Afrika inapaswa kutumia fursa zinazotolewa na China hasa kwenye masuala ya anga za juu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,021
1,043
1714626759230.png

Hivi karibuni China ilirusha chombo chake cha anga ya juu cha Shenzhou-18, ambacho kilibeba wanaanga watatu wakiwemo Ye Guangfu, Li Cong na Li Guangsu. Kabla ya kurusha chombo hicho Alhamis ya tarehe 25 Aprili, China ilisema itahimiza ushiriki wa wanaanga wa kigeni katika safari zake za kituo chake cha anga ya juu.

Ili kuweza kutimiza azma hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Anga za Juu la China (CMSA), Lin Xiqiang alisema China itaongeza kufanya utafiti zaidi kwa ajili ya kuwezesha ushiriki wa wanaanga hawa wa kigeni kwenye safari zake za anga ya juu.

Mwaka jana kupitia Bw. Lin Xiqiang, China ilitoa mwaliko duniani ikizikaribisha nchi na kanda zote zenye nia ya kutumia kwa amani anga ya juu kushirikiana nao na kujiunga kwenye safari za anga ya juu za China, ikiwa ni pamoja na kuwajumuisha wanaanga hao wa kigeni kwenye safari za kutua kwenye mwezi pale vigezo muhimu vitakapofikiwa.

Wakati China inafungua milango yake kukaribisha wanaanga wa nchi za nje kushiriki kwenye programu yake ya safari za anga ya juu, je nchi za Afrika zimejipanga vipi ili kuhakikisha nazo zinatumia fursa hii azimu kama ipasavyo?

Huko nyuma nchi za Afrika ziliathirika sana na mifumo na miundo ya kikoloni iliyowekwa wakati huo, na kufanya nchi hizi zisiweze kudhibiti maliasili zao na rasilimali watu. Ukoloni ulizifanya nchi hizi kuzingatia zaidi nguvu kazi, malighafi na mazao ya kilimo ambayo yalihitajika na mabwana wao wa kikoloni, na kushindwa kuzingatia kufanya tafiti za kisayansi na kuleta maendeleo yao, haswa katika masuala ya nyuklia, anga ya juu na bahari. Hadi mifumo ya elimu iliyokuwepo pia ilikuwa ni kwa ajili kukidhi mahitaji ya mabwana wa kikoloni. Kwa hiyo, anga za juu halikuwa suala linaloshughulikiwa na nchi za Afrika.

Baada ya mataifa haya kuwa huru kwa miongo kadhaa, yalipaswa kwa namna fulani kudhibiti rasilimali watu na fedha. Hotuba iliyotolewa na Kwame Nkrumah wa Ghana katika uzinduzi wa Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) mwaka 1963 inatukumbusha vizuri namna maendeleo na ustawi wa Afrika unavyohitaji sayansi na teknolojia.

Tukiangalia maisha yetu ya kisasa kweli yanategemea sana bidhaa na huduma za anga. Ili kupatikana kwa huduma hizo, kwa sasa nchi kadhaa wa kadhaa za Afrika zikiwemo Misri, Afrika Kusini, Algeria, Nigeria, Morocco, Ghana, Kenya, Rwanda, Angola, Sudan, Ethiopia na Mauritius zimeanza kurusha satelaiti katika obiti. Lakini kurusha satellite pekee haitoshi, kwakuwa tunafahamu kwamba anga ya juu ina fursa nyingi sana. Kwa maana hiyo kuandaa wanaanga watakaokwenda kwenye safari za anga ya juu kufanya uchunguzi zaidi pia ni jambo linalopaswa kutiliwa maanani na kupewa kipaumbele.

Laiti kama nchi za Afrika zingekuwa na vyombo vyake vinavyorushwa kwenye anga ya juu pamoja na wanaanga wake, basi bila shaka zingeweza kutumia fursa hii iliyotolewa na China ya kukaribisha wanaanga wa kigeni kushiriki kwenye safari zake, na kupata kujifunza zaidi kupitia kwa wanaanga wenzao wa China.

China inapanga kutimiza azma yake ya kutua kwenye mwezi ifikapo mwaka 2030, huku ikiendeleza kithabiti kazi ya utafiti na maendeleo ili kuhakikisha lengo hili linafikiwa kama ilivyopangwa. Mbali na wanaanga wa nchi za kigeni kwenda kwenye safari za kituo cha anga ya juu cha China, ushirikiano huu pia utajikita katika masuala ya uendelezaji na majaribio ya upakiaji wa taarifa za anga ya juu, usimamizi wa mazingira ya anga ya juu na elimu ya sayansi ya anga ya juu kwa vijana.
 
Back
Top Bottom