuo, China pia ni mwenzi mkubwa wa biashara wa Ujerumani kwa miaka minane mfululizo.

Kama alivyosema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, China na Ujerumani zimenufaika sana na maendeleo ya kila upande, na hivyo kuchangia pakubwa ustawi wa watu wa nchi hizo mbili. Amesema nchi hizo mbili zimeongoza uhusiano wa China na Umoja wa Ulaya katika mwelekeo wa utulivu na endelevu na kuongeza zaidi utulivu duniani.
 
Back
Top Bottom