Zanzibar: Marufuku kucheza kwa kulowanisha nguo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Serikali ya Zanzibar kupitia Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni imepiga marufuku mtindo wa Wanawake kulowesha kwenye maji nguo walizovaa na kisha kucheza nazo mziki kama ambavyo imekua ikifanyika kwenye baadhi ya sherehe ama mikusanyiko.

Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt.Omar Adam amesema haya leo akihojiwa na ZBC kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Sanaa na Filamu na namna wanavyosimamia Mila, Desturi na Utamaduni wa Zanzibar.

"Zanzibar kwa siku moja huwa kuna shughuli 50 hadi 100 hatuwezi kuzuia hilo, hatujapiga marufuku kupiga muziki bali kupiga muziki kwa sauti iliyopitiliza na kucheza muziki kwa mitindo isiyofaa na inayopingana na desturi za Zanzibar hasa huu mtindo wa wakina Dada kucheza kwa kulowesha nguo maji, ni marufuku na Askari wana ruhusa ya kuwakamata”



Pia soma:
Marufuku nyingine Zanzibar soma:

Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika

 
Mtapiga marufuku mpaka mchoke, watu na maisha yao.
 
So kama wakiwa wanacheza mziki then mvua ikawanyeshea wanakamatwa, au pia hawaruhusu watu kucheza kwenye mvua

Zanzibar bhana
 
Na bara pia I've huku
Maana huku sahv ni kama
Sodoma na gomora

Ova
 
viongozi wa ccm mambo ya ni ovyo kabisa, badala kutafuta mambo ya msingi wapo bzy wanachokonoa privacy za watu.
 
Back
Top Bottom