Zanzibar: Waziri wa Fedha aelezea sakata la Mbunge Toufky Turky, asema amekamilisha kulipa ushuru wa Marcedes Benz G Wagon, ampongeza

Ntakufaaa nifufuke tena kwa mshtuko
Mkuu usiseme hivyo basi
Maana jana pension schemes karibu zi collapse ila tumeponea chuchupu
Pension schemes za bongo hizi wanazokulioa 33% halafu 66% wanakupa kwa style ya pension? Ni bora ukatengeneza michongo mingine ya mipunga uvute hiko chuma maana hapo kwa haraka haraka si chini ya 600m utahitaji kuilaza halafu umepaki zako mtoto anakuja kuichuna rangi na kisoda...🤣🤣🤣
 
Pension schemes za bongo hizi wanazokulioa 33% halafu 66% wanakupa kwa style ya pension? Ni bora ukatengeneza michongo mingine ya mipunga uvute hiko chuma maana hapo kwa haraka haraka si chini ya 600m utahitaji kuilaza halafu umepaki zako mtoto anakuja kuichuna rangi na kisoda...
Mkuu ya huko wala nisingeisubiri hata kama mfanyakazi wa serikali
Mimi niko nje na muanguko huo ni uk
Haha eti aichune na kisoda
Tena sio mtoto bali jitu zima kwa husda

Hilo ndinga la 2022 iliyotembea 1000km ni $800,000 ila mimi ntachukua la miaka 15 nyuma mzee
Sio mbaya na haikanyagi huko
 
Huyu mbunge Baba yake alikuwa ni mtu na nusu, Mzee Turky ndio alitowa pesa akiwa bungeni Dodoma Lisu akodiwe ndege kuwahishwa Nairobi, huyu mtoto Sasa figisu za Ccm wenzake hazijui hata hivyo alipe kodi, ameachiwa utajiri mkubwa sana zikiwemo boti za kisiasa za Dar Zanzibar.
Hakutoa fedha bali aliwadhamini kwa mali kauli.
 
Huyu mbunge Baba yake alikuwa ni mtu na nusu, Mzee Turky ndio alitowa pesa akiwa bungeni Dodoma Lisu akodiwe ndege kuwahishwa Nairobi, huyu mtoto Sasa figisu za Ccm wenzake hazijui hata hivyo alipe kodi, ameachiwa utajiri mkubwa sana zikiwemo boti za kisiasa za Dar Zanzibar.
Na hicho sasa cha kulipa gharama za ndege iliyombeba Lissu kwenda Nairobi, alandamwa mpaka umauti ukamfika.

Magufuli alikuwa ni SHETANI mwenye jicho Moja na pembe kichwani
 
Baada ya awali kuelezwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo mbioni kuuza mali za Mbunge Toufky Turky ambaye ni Mfanyabiashara aliyedaiwa kushindwa kulipa ushuru wa Gari aina ya Marcedes Benz G Wagon aliloliingiza Nchini Januari 2022, fafanuzi umetolewa.

Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya amenukuliwa na Clouds FM kuwa tayari deni hilo limekamilishwa kulipwa huku akitolea ufafanuzi kilichotokea.

Zanzibar waelezea
Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Juma Mwenda amesema “Kampuni yake (Mbunge Turky) ilikuwa inadaiwa hiyo kodi, alitegemea apate msamaha lakini hakuupata, msamaha alioomba upo chini ya mamlaka ya Waziri.

“Gari hilo (Marcedes Benz G Wago) lililetwa na kwa matumizi ya Kampuni na si matumizi ya Mbunge na ndiyo lilikuwa likiombewa msamaha, lingekuja kwa jina la Mbunge kuna taratibu zake za msamaha ambazo angezitumia kwa ajili ya msamaha.”

Kuhusu tofauti ya kodi ya Bara na Zanzibar, amesema Mwenda amesema “Tofauti ipo lakini huwa ni kwa magari yaliyotumika, hili linalohusika hapa ni jipya, lilikuja likiwa jipya, hivyo lilitaiwa kulipiwa ushuru sambamba na ule unaolipwa Tanzania Bara.

“Utaratibu ulivyo ni kuwa endapo kutakuwa na kodi inadaiwana na haijalipwa mali ya mhusika inaweza kukamatwa na kupigwa mnada.

Kuhusu mali za Mbunge kupigwa mnada
“Hivyo, mali za hiyo kampuni ya Mbunge hazikuwa zimepigwa mnada, lakini hiyo ni option ambayo ingefikiwa ikiwa kodi isingelipwa.”

Kuhusu madai kuwa gari hilo limetangazwa kupigwa mnada, amesema “Kama kuna mazingira ya mlipa kodi ameomba kulipa kidogo kidogo hayo yanaheshimiwa na anapewa nafasi hiyo.

“Wanaoamua kuhusu msamaha ni Waziri wa Fedha kwa kufuata ushauri wa taasisi inayosimamia uwekezaji, baada ya hapo mamlaka ya mapato inapewa maagizo ya utekelezaji.”

Waziri afafanua
Akizungumzia sakata hilo, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya akasema “Utaratibu ambao umetumika kuleta hilo gari ni za uwekezaji wakati wa ujenzi, mfano linaweza kutumika kurahisha ujenzi.

“Wakati hilo gari limekuja mradi ulikuwa umeshakamilika, hivyo mwanzoni Sheria zikawa haziruhusu kwa kuwa muda ulikuwa umeshapita.

“Hapa Zanzibar ukiingiza gari kwa matumizi yako ya kawaida, utaratibu upo wa kulifanyia tathmini ili kuendana na mazingira ya Zanzibar, kama tunavyojua uchumi wa hapa ni tofauti, lengo ni kuwawezesha Wananchi kujikimu na kununua magari.

“Ndio maana (Mbunge) alipofanyiwa tathimini ikaja ile ambayo aliambiwa.”

Alipoulizwa suala la Mbunge Turky kulipa kodi kidogokidogo, kwanza alipongeza uwekezaji wa Turky katika kiwanda cha mifuko na akajibu kwa ujumbe wa maandishi kuwa tayari Mbunge huyo ameshakamilisha kulipa.

Thamani ya gari
Gari hilo lenye thamani ya Dola za Marekani 214,668.71 (Tsh. 498,462,891), liliingizwa kupitia bandari ya Malindi na kampuni ya uwakala wa mizigo ya Kimataifa HT Motors Group LTD (UK) kwa kushirikiana na kampuni ya uwakala wa mizigo ya ZARA Freight Forwaders ya Malindi, Zanzibar.

Chanzo: Clouds FM

Pia soma: TRA yaendelea kumkaba koo Toufiq Salum Turky kodi ya gari milioni 308.5
Tshs 498,462,891 ndo ilete kodi 308,500,000? Mbona kama kuna kitu sikielewi hapa?

Hii nchi inanyonga sana uchumi wa raia wake. Jasho la mtu lakini serikali INAKWAPUA zaidi ya 40% ya jasho hilo.

Ndo maana CCM haitoki madarakani kwa sababu viongozi wake wanaficha siri kubwa ya unyonyaji wanaoufanya kupitia sheria walizozipitisha wao
 
Tshs 498,462,891 ndo ilete kodi 308,500,000? Mbona kama kuna kitu sikielewi hapa?

Hii nchi inanyonga sana uchumi wa raia wake. Jasho la mtu lakini serikali INAKWAPUA zaidi ya 40% ya jasho hilo.

Ndo maana CCM haitoki madarakani kwa sababu viongozi wake wanaficha siri kubwa ya unyonyaji wanaoufanya kupitia sheria walizozipitisha wao
Ndio sababu magari mapya na mazuri yananunuliwa na serikali tu.
 
Tshs 498,462,891 ndo ilete kodi 308,500,000? Mbona kama kuna kitu sikielewi hapa?

Hii nchi inanyonga sana uchumi wa raia wake. Jasho la mtu lakini serikali INAKWAPUA zaidi ya 40% ya jasho hilo
Hiyo Kodi ni almost 62% 🙄
 
Mkuu ya huko wala nisingeisubiri hata kama mfanyakazi wa serikali
Mimi niko nje na muanguko huo ni uk
Haha eti aichune na kisoda
Tena sio mtoto bali jitu zima kwa husda

Hilo ndinga la 2022 iliyotembea 1000km ni $800,000 ila mimi ntachukua la miaka 15 nyuma mzee
Sio mbaya na haikanyagi huko
Kodi TZ ni sawa na lile onyo la Mmakonde "uchiteme, uchimung'unye, wala uchimeche. Uchitema nchale, uchumungunya nchale, na uchimecha nchale". Ukileta mpya kodi juu. Ukileta nzee unalipa kodi za kawaida za thamani ya gari na unaongezewa kodi nyingine ya uchakavu. Hakwepi ntu hapo.
 
Waziri alionesha msimamo mzuri sana kwenye hili suala, hasa kwenye sababu alizotoa za kukataa msamaha wa kodi ulioombwa na huyo mbunge, nampongeza.

Naamini maelezo aliyotoa waziri ni sahihi na hapakuwepo na kimemo toka juu kumtaka afanye hivyo, hili taifa lazima liende na standard ya aina hii, tuache kujuana na kuishi kwa mazoea ya masikini pekee ndio wakulipa kodi
Full of doubts
 
Kodi TZ ni sawa na lile onyo la Mmakonde "uchiteme, uchimung'unye, wala uchimeche. Uchitema nchale, uchumungunya nchale, na uchimecha nchale". Ukileta mpya kodi juu. Ukileta nzee unalipa kodi za kawaida za thamani ya gari na unaongezewa kodi nyingine ya uchakavu. Hakwepi ntu hapo.
Tatizo hakuna ajira za kuingiza kipato na kodi serikalini
Ubunifu zero na elimu zero pia

Shahada zao za kukariri hapo serikali na wasomi hawachekani na wanabaki kutafuta hela kwa nguvu kama bandarini na hata tozo za kila aina

Tuliaminishwa na yule jamaa kuwa kuna viwanda kila kona ila hatujasikia wafanyakazi wa hivyo viwanda wanalipa kodi kiasi gani na wamefanikiwa na nini

Vijana nao wamekuwa kama disabled tu
 
Back
Top Bottom