Zanzibar yatoa msimamo

S.Liondo

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,408
1,712
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) visiwani hapa, kimetoa tamko rasmi kuhusu mchakato wa uundwaji wa katiba mpya, na kuweka bayana kuwa utaratibu wa zamani wa Rais wa Zanzibar kuwa Makanu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano urudishwe.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilitolewa kwa tahadhari kubwa baada ya msemaji wa chama hicho kuwazungusha waandishi wa habari walioitwa Ofisi Kuu eneo la Kisiwandui tangu saa 5.00 asubuhi.

Katika hali ya kushangaza, Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu Zanzbar na Idara ya Itikadi na Uenezi, Issa Haji Ussi Gavu, aliingia ukumbini hapo akiwa amevalia kaunda suti ya bluu, huku akiwa hana kitu chochote mkononi na kuwaeleza waandishi kuwa kile walichokuwa wakiseme kimeahirishwa hadi wakati mwingine.Wakati wanahabari wakiwa kwenye mshangao huo, alikuja mmoja wa maafisa wa CCM na kuwaambia kikao kipo hivyo wasiondoke, ndipo baada ya dakika kama 10,Ussi alirudi tena akiwa amevalia sare za chama na kutoa taarifa hiyo.

Maoni yangu:
Kutokana na kipande hiki nilichokipata kutoka gazeti la Tanzania Daima toleo la leo, ni wazi kwamba ndani ya CCM kuna maoni yanayovutana kuhusu masuala ya Muungano. Kama maoni yangu ni sahihi, basi kuna hatari ya muungano huu kufia mikononi mwa CCM.

Mzanzibari atakapochaguliwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania..... makamu wa Rais atatoka upande wa bara (Tanganyika) ambayo haichagui Rais.... itakuwaje?

Hata hivyo, kama Muungano utaendelea kuwepo, naona bado upo umuhimu wa Rais wa zanzibar kutambuliwa kama makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano....... tutafute utaratibu ili kurudisha hadhi ya wazanzibari kwenye Muungano.
 
Muungano ukifa tu na Mapinduzi yanakufa. Muungano uliletwa na Mapinduzi. Hivi Dr Shein naye anaongoza SMZ au SUK? Baraza la Mapinduzi bado lipo? Lina akina nani?
 
Cheo cha makamo wa Rais ni cheo kilichobandikwa kinyume na mkataba wa makubaliano ya muungano. Hivyo cheo hicho kimewekwa kisiasa na sio kisheria.

lazima kuheshimu makubaliano yanu. na sio ujanja ujanja.
 
Mzanzibari atakapochaguliwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania..... makamu wa Rais atatoka upande wa bara (Tanganyika) ambayo haichagui Rais.... itakuwaje?

Hata hivyo, kama Muungano utaendelea kuwepo, naona bado upo umuhimu wa Rais wa zanzibar kutambuliwa kama makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano....... tutafute utaratibu ili kurudisha hadhi ya wazanzibari kwenye Muungano.

Unajua tunaweza tukawa hatuhitaji rais.
 
Mzanzibari atakapochaguliwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania..... makamu wa Rais atatoka upande wa bara (Tanganyika) ambayo haichagui Rais.... itakuwaje?

Hata hivyo, kama Muungano utaendelea kuwepo, naona bado upo umuhimu wa Rais wa zanzibar kutambuliwa kama makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano....... tutafute utaratibu ili kurudisha hadhi ya wazanzibari kwenye Muungano.

Itakuwa simple kabisa, kana rais akitoka zanzibar cha cha CUF basi makamo wake atatoka bara chana cha CUF pia! ITAFUTENI TANGANYIKA hizi confusion zitoweke!! Eeeee
 
Kuna mambo mengi ya ku consider kama tutaendelea na muundo huu wa serikali 2.

Kama Makamu wa Rais atakuwa Rais wa ZNZ

1.Je Rais wa JMT akitoka ZNZ ina maana Makamu wa Rais pia atakuwa Mzanzibari. Viongozi wote wakuu watatoka upande mmoja ya muungano.
2. Mathalani CDM ikashinda kiti ca U-Rais wa JMT na CUF ikashinda kiti cha Urais wa ZNZ, Je Rais wa CDM na Makamu wa Rais wa kutoka CUF watafanyaje kazi?
3. Rais aliyeko madarakani (JMT) akifariki wakati ameshatumikia nusu ya muhula wake hakuna uchaguzi Makamu wa Rais anakuwa Rais JMT. Je Watangayika tutakubali kuongozwa na Makamu wa Rais (Mnzazibari) aliyechaguliwa na watu laki 6 TU.

Lazima CCM wakubali Tatizo la Muungano ni Muundo serikali 2. Solution yake ni aidha kuwa na serikali moja au kuwa serikali tatu PERIOD.
 
nilisoma humuhumu upande wa Kenya kuwa Mombasa nao wanahitaji kurudi kuungana na wenzao (Zanzibar) hii nayo imekaaje.........?
 
Back
Top Bottom