S.Liondo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 3,408
- 1,712
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) visiwani hapa, kimetoa tamko rasmi kuhusu mchakato wa uundwaji wa katiba mpya, na kuweka bayana kuwa utaratibu wa zamani wa Rais wa Zanzibar kuwa Makanu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano urudishwe.
Hata hivyo, taarifa hiyo ilitolewa kwa tahadhari kubwa baada ya msemaji wa chama hicho kuwazungusha waandishi wa habari walioitwa Ofisi Kuu eneo la Kisiwandui tangu saa 5.00 asubuhi.
Katika hali ya kushangaza, Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu Zanzbar na Idara ya Itikadi na Uenezi, Issa Haji Ussi Gavu, aliingia ukumbini hapo akiwa amevalia kaunda suti ya bluu, huku akiwa hana kitu chochote mkononi na kuwaeleza waandishi kuwa kile walichokuwa wakiseme kimeahirishwa hadi wakati mwingine.Wakati wanahabari wakiwa kwenye mshangao huo, alikuja mmoja wa maafisa wa CCM na kuwaambia kikao kipo hivyo wasiondoke, ndipo baada ya dakika kama 10,Ussi alirudi tena akiwa amevalia sare za chama na kutoa taarifa hiyo.
Maoni yangu:
Kutokana na kipande hiki nilichokipata kutoka gazeti la Tanzania Daima toleo la leo, ni wazi kwamba ndani ya CCM kuna maoni yanayovutana kuhusu masuala ya Muungano. Kama maoni yangu ni sahihi, basi kuna hatari ya muungano huu kufia mikononi mwa CCM.