Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

Discussion in 'Sports' started by Asha Abdala, Oct 12, 2007.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HII IKAE KWENYE SIASA INGAWA ZE COMEDY NI BURUDANI

  Jana Masanja amemkandamiza LIVE Dr Slaa kwa kuigiza:

  Dr Slaa alifukuzwa upadri kwa sababu ya kutembea na mwanamke.

  Dr Slaa alifukuzwa upadri kwa sababu ya kula fedha za walemavu.

  Dr Slaa anapaswa kuondoa kwanza boriti yake ya ufisadi kabla ya kutazama wengine.

  Dr Slaa ametunga orodha ya mafisadi sio ya kweli kabisa.

  Dr Slaa aliwahonga waandishi wa habari ili wasiandike ukweli kuhusu kufukuzwa kwake upadri sababu ya mwanamke na kula fedha za walemavu.

  Masanja aliyakandamiza haya yote kama vile ni ukweli mtupu.

  KIPIMA BARIDI: Je, Ze Comedy walikuwa sahihi?

  Jinsi ya kushiriki kipima baridi, mpigie simu Meneja wa Ze Comedy Bwana Sekione Kitojo(Seki) kupitia 0787513633 kutoa jibu lako ama changia hoja yako hapa JF na kama unataka ujumbe umfikie mmiliki wa EATV bwana Reginald Mengi nitumie ujumbe kwenye [email protected]

  Asha

  Asha
   
 2. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii ni siasa safi kabisa wala usiwe na shaka dada Asha kuhusu kuondolewa hapa !

  Sidhani kama Dr. Slaa alisema uongo kuhusu hao mafisadi, na THEREFORE sidhani kama ze comedy wamesema uongo, ili kujua ukweli tuangalie pande zote mbili !

  Kama alikula pesa za walemavu sidhani kama siasa ataiweza, atakula hadi uji wa mgonjwa huyo Bunduki (Slaa)!
   
 3. Y

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 3,794
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao ze comedy 'watachuja' siku si nyingi......mie sioni haja ya kutoa malalamiko sehemu yeyote, kwani kama 'wamebugi' na watu wame-mind, basi ratings zao zitaporomoka na huyo Masanja itabidi arudi kwao huko 'swekeni' akalime. Mie nilidhani watoto wa mjini wana ganga njaa kumbe mazoba, yaani wanakubali kuwa "mules" wa mafisadi??? hii kweli aibu.
   
 4. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni vizuri lakini pia tuangalieni pande zote mbili, hata kama chizi lakini msikilizeni yoyote yule ! in this case, if we dont weigh in both sides then thats a clear sign of avoiding the truth !
   
 5. Y

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 3,794
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndio maana mie nimesema haina haja ya kulalamika sehemu yeyote, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwanyamazisha kitu ambacho kitakuwa sio fair........nikaongeza kwamba, kama wamekosea basi wataadhibiwa na wananchi wanaoangalia hicho kipindi!!!!. Nahisi overtime watalipa kwa kukurupuka kwao kitoto bila ku-research kwa kina juu ya U-alwatan wa wakina Slaa na hoja zao miongoni mwa wananchi!. Let's see...hiyo ndio Bongo ya Darisalame, kama sio wao watakao kuwa mdebwedo!!
   
 6. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yap ! right on ! lakini kama pesa za vilema zimeliwa bana mie hiyo sihusudu hata chembe yaani !
   
 7. Y

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 3,794
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama pesa za vilema zimeliwa haina haja ya makelele, wakawatafute watuletee na kutuonyesha.....kwamba hawa ndio vilema wenyewe!!! sio story tu za ma-comedian uchwara wa kibongo, ambao wanavuma tu kwasasa kama mvua za masika zisokuwa na wingu la kutosha!!!
   
 8. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  alaa ! kwa kuwa umeshajua vilema hawala sauti kubwa basi ndio unataka evidence, unajua how hard it is kuproove hilo jambo ? kama keshakula ameshakula hivyo na yeye Bunduki ( slaa ) siku si nyingi atachuja kama kweli alikula pesa za wanyonge. nani aliyekwambia wanasiasa ni wasafi ?
   
 9. Y

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 3,794
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  aah sheikh mbona maneno yako yanapandiana bwana?? mie sipo kwenye mood ya mijadala mirefu leo..........ma-friday haya na bootycall, sitaki nianze kuulizwa mbona upo serious namna hiyo!!???
   
 10. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sipo sillyass bana wee vipi.
   
 11. Y

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 3,794
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya sheikh.........weekend njema!!!!
   
 12. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haya ustadh !
   
 13. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,618
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Ninafikiri hapa hatuna haja ya kumwandama mtu, tujali hoja. kama hoja imetolewa na mtu mwenye mapungufu na ikaonekana ina faida kwa taifa, hatuna haja ya kumjadili mtoa hoja, bali hoja hiyo ijibiwe kwanza ndipo tuangalie mapungufu ya mtoa hoja.

  kinachoonekana sasa ni kutapatapa kwa viongozi wa ccm na serikali yake. lakini wenye akili tunajua nani ana hoja na nani anatapatapa. mfa maji haishi kushikilia hata majani akidhania ni tawi la mti.

  CCM wajibu hoja, wakishajibu, walete hiyo ya slaa na ushahidi wa kutosha mfano wa slaa aliyeanika peupee kila mtu anasoma ili nasi tuangalie huo upande wa pili, vinginevyo hizi ni ngonjera za majukwaani. watawapata wasio na ufahamu wa mambo na mashabiki wa ufisadi.
   
 14. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lakini kama utaangalia vizuri ni kwamba 99% ya hoja zoooote hapa JF zimelean upande mmoja ambao ni serikali/ccm,(kitu ambacho sio kibaya ) lakini pia tuangalie long term benefits kwa taifa letu, leo ccm kesho wapinzani, kabla hatujawachagua viongozi wapinzani kushika madaraka ni vizuri tukajua kama wamekula pesa za walemavu au la, na wao pia wajibu haya mambo, la sivyo wasipojibu na wakichaguliwa ni tutakuwa tumefanya KAZI BURE, kuchagua wale wale tunaowapinga waliopo madarakani ! leo wamekula pesa za walemavu kesho za walalahoi na za wagonjwa pia ! mwizi haibi mara moja akiiba mara moja basi huyo mdokozi !

  Dr. Bunduki itafaa kama akijibu hayo waliyosema ze comedy bana otherwise naye ananuka wizi tu kama hao anaowapigia kelele aka kama anayowaita wahujumu uchumi huku yeye kala pesa za walemavu * i will say kala pesa za walemavu as long as he doesnt answer these accusations*

  asanteni !
   
 15. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2007
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Sioni kama ni tatizo wala sishangai kwa ze comedy kuja na haya sababu hawa najua ni njaa tu ndio zinawafanya hata wasahau kuwa wanaharibu reputation waliokwisha jijengea kwa sababu ya kuganga njaa.
  Hata hivyo najua dhumuni lake ni ku-divert mjadala wa ufisadi na pia kupunguza uzito wake kisa eti mbona aliyezitoa yeye pia alikula pesa ya walemavu mara ooh alitembea na mwanamke,yaani tuache kujadili trilioni zilizodaiwa kuliwa na kikundi cha watu flani eti tuanze kumjadili Dr.slaa
  Washindwe wote wasio litakia mema taifa la Tanzania
   
 16. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,618
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Kada, what am saying, it is not wrong kumtuhumu slaa. lakini data ziko wapi? maana hizi pesa lazima zilikuwa na transaction zake, I meen lazima kuna records kwenye vitabu.

  ziletwe data watu wazijadili.
   
 17. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa ukiambiwa dr. slaa kafumaniwa, unataka ze datas tena ?
  kwi kwi kwi kwi kwi kwi ! mkuu hapa unanichekesha yaani hadi basi !
  kama alikula pesa za walemavu unataka data pia ? waliandikishana kwani ? hiyo ni tofauti na mkataba, ndio maana kitu kikatiwa mkataba, lakini you cant be a sillyass kuuliza data za hizo accusations !
   
 18. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unajua hii kitu inaweza kabisa ikawa njaa ndio maana wanasema, na kuna kipindi pia mrema alikuwa anapiga kelele weee wakawa wanasema njaa, njaa ! sasa huyo Dr. Bunduki hana njaa jamani ? kama mwenyekiti wake ana njaa, itakuwa yeye ? unajua dr. bunduki ni sawa na mtu na mke wake, anamwambia kapime ukimwi huku yeye kabaki nyuma, hataki ! nendeni mkapime wote muonekane wasafi then mambo mengine baadae, lakini kama Dr. Bunduki nae mchafu au wamemuaccuse then ajisafishe basi kwa kujibu hizo tuhuma !
   
 19. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,618
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Kwani walioliwa hizo pesa hawapo? au huyo mwanamke aliyefumaniwa naye hayupo?
   
 20. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyu Sekioni Kitojo ni yule aliye kuwa mtangazji wa RTD??
   
 21. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #21
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wamesema kwa niaba ya walioliwa ! kama watz walivyokuwa kimya juu ya mkataba!
   
 22. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #22
  Oct 12, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,751
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukihangaika na wanachosema ze comedy utajikuta unataka Kada mpinzani ajieleze kama ni kweli ameolewa na Karamavi...

  ze comedy wanadai kuwa kada ameolewa na Karamavi na wana mtoto mmoja anayekwenda kwa mccain kila wiki!...

  next week watadai pia kuwa kada ameolewa na muuaji dito....
   
 23. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #23
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyo huyo !
   
 24. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #24
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa hayo matusi ! admn. ebu angalia watu wanaotaka kuvuruga hoja za watu kwa manufaa yao !

  Mie sitojizibana tena na huyu mtoto ! fungia huyu kiumbe, anatukana hivi hivi mchana wote !
   
 25. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #25
  Oct 12, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,751
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poor thing!

  umeshaanza kulia tena!

  uliutaka ulimwengu wa ze comedy na umeupata!
   
 26. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #26
  Oct 12, 2007
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,394
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo Seki anaitwa Sekioni David, usimchanganye hata kidogo na mkongwe Sekioni Kitojo wa RTD.

  Kama Masanja kafanya hivyo kweli ni vibaya, lakini kuna mawili:
  1. Ama anachokoza apate reaction aitumie kwenye vipindi vijavyo (maana inabidi azalishe vipindi ili apate kula)
  1. Au kapewa kitu kidogo na hayo mafisadi, yana njia nyingi za kuvuruga mambo.

  Lipi kati ya hayo hapo juu ni la kweli? Tuvute subira tutajua hivi punde.
   
 27. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #27
  Oct 12, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 4,981
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wabongo wamelewa na ze comedy !
   
 28. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #28
  Oct 12, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo Sekioni atajwaye hapa si yule aliye kuwa mtangazaji wa RTD?
   
 29. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #29
  Oct 12, 2007
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,394
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siye hata kidogo. Huyu Seki ni bwana mdogo fulani ambaye mwanzoni alikuwa anaigiza na kina Bishanga Bashaija kwenye kipindi cha ITV kilichokuwa kinaitwa "Mambo Hayo". Siku hizi ni mtangazaji wa EATV.
   
 30. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #30
  Oct 12, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 4,085
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi serikali(waliotajwa) wangekuwa na evidence ya Slaa wangeshatoa kwenye magazeti, well labda wanacook up something...na kama hiyo hela ya walemavu aliyoila haina records then itakuwa ni hela ndogo sana kulinganisha na mabilioni yanayotafunwa kila siku(Wizi ni wizi kama kweli alikula basi itabidi naye atoe maelezo na ikiwezekana ashitakiwe)
   

Share This Page