Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

logic sina, ila nilichosema from the beginning kwamba tokea lini mafisadi wakachunguza mafisadi wengine bila ya wao kuchunguzwa ? kwa kuwa huyo karamagi alifanya large scale theft ndio awe tofauti na huyo dr. slaa ambaye ameiba kidogo kidogo lakini mara nyingi ? dont ask where this came from, someni post ya kwanza na main aim ya hii thread utajua !

once a murderer always a murderer ! once a fisadi always a fisadi !
 
Mtaweza vipi kuwazomea?.. jamani ebu twende mbele tukitazama nyuma.. tusiogope kugeuka mawe..
hawa jamaa wanasumbuliwa na njaa tu muhimu ni kuwapuuza kwani madai yao ni ktk comedy. Lengo la michezo kama hii ni kuwachekesha watu.
Nakuombeni yachukulieni mawazo yao kama kichekesho mtaona starehe zaidi ktk nyoyo zenu... unless kama nanyi mnafikiria kuwa walikuwa na points za maana ambazo inabidi watu wazikubali. Beside that hawa ni wachekeshaji ambao kama sikosei wamewahi kumuiga El akizungumzia ndege kupaa!
 
Kwa hiyo kutokana na wimbo au mchezo wa kuigiza wa ze commedy ume hitimisha kuwa Dr. Slaa ni mfisadi. Ingawa siwezi kukataa au kukubali kama yeye si mfisadi, lakini hakuna point inayonifanya nihitimishe hivyo (kuwa Dr. Slaa ni mfisadi). Ze commedy, and the like should come with a detailed report, like that, which conviced me that, mafisadi have a case to answer.

Wandugu, hebu niwaambie kitu ambacho labda wengi you are far and it will take a decade for an ordinary Tanzanian to understand; that why i say you should play with logic. most of the money lost through compuni hewa, was a means of the government ruling elite to launder the money to be used in the general elections. Massive cash was used in that election, and there was a very systematic arrangement with CCM and the sitting government to plan how to launder this money.

Bet, the opposition have all the references! They are waiting when the time is ripe. Balali, mgonja, or any in the list were used, and everybody knows, nobody will go to jail, and believe me; the government is now working with Brela, BOT, to clean all evidence existing in the government. The only issue, what they will get hard time to clean, is those accounts and registrations offshore. But all will depend on the amount of transaction.

Don't ask me where I got this, is up to you to speculate.
 
Mkandara umeongeA Pointi kubwa sana, hawa watu(ze comedy) wana lengo la kuchekesha au kuburudisha kwa kutumia sanaa ya maonyesho, akiigizwa lowasa kwa nini iwe sawa lakini akiigizwa Slaa inakuwa Nongwa?

Tuache kuwa biased kwa kudhani kwamba wanaotakiwa kuigizwa ni viongozi wa ccm na serikali pekee na wala si wapinzani.

Isitoshe ze Comedy sidhani kama waliziponda hoja za Msingi za Slaa, nabadala yake naamini walimuigiza Slaa mwenyewe , sasa hapo ugomvi uko wapi?

Tusiue fasihi kwa sababu ya itikadi za kisiasa!.

Halafu hao wanaoamini kwamba Ze comedy wamefanya kosa la kiteknikali, kwa nini isiwe kwamba wao ndo wamechukua advantage ya kiteknikali, kwa sababu Mwanasiasa dokta Slaa sasa hivi ndo yuko Chati katika masikio ya watanzania wengi, sasa kwa nini ze comedy wasitumie nafasi hiyo kufanya vitu vyao?

Jamani mkuki kwa Nguruwe eh! kwa binadamu.....
 
Kuigiza ni professional kama alivyo Engineer,Lawyer na nyinginezo. Kama professional kuna jinsi ya kuigiza na ujumbe ukafika bila kuathiri muhusika. Ili lilifanyika kwa Edward, na ilitakiwa ufikirie ili uweze kujua wanamuigiza nani.

Lakini kitendo cha kumtaja kabisa jina, na kutoa maneno ambayo hayana ushahidi ni kuvuka mipaka ya taaluma yao.

Lakini wanaelekea kujimaliza maana nakumbuka zamani hata watoto wadogo wamekuwa wakikimbilia TV wakati wa kipindi. Juzi kwa sababu wameongea siasa hata watoto ukiwauliza Ze commedy wamezungumzia kitu gani hakuna anayependa kusikia kitu hicho.

Kwa wale walioko Dar es Salaam na mikoa mingine jaribu kufanya utafiti, wamekera watu kweli maana wamepoteza maana ya mchezo wao.

Hawakuwa tofauti na kingunge ambaye watu wanasema inawezekana umri umepita ndiyo maana anaongea vile.
 
i dont have to speculate anything maana najua kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho ! lets not act now kama hatujui ni kiasi gani CUF walikuja kwa nguvu kipindi kile hadi kutishia uhai wa ccm, na sasa wako wapi ? kumbuka angalau hapa yanayozungumzwa ni maslahi ya taifa, lakini pia kuna mambo binafsi ambayo wanasiasa wa pande zote mbili wameyaweka mbele, esp. CHADEMA ! yes CHADEMA !

Therefore, sidhani kama mimi au mwanaccm yoyote yule mwingine anatishwa na hizi kelele chache za wapinzani, zitaisha tu !

Najua wengi mtanishangaa na kunijia juu, but hey come on !
 
Najua wapo watakaoniunga mkono na watakao nipinga. Kwa sababu wananchi hawana pesa ya kuwanunua Ze Comedy kama wafanyavyo akina Rostam Aziz silaha pekee tuliyonayo ni kuwazomea na kutoangalia kipindi chao. Comedy Ziiii! Comedy wanawatete mafisadi!!1 Kwanini hao ze Comedy wasioneshe pesa za wananchi zinavyoliwa? kwanini wasioneshe wagonjwa wanaolala chini sakafuni na wengine wanalala kitanda kimoja watu 4? Kwanini wasioneshe ubovu wa bara bara zetu na reli yetu wakati watu wanajenga mahekalu huko mbezi?

Ze comedy wasipoangalia watakufa natural death. Hawa ze Comedy hawajui wananchi ndio wateja wao wakuu? Jamani kwa wale wanaonieunga mkono lets us tuwakomeshe hawawanasiasa njaa Ze Copmedy.

Kwa uelewa wangu mdogo, "Ze Commedy" ni Video Version ya Magazeti ya Udaku";

Sijawahi kumuona Serious Individual/Organisation yoyote iliwahi kwenda pale Maelezo kupinga mambo ya Ki-Udaku...

Sasa kama ninyi mnataka kufanya hivyo ati kuwazomea au juhudi zozote zinazofanana na hizo,,, mimi nitawaona ninyi ndio mnamatatizo makubwa kuliko hao "Ze Commedy" Ama kweli JF inakosa muelekeo...

Hivi ni kwa kuwa mpendwa wenu ame-be-hurted,,, walivyokuwa wanamuiga Mudhihir ilikuwa poa!!!

Du! Yes binadamu ana mapungufu makubwa sana...

Haya tafuteni mbinu za kuwazomea "Ze Commedy"
 
Kwa anayebisha kuhusu tuhuma hizi dhidi ya Slaa nasema: naweza kumtafuta mtu aliyeshuhudia "live" Padri Slaa akimla uroda chnagudoa (ambaye baadaye alikuja kumuoa baada ya kuacha upadri) kwenye nyumba ya Dayosisi pale Ngarenaro. Hiyo ni moja. Pili, Slaa alianza shughuli ya kujenga nyumba yake pale Kijitonyama akiwa bado ni padri na tena alimtumia mkandarasi wa TEC. Hii habari ilichapishwa hata kwenye gazeti la "Kiongozi" enzi hizo.
 
Therefore, sidhani kama mimi au mwanaccm yoyote yule mwingine anatishwa na hizi kelele chache za wapinzani, zitaisha tu !

Mara nyingi Mafisadi huwa wanataka kuwakatisha tamaa watu wanaoona kuwa wanataka kufuatilia mambo yao.

maswali yaliyoulizwa kwa mafisadi hayakutaka mtu mwenye shahada kuyajibu. Yote yana majibu yake hila majibu inawezekana ndio ufisadi wenyewe.

Swali mojawapo kwanini kampuni ya serikali imesajiriwa ktk nchi ya kigeni? Swali la pili serikali ina watoto?

Jibu lake hata mtoto mdogo akijibiwa kuwa: Tafuta lingine maana naona unataka kuleta fujo, ni kichekesho kabisa! au hukufaa kuwa kiongozi.(kwa nini hata kama ni mkuu kiasi gani usizomewe?)

Najua yatapita kama unavyosema ila alama itabaki, na tayari bao la kisigino limeingia na kaburi limechimbwa.

Na hapo ndipo tunagundua kwa nini Tanzania bado ni masikini
 
Sasa kama ninyi mnataka kufanya hivyo ati kuwazomea au juhudi zozote zinazofanana na hizo,,, mimi nitawaona ninyi ndio mnamatatizo makubwa kuliko hao "Ze Commedy" Ama kweli JF inakosa muelekeo...

Hivi ni kwa kuwa mpendwa wenu ame-be-hurted,,, walivyokuwa wanamuiga Mudhihir ilikuwa poa!!!

Du! Yes binadamu ana mapungufu makubwa sana...

Haya tafuteni mbinu za kuwazomea "Ze Commedy"
Maneno yapo juu ya mstari!
 
Wakati Ze Comedy wanamuigiza Lowassa, Mwapachu, Karamagi, Tibaigana wazomeaji mlikuwa wapi?

Je hamkuona wakati wanaigiza mkataba wa Buzwagi ulivyosainiwa Hotelini? Je wazomeaji mlikuwa wapi?

Hivi Slaa ana immunity ya kutoigizwa? acheni usanii wenu, mwiba ulioingia ndio hapo hapo utakapo tokea!
 
Ze Comedy wanatumia haki yao ya msingi kama wasanii.

Kama hamkuwazomea wakati wanawaigiza akina Lowassa, mkiwazomea sasa nyie mnakuwa hamjui demokrasi mnayoililia kuliko hata hao Ze Comedy.

Kama huridhiki na wanachoonyesha, tafuta kikundi kingine ambacho unaona kinakufaa.

Demokrasia ni pamoja na kulinda kwa nguvu zote haki ya mbaya wako.
 
The next day baada ya kuharibu via TV nimtumia email program manager na kumwambia"vijana wako wameanza kuganga njaa vibaya watapoteza umaarufu soon na kuambulia a natural death"
Ninachoshangaa wanajua fika wananchi wana jazba na upotevu wa mali zao pamoja na ufisadi alafu wao wanautetea kwa kumponda Dr Slaa.
Fedha kitu kingine wajameni vijana wamenunuliwa bila kujau impact yake.
Mbaya zaidi pale nilipokuwa bar kila mtuu akangaka"oohhh ccm nao mpaka ze comedy???????!!!!!!!!!!".
Wasipoangalia umaarufu wao utatoweka kama kichaka kikavukilicholipuliwa kwa moto wa petroli
 
tatizo siyo kwamba hao ze comedy wamemsema nani! tatizo ni kwamba wamemsemaje! There is humour in every thing, if you have the sense of humour you will be able to see it, but if you dont have it, you will think it is an insult!.

Kama ze comedy walishindwa kutumia sanaa ya kutosha kumuigiza slaa, basi kosa ni lao, lakini kama walifanikiwa kuburudisha watazamaji basi waliofanikiwa ni wao.
 
Unajua haingii akilini watu kuwarubuni vijana wetu wa ze comedy kwa vijela vya apa na pale eti kumzima Dr Slaa.
Nawasihi hao vijana wasigange njaa kiivyo wataja poteza umaarufu.
Raisi mwenyewe anajikanyaga kujibu izo hoja ze comedy ndo wanajfanya vimbelembele kujibu hoja kwa kumchafulia jina Dr Slaa.
Nilikuwa bar while nawatch ze comedy unajua kila mtu bar akasema"CCM hadi the comedy wameinunua"
Walai vijana watapoteza umaarufu soon kama wataendekeza izo senti ambazo zitawamaliza a natural death.Wananchi bado wana hasira na mali zao na hayo marushwa wao wanajifanya wanadilute from today kheri waitwe Ze CCM.
 
The next day baada ya kuharibu via TV nimtumia email program manager na kumwambia"vijana wako wameanza kuganga njaa vibaya watapoteza umaarufu soon na kuambulia a natural death"
Ninachoshangaa wanajua fika wananchi wana jazba na upotevu wa mali zao pamoja na ufisadi alafu wao wanautetea kwa kumponda Dr Slaa.
Fedha kitu kingine wajameni vijana wamenunuliwa bila kujau impact yake.
Mbaya zaidi pale nilipokuwa bar kila mtuu akangaka"oohhh ccm nao mpaka ze comedy???????!!!!!!!!!!".
Wasipoangalia umaarufu wao utatoweka kama kichaka kikavukilicholipuliwa kwa moto wa petroli

..usiwe na wasi,kama wamechemsha watalinywa!

..nadhani ni vyema watazamaji wakaamua kuliko kuanza kuwahukumu sasa!subra!subra!pengine waliteleza au ndo hivyo fedha sabuni ya roho!

..hiki ni kipindi kinachochekesha watu kwa ku-make fun ya vitu vinavyowagusa,sasa kama wameisema vibaya ya slaa, reaction itatoka kwa watazamaji.

..tusizidishe siasa kwenye hili!
 
Mi naamini ni wazo zuri, na naamini mtoa mada hii anaposema 'kuzomea' ni moja ya tool inayoweza kutumika, na tunaposema tuwazomee haimanishi kwamba kwa kutumia computer yako tu bali kwa njia yoyote inayowezekana, e.g. SMS,Radio, direct kwa wale wanaokutana nao, ikiwa ni pamoja na kuwaambia 'wawe makini wasigeuze kipindi chao kuwa cha kisiasa na cha kutetea wahalifu' kwa kuwa wananchi wakikasirika itakua ndio mwisho wa kipindi chao, by the way, KAMA WANAZOMEWA MAWAZILI, WHO IS THE COMEDY!
 
Kwa anayebisha kuhusu tuhuma hizi dhidi ya Slaa nasema: naweza kumtafuta mtu aliyeshuhudia "live" Padri Slaa akimla uroda chnagudoa (ambaye baadaye alikuja kumuoa baada ya kuacha upadri) kwenye nyumba ya Dayosisi pale Ngarenaro. Hiyo ni moja. Pili, Slaa alianza shughuli ya kujenga nyumba yake pale Kijitonyama akiwa bado ni padri na tena alimtumia mkandarasi wa TEC. Hii habari ilichapishwa hata kwenye gazeti la "Kiongozi" enzi hizo.

Jokofu,
Hivi Slaa kula uroda changudoa ina uhusiano gani na wizi wa mabilioni yetu watanzania ya BOT and the likes?? c'on guys letus be serious!!!

Tukifungua kurasa za walauroda machungudoa/ wake za watu n.k.. nadhani halitasalia jiwe juu ya jiwe!!!!
 
kadaMpinzani,Kakindo,Mwakasege,JokofuKiwete,InterestedObserver,

Mwaka 1997 wakati wa kampeni za Ubunge Temeke, CCM waliibuka na kashfa ya Mrema na Mama Anjelina. NCCR nao kulipiza kisasi wakaja na picha za Ditopile na ma-girlfriend wake akiwa Mikumi loddging.

Mwaka 1995 Prof.Ibrahim Lipumba aliibuliwa "kashfa" kwa si Muislamu "safi" kwasababu inasemekana alivunja ndoa ya mtu. Hapa hapa jamboForums ukichambua posting mbalimbali utakuta kuna viongozi mbalimbali wa serikali wanatuhumiwa kutembea nje ya ndoa zao.

Sasa hapa naona hawa ZeComedy wameanza kujadili mambo ya CHUPI za watu. Mambo ya CHUPI hayabagui Chadema,CCM,au CUF, kama nilivyoelekeza hapo juu.

Mimi nadhani hawa ZeComedy wamefungua uwanja kwa Comedians wengine kuwajadili na kuwachambua wanasiasa. Mimi nadhani hiyo inaongeza ushiriki wa jamii ktk siasa. Hilo ni jambo zuri kwangu.

Suala la msingi hapa, na ninaamini wananchi wana busara za kutosha, ni kutafakari kati ya hizi kashfa zinazorushwa ni zipi zina uzito kushinda nyenzake.

Mfano mzuri ni Maraisi Clinton na Nixon wa Marekani. Wote walikuwa impeached. Sasa ni kwanini Nixon akaiacha Ikulu bila kujitetea mbele ya Senate? Je, ni kwanini senate iliamua kumvua "kitanzi" Clinton na kumuacha amalize ngwe yake ya uongozi?

Naomba kama Watanzania tujiulize ndani ya nafsi zetu maswali yafuatayo:-

1.Je, fedha zilizoibiwa na wana CCM kutokana na mradi wa OGL ni sawa na fedha anazotuhimiwa Slaa kuwaibia walemavu?

2.Je, hasara tuliyoingia kutokana na mikataba ya madini inalingana na hasara iliyoingia Kanisa Katoliki wakati Slaa akiwa Katibu wake?

3.Leo hii sidhani kama Slaa anaweza kugombea uongozi huko anakutohumiwa na walemavu au kanisa katoliki. Je, kwanini sisi tunawatetea hawa viongozi ambao wanafanya makosa kama yale ya Slaa na pengine hata zaidi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom